Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Nisaidie kumuongezea[emoji23][emoji23]Mjita anastahili tusi la ziada[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nisaidie kumuongezea[emoji23][emoji23]Mjita anastahili tusi la ziada[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Deejay waleteeeeeAnd Another...
Nimepambania kombe huku na kule Mil 3 hizi hapa. Nawaza sasa pa kuzipeleka ili mtonyo uongezeke. Mishe zilizopo mezani wakati huo zimebana sana. Kwaiyo kusema niende nikafanye kilimo au nifungue biashara mahali itakua changamoto kidogo kwenye kufuatilia.
Napita pita social media [wakati huo facebook ni moto sana sio kama saivi] nakutana na habari za kudownload pesa kwa mara ya kwanza; mambo ya cryptocurrency na forex. Nikawa interested. Nikaanza kufuatilia kwa ukaribu nikagundua kuna jamaa mmoja mkenya anasaidia watu ambao hawana uzoefu wa ku trade then baadae mnagawana faida.
Mshenzi yule alikua amejipanga. Alikua hadi ana post video za watu mbali mbali wanaotoa ushuhuda namna jamaa alivyo wasaidia na kubadilisha maisha yao. Duh, nikaona mtonyo si ndio huu sasa. Na hivi sina muda mishe kama hizi za kimtandao ndio zenyewe. Namalizia kila kitu kwenye simu. Sasa nikapiga mahesabu wale watu ninao waona kwenye clips hawakua hata na cha kuanzia kikubwa na sasahivi maisha yao yamebadilika, Je mimi mwenye Mita 3? Si ndio na kazi nitaacha kabisa. Nikaona hii ni fursa ngoja nim.dm mwamba.
Jamaa alikua Active sana. Akanitumia magazeti kadhaa ya kupitia ili nielewe namna utaratibu mzima unavyoenda. Nikayasoma yote nikawa nimeelewa. Maskini mtoto wa watu kumbe naingizwa mjini hata sielewi.
Nakumbuka alini.introduce kwenye platform moja inaitwa coinxtrading au paxel kama sikosei. Una create account unaweka details zako personal mpaka bank Account No. zako. Then kianzio cha chini ni USD 100, wakati huo ilikua kama laki 2 kasoro hivi, sikumbuki vizuri exchange rate ya siku hiyo. Mwamba nikatupia Dollar zangu 100.
Hiyo system ukishajisajili lazima umchague jamaa kama meta trader wako unayemuamini. Kwaiyo akaniambia jina la kuchagua pale nikamchagua chap kazi ikaanza.
Mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya kama siku mbili naingia kwenye system, nakuta mtonyo unasoma USD 400. Nikasema mambo si ndio haya sasa. Unaingiza Dollar 300 ndani ya masaa 48 tu, tena hata sijatoka Jasho. Ewaaa nimeulaaa huku nikicheka kitajiri. Sikujua kitakachonikuta..
Siku moja baada ya kuona ile $400, jamaa akanicheck inbox. Akaniambia mambo yanaenda vizuri kwaiyo nimtumie commision yake ya $150 maana tunagawana faida. Nikamwambia toa tu hapo kwenye hiyo iliyopatikana kwenye mfumo. Akasema niache ujinga kwa sababu nikipunguza pesa ya kwenye system itabidi nianzie chini tena. Wakati nikiacha hiyo $400 aka trade itaongezeka haraka zaidi. Akanipa ka somo nikamuelewa.
Basi nikaenda Bank nikafanya niliyotakiwa kufanya jamaa akapata pesa zake. Akaendelea kutrade.
To cut a long story short;
Kuna muda ilifika hadi $3000. Akawa ameniambia nimpe faida yake then anifanyie namna nitoe pesa zangu. Yule Mbwa sijui alinusa harufu kuwa nitamsanukia maana nilikua kama nimeshachoshwa na hizo habari za niache hela kule kwenye mfumo hadi zijae jae.
Nakumbuka kuna kipindi nilijaribu ku withdraw ikawa inagoma. Jamaa akaniambia siwezi ku withdraw bila yeye kunisaidia. Kana kwamba kuna process kidgo za kupitia mpaka pesa itoke. Daah nilitakiwa nikimbie haraka sana baada ya kuambiwa hivyo ila tamaa zikanifanya nimuamini ki bloody f*cking sana.
Baada ya kumtumia commision yake ya kitu kama $1200, dana dana zikaanza. Hapo karibu hela yote ameshachukua. Nimebaki na kama laki 2 tu kwenye ile Mil 3 niliyokua nayo. Sasa akili ndio zikaanza kurudi. Alivyoona kila anavyoniletea story za kuendelea kutrade nagoma, na ninachotaka ni kuwitthdraw tu pesa.. akaniblock. Sijakaa vizuri nikawa logged out kwenye system. Aiseee
Niliumia sana. Nulijuta kuamini watu ki rahisi rahisi. Nilihangaika sana ku log in lakini wapi. Tukana sana jamaa inbox lakini wapi. Pesa imekwenda na maji. Hairudi tena. 3M niliyoitesekea zaidi ya mwaka is gone tena ndani ya wiki mbili tu. Nilikua depressed sana. Nikaona hii aibu siwezi hata kushirikisha wenzangu. Nikachukua leave nikaomboleze kidogo nyumbani.
Hapa nilijifunza kitu kuhusu utapeli. Nika recover, maisha yakaendelea [emoji1491]
Ukiona unalazimishiwa sana fursa, ujue wewe ndiyo fursa yenyewe.
Ivi sisi watoto wa kiume na uwizi qu udokozi uko kwenye damu nn?Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).
Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri. Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.
Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni. Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii. Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.
Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.
Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.
Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale. Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.
Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Mkuu wapi ulielezea weka link[emoji3][emoji3][emoji3]Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).
Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri. Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.
Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni. Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii. Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.
Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.
Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.
Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale. Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.
Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Wami wamekufa wengi pale yni ukipita pale lazima mwili usisimkeWajuba mimi sintokaa nisahau kipind nasoma O level ilikua form 3 kama sikosei shule ilikua ya day....
Kuna Mdau mmoja kitaa alikua anataka vipande vya nondo kutokana na pale shule kulikua kuna gorofa afu kashanitangazia dau kwa hio ilitakiwa nichukue zile za kusukia nguzo..
Sasa nilikua na kawaida ya kutoroka shule na tulikua na teacher mmoja mpare alikua second master mnoko kinoma noma na mateacher wa enzi hizo walikua wanatutembezea mboko balaa...
Sasa ile nimeenda nikabeba vipande vyangu vine vya nondo nikawa nakatiza njia ambayo ipo karibu na toi za mateacher mara paaap bin Vup yule mpare Huyu hapa mbele yangu.. Akaniuliza unapeleka wapi hivi vipande? Dah nilihis mkojo unatoka huyo akanipeleka hadi kwa headmaster.. Nikampiga kiswahili headmaster hanielew... Duh sitakaa nisahau yani mikono jasho mdomo kigugumizi mate mazito mdomoni
akaniambia njoo kesho na mzazi afu dingi kavu kinoma yani unataman usiingie anga zake anakupiga kama punda na haangalii pa kupiga..
Kesho yake sikwenda shule wala sikumwambia baba nikaamka mapema poriniii... nikawa narud ucku..
Kiufupi kilichonisaidia yule headmaster alianza kuugua na mkewe akafa akawa yuko bize kulea wanae ila shuleni niliishi kama digdigi mbele ya simba pared hupatamani class asiingie headmaster so niliuskip msala kwa utoro na mwisho nae alikufa kwa ajali ya basi pale Wamii ila bada ya mm kumaliza shule ..
😂😂😂 pole sana na hongera sana mkuu. Kwa kuchagua njia yako ila nimeona tu, watu wanatoka mbali. Tusichukuliane poa!!And Another!
Katika harakati za kutafuta Ugali nilijikuta nimeomba kujiunga na jeshi la JKT. Nikatupiwa Kigoma, kule Bulombora 821KJ.
Nikapigishwa jaramba na kulishwa vumbi huku nikitazama ziwa Tanganyika kwa ukaribu kabisa lililozungukwa na mawese ya kutosha. Ruka Juu, Kanyaga Chini kwa nguvu mpaka mguu utoke nje ya kiatu.
Mikesha ilivyozidi nikaona hapa nitakufa. Nikaanza harakati za kutafuta nafasi ya kulala vizuri maana zile Dakika 5 unazopewa za kulala hazitoshi kabisa. Nikaanza kutafuta machimbo. Wenzangu wakienda mkesha, mimi najipeleka porini. Siku nyingine nakutana na ma afande na wao wamedoji kwenda lindo wananitimua najikuta nimerudi kulala uvunguni.
Tabia yangu ya kujizoesha kulala ikaanza kunigharimu. Ikafika mahali nikawa siwezi kabisa kwenda kukesha hata siku moja. Nikaanza kuona hadi uvivu wa kwenda kulala mbali na anga letu. Nakumbuka nilikua Eagle Coy.
Siku hiyo nimelala uvunguni nakoroma kabisa, saa ngapi afande asiingie ndani kutafuta watoro. Si akaniskia navyokoroma kule chini ya kitanda. Dah sitasahau hiyo kipigo niliyopewa. Nakumbuka al manusura nipoteze jicho. Maana vile vitanda vimechomelewa kwaiyo kuna kama vichuma flani hivi kama nondo vimejitokeza kwa juu, alinibamiza kichwa kwenye kile kitanda ile nondo ikachubua kidogo pembeni ya jicho.
Sijui nilipata wapi ujasiri nikamsukuma pembeni nikasogeza kioo cha dirisha nikarukia nje nikaanza kukimbia huku nachechemea machozi yananitoka ya kutosha. Jamaa nadhani aliniangalia navyokimbia kwa tabu akanionea huruma akaamua kuachana na mimi huku akisema "Nitakuua Mbwa Wewe".
Nilivyofika walipo wenzangu kwenye mkesha nikapokelewa tena na adhabu za kubiringita na kukwepa ndege za kivita. Dah.. nilihisi mwisho wangu umefika, nikasema kwa sauti "Nakufa" huku machozi yanatoka ili hata jamaa anionee huruma lakini wapi. Yeye kakazana kunioshea na kunifanya mfano kwa wengine. Saiyo pumzi imekata, maumivu kila mahali, machozi yameshatoka mpaka yamekauka, siwezi kuongea tena. Ni kwa Neema za Allah pekee nilifanikiwa kuona tena Jua siku iliyofuata maana nilikua nahisi kabisa nakufa. Hali yangu ilikua mbaya sana!
Sikuwahi kujuta kwenye maisha yangu kama hiyo siku. Nililaani uamuzi wangu wa kwenda huko. Kile kitu kilinikaa sana moyoni kwa muda mrefu. Niliona kabisa huku sio kwangu. Course ilivyoisha, wakati wengine wanasikilizia kwenda JWTZ na Polisi, mimi nikaandaa nauli yangu, nikavizia ule muda tunaotumwa kwenda town...nikatorokea huko mazima na nikaapa sitarudi tena. Ikawa imeisha hiyo!
Kwa kweli mambo ya Jeshi yana watu wake. I was not one of them!
😂😂😂 mzee wa vipande vya nondoWajuba mimi sintokaa nisahau kipind nasoma O level ilikua form 3 kama sikosei shule ilikua ya day....
Kuna Mdau mmoja kitaa alikua anataka vipande vya nondo kutokana na pale shule kulikua kuna gorofa afu kashanitangazia dau kwa hio ilitakiwa nichukue zile za kusukia nguzo..
Sasa nilikua na kawaida ya kutoroka shule na tulikua na teacher mmoja mpare alikua second master mnoko kinoma noma na mateacher wa enzi hizo walikua wanatutembezea mboko balaa...
Sasa ile nimeenda nikabeba vipande vyangu vine vya nondo nikawa nakatiza njia ambayo ipo karibu na toi za mateacher mara paaap bin Vup yule mpare Huyu hapa mbele yangu.. Akaniuliza unapeleka wapi hivi vipande? Dah nilihis mkojo unatoka huyo akanipeleka hadi kwa headmaster.. Nikampiga kiswahili headmaster hanielew... Duh sitakaa nisahau yani mikono jasho mdomo kigugumizi mate mazito mdomoni
akaniambia njoo kesho na mzazi afu dingi kavu kinoma yani unataman usiingie anga zake anakupiga kama punda na haangalii pa kupiga..
Kesho yake sikwenda shule wala sikumwambia baba nikaamka mapema poriniii... nikawa narud ucku..
Kiufupi kilichonisaidia yule headmaster alianza kuugua na mkewe akafa akawa yuko bize kulea wanae ila shuleni niliishi kama digdigi mbele ya simba pared hupatamani class asiingie headmaster so niliuskip msala kwa utoro na mwisho nae alikufa kwa ajali ya basi pale Wamii ila bada ya mm kumaliza shule ..
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).
Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri. Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.
Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni. Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii. Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.
Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.
Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.
Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale. Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.
Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] haya Mambo banana mm nimewahi doji pindi wenzangu wanagawia full kombati- ile ya karanga kilichonipata hiyo siku najutaaaAnd Another!
Katika harakati za kutafuta Ugali nilijikuta nimeomba kujiunga na jeshi la JKT. Nikatupiwa Kigoma, kule Bulombora 821KJ.
Nikapigishwa jaramba na kulishwa vumbi huku nikitazama ziwa Tanganyika kwa ukaribu kabisa lililozungukwa na mawese ya kutosha. Ruka Juu, Kanyaga Chini kwa nguvu mpaka mguu utoke nje ya kiatu.
Mikesha ilivyozidi nikaona hapa nitakufa. Nikaanza harakati za kutafuta nafasi ya kulala vizuri maana zile Dakika 5 unazopewa za kulala hazitoshi kabisa. Nikaanza kutafuta machimbo. Wenzangu wakienda mkesha, mimi najipeleka porini. Siku nyingine nakutana na ma afande na wao wamedoji kwenda lindo wananitimua najikuta nimerudi kulala uvunguni.
Tabia yangu ya kujizoesha kulala ikaanza kunigharimu. Ikafika mahali nikawa siwezi kabisa kwenda kukesha hata siku moja. Nikaanza kuona hadi uvivu wa kwenda kulala mbali na anga letu. Nakumbuka nilikua Eagle Coy.
Siku hiyo nimelala uvunguni nakoroma kabisa, saa ngapi afande asiingie ndani kutafuta watoro. Si akaniskia navyokoroma kule chini ya kitanda. Dah sitasahau hiyo kipigo niliyopewa. Nakumbuka al manusura nipoteze jicho. Maana vile vitanda vimechomelewa kwaiyo kuna kama vichuma flani hivi kama nondo vimejitokeza kwa juu, alinibamiza kichwa kwenye kile kitanda ile nondo ikachubua kidogo pembeni ya jicho.
Sijui nilipata wapi ujasiri nikamsukuma pembeni nikasogeza kioo cha dirisha nikarukia nje nikaanza kukimbia huku nachechemea machozi yananitoka ya kutosha. Jamaa nadhani aliniangalia navyokimbia kwa tabu akanionea huruma akaamua kuachana na mimi huku akisema "Nitakuua Mbwa Wewe".
Nilivyofika walipo wenzangu kwenye mkesha nikapokelewa tena na adhabu za kubiringita na kukwepa ndege za kivita. Dah.. nilihisi mwisho wangu umefika, nikasema kwa sauti "Nakufa" huku machozi yanatoka ili hata jamaa anionee huruma lakini wapi. Yeye kakazana kunioshea na kunifanya mfano kwa wengine. Saiyo pumzi imekata, maumivu kila mahali, machozi yameshatoka mpaka yamekauka, siwezi kuongea tena. Ni kwa Neema za Allah pekee nilifanikiwa kuona tena Jua siku iliyofuata maana nilikua nahisi kabisa nakufa. Hali yangu ilikua mbaya sana!
Sikuwahi kujuta kwenye maisha yangu kama hiyo siku. Nililaani uamuzi wangu wa kwenda huko. Kile kitu kilinikaa sana moyoni kwa muda mrefu. Niliona kabisa huku sio kwangu. Course ilivyoisha, wakati wengine wanasikilizia kwenda JWTZ na Polisi, mimi nikaandaa nauli yangu, nikavizia ule muda tunaotumwa kwenda town...nikatorokea huko mazima na nikaapa sitarudi tena. Ikawa imeisha hiyo!
Kwa kweli mambo ya Jeshi yana watu wake. I was not one of them!
Ujana + utoto una mengi sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI
Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.
Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.
Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro[emoji2955][emoji2955][emoji2955].
Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.
Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.
Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.
Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.
Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91].
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.
Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.
Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.
Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.
Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.
Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.
Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.
yaani wewe ni mi mi kabisa mkuu-mimi jana tu nimetoka kuwakiana na mmoja hapo Bungoni....kila kitu nalipa kuanzia ada,nguo,sikukuu,chakula etc,..halafu anawapigia simu rafiki zangu eti sihudumii mtoto.Najutia sana kuwazalisha wadada. Sasa hivi maisha yananiendea kombo yaani niko na familia yangu lakini utasikia unapigiwa simu mara mwanao anaumwa mara ada. Yaani hata mke wangu hayuko comfortable na masimu simu.
Kuna siku aliniambia yani ungeniambia una watoto nje hata nisingekukubali. Daah naumia sana.
Acha tu mkuu, pamoja na mengine ila nilijuta na kuogopa sana endapo vifo vingetokea.Ujana + utoto una mengi sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app