Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kitu najutia ni kusoma chuo na life la chuo kwani nilikutana na maisha ya ovyo kabisa mazila ya kila aina nimegombana na watu wa karibu nimejuana na watu wengi hawana msaada .Nimekutana na watu wabaguzi

Yaani daily nilitamani kumaliza nihame baada ya kumaliza nikaondoka hata mwezi sijakaa nikapata mishe nikarudishwa tena huku dar nakutana na watu wale wale yaani sipendi nimeandika barua nihame mji imeshindikana

Group la chuo nilileft kitambo tangu mwaka wa pili ikawa nawasiliana na CR maana mtu wangu wa karibu sana.
 
Dah yule demu falansana kaniunganisha kwenye grid ya taifa[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]hapa ni kuishi kwa matumaini tuu
Duh pooole mkuu...kama uko serious lakini[emoji848]
 
Hela ndio ilikua motivation. Siwezi kuingia kwenye msala kama hakuna Chambi kidogo. Toka nikiwa mdogo kuna Mentality fulani Mother alikua anaijenga kichwani kwangu kila nikifanya kosa..

Mara nyingi alikua ananiambia "Wewe umefanya kitu flani umekamatwa, umechapwa sasa kilikua kinakusaidia nini hata kama usingedakwa?"

Kwaiyo ni kama alikua ananiambia niweke kila tukio kwenye uzani (balance) na faida nayopata kabla sijalifanya. Kama hakuna faida nitakayopata nikifanya tukio fulani ni bora niachane nalo tu maana its not worth it!

Kwaiyo ilikua nikisha calculate faida nayopata, nina jump-in chap sana, bila ku evaluate risks ndio maana nikawa nafeli, LOL
Hapo nimejifunza kitu mkuu big up sana
 
Niliiba Matofali ya mwalimu Nyerere palee mwitongo wkt huo nikiwa na Mjomba wangu!!ila mjomba ndo aliniingiza mkenge Basi bana askari ana akili sana alijifanya haja tuona kabisaaa!!..... tukaenda tukarudia mara kibao!! kwa akili za utoto nilidhani ni kawaida.

kuumbe mwenzngu yule anaiba na mie namsaidia kuiba!! ........na uzuri ni kwamba Julius alikuwepo wakati huo!!! ...akatukamata kiulainiiii!!

tukapelekwa kwa julius Live.......mengi yalifanyika pale .........ila yule Mzee alikuwa ni wa ajabu sana narudia tena, sijakosea alikuwa wa ajabu mnoooo sana tuuu!!... .......lkn to cut long story short ndo ukawa mwanzo wa mie kusaidiwa shule tena nzuri sana abroad nilishangaa mpaka leo hapa nilipo bado nashangaa!! ......na marehemu kazi hii ilifanywa na Rais huyo huyo!..... hapo ni kwa kifupi sana nimeitoa hii!
 
[emoji38][emoji38][emoji38] inafurahisha na kusikitisha at the same time. Vipi magodoro ulilipa?
Magodoro hatukulipa maana headmaster ndo alikua na list ya majina yetu Kwahyo kile kipindi cha kuchukua result slip kilipofika alikua anauguza mkewe ambaye anaishi wilaya nyingine

Kwahyo hakuwepo shule na shule ikawa chini ya academic master kwa kipindi ambacho headmaster hayupo Kwahyo academic master akagawa tu result slip maana kwa wahuni naskia headmaster ali mind kinyama alivorudi kakuta watuhumiwa tushachukua Mali [emoji23][emoji23]
 
And Another!

Katika harakati za kutafuta Ugali nilijikuta nimeomba kujiunga na jeshi la JKT. Nikatupiwa Kigoma, kule Bulombora 821KJ.

Nikapigishwa jaramba na kulishwa vumbi la kutosha huku nikitazama ziwa Tanganyika kwa ukaribu kabisa lililozungukwa na mawese ya kushato. Ruka Juu, Kanyaga Chini kwa nguvu mpaka mguu utoke nje ya kiatu.

Mikesha ilivyozidi nikaona hapa nitakufa. Nikaanza harakati za kutafuta nafasi ya kulala vizuri maana zile Dakika 5 unazopewa za kulala hazitoshi kabisa. Nikaanza kutafuta machimbo. Wenzangu wakienda mkesha, mimi najipeleka porini. Siku nyingine nakutana na ma afande na wao wamedoji kwenda lindo wananitimua najikuta nimerudi kulala uvunguni.

Tabia yangu ya kujizoesha kulala ikaanza kunigharimu. Ikafika mahali nikawa siwezi kabisa kwenda kukesha hata siku moja. Nikaanza kuona hadi uvivu wa kwenda kulala mbali na anga letu. Nakumbuka nilikua Eagle Coy.

Siku hiyo nimelala uvunguni nakoroma kabisa, saa ngapi afande asiingie ndani kutafuta watoro. Si akaniskia navyokoroma kule chini ya kitanda. Dah sitasahau hiyo kipigo niliyopewa. Nakumbuka al manusura nipoteze jicho. Maana vile vitanda vimechomelewa kwaiyo kuna kama vichuma flani hivi kama nondo vimejitokeza kwa juu, alinibamiza kichwa kwenye kile kitanda ile nondo ikachubua kidogo pembeni ya jicho.

Sijui nilipata wapi ujasiri nikamsukuma pembeni nikasogeza kioo cha dirisha nikarukia nje nikaanza kukimbia huku nachechemea machozi yananitoka ya kutosha. Jamaa nadhani aliniangalia navyokimbia kwa tabu akanionea huruma akaamua kuachana na mimi huku akisema "Nitakuua Mbwa Wewe".

Nilivyofika walipo wenzangu kwenye mkesha nikapokelewa tena na adhabu za kubiringita na kukwepa ndege za kivita. Dah.. nilihisi mwisho wangu umefika, nikasema kwa sauti "Nakufa" huku machozi yanatoka ili hata jamaa anionee huruma lakini wapi. Yeye kakazana kunioshea na kunifanya mfano kwa wengine. Saiyo pumzi imekata, maumivu kila mahali, machozi yameshatoka mpaka yamekauka, siwezi kuongea tena. Ni kwa Neema za Allah pekee nilifanikiwa kuona tena Jua siku iliyofuata maana nilikua nahisi kabisa nakufa. Hali yangu ilikua mbaya sana!

Sikuwahi kujuta kwenye maisha yangu kama hiyo siku. Nililaani uamuzi wangu wa kwenda huko. Kile kitu kilinikaa sana moyoni kwa muda mrefu. Niliona kabisa huku sio kwangu. Course ilivyoisha, wakati wengine wanasikilizia kwenda JWTZ na Polisi, mimi nikaandaa nauli yangu, nikavizia ule muda tunaotumwa kwenda town...nikatorokea huko mazima na nikaapa sitarudi tena. Ikawa imeisha hiyo!

Kwa kweli mambo ya Jeshi yana watu wake. I was not one of them!
[emoji1][emoji1][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji1]nilikataa mwanzoni kabisaa siwezi

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Kuna mchezaji mmoja wa polisi Tanzania alikuwa anahojiwa kwenye soka kijiweni akasema ukimuona mtu amevaa gwanda la jeshi muheshimu sana maana yeye na wenzake walikimbia baada ya kupigishwa tizi la kufa mtu sema nimemsahau jina lake .
 
[emoji16][emoji16][emoji16]Ntakuua mbwa wewe,shenzi kabisa yani umeumia bado unatukana afande
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua,,,, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp
Polee broo hii issue inaniumiza sana hata mimi

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kitu najutia ni kusoma chuo na life la chuo kwani nilikutana na maisha ya ovyo kabisa mazila ya kila aina nimegombana na watu wa karibu nimejuana na watu wengi hawana msaada .Nimekutana na watu wabaguzi

Yaani daily nilitamani kumaliza nihame baada ya kumaliza nikaondoka hata mwezi sijakaa nikapata mishe nikarudishwa tena huku dar nakutana na watu wale wale yaani sipendi nimeandika barua nihame mji imeshindikana

Group la chuo nilileft kitambo tangu mwaka wa pili ikawa nawasiliana na CR maana mtu wangu wa karibu sana.
Babuu kuna tukio ulipiga bila shakaa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ni mengi sana kwanza washkaji tulitoka advance tukaaa getto moja tulikuwa tunapendana ila tuligombana yaani mikosi mpaka leo hatuko pamoja

Mwanangu mmoja alikuwa mtu wa karibu alitaka kujiua kisa kuachwa na demu wake na kuolewa akadisco nikawa sina mtu was karibu na alivyodisco akarudi kwao mbeya yaani balaa

Mpaka nafika mwaka wa tatu crew yetu niliku2a alone na getto naishi mwenyewe hamna sapot wau tumegombana wengine wamecarry yaani mpaka 🎓 graduation hakuna Ile hamsha hamsha
Babuu kuna tukio ulipiga bila shakaa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile ap
 
Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six

Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa

Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)

Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)
Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea

Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani

Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana

Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform

Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika
Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)

Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa

Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
Asee nimecheka mpaka mbav zimeumaa

Back
Top Bottom