Kisa cha pili .....
Nikiwa nimemaliza form six , basi ikabidi nitoke dar niende kagera kumsabai bibi yangu , Bibi yangu alikuwa akiishi bukoba mjini mitaa ya town kabisa.
Sasa pale kwake alikuwa na vyumba kama kumi na nne, amevipangisha , hivyo ni kawaida mimi kuonana na wapangaji pindi nitokapo ndani .
Sasa katika wale wapangaji kuna mdada alikuwa amepanga na pia anaishi mwenyew tu , ila story za watu eti ni malaya na pia ameathirika na gonjwa la taifa .
Hata bibi aliniambia hivyo pia , ila siku zilivyozidi pale nyumbani Mazoea na wale wapangaji yalizidi , sasa yakawa yamezidi kwa huyu dada, anayeishi pekee yake , Bibi akaendelea kunikanya kuwa niwe mbali na huyo binti , kwanza kanizidi umri pia ana tabia za umalaya .
Dah shetani , msikie tu , si nikajikuta nishaingia kwenye mazoea na yule dada , mwisho nikawa usiku nafungua geti taratibu naenda nalala kwake, asubuhi na mapema narudi, maisha yakawa safi , ila moyoni nikawa sina amani tena maana nilikuwa napiga kavu , hivyo nikawa najua nishaathirika .
Penzi likanoga kwa siri , Bibi hajui kitu kuwa mjukuu nishaingia kwenye penzi la mpangaji japo baadhi ya wapangaji walijua.
Sasa usiku mmoja kulikuwepo na mechi ya Arsenal na man u , nikamueleza bibi naenda mpirani akasema hapana, si uangalizie hapa , nikagoma akakubali niende atanifungulia mageti.
Sasa kumbe mwenzake sina mpango wa kurudi nyumba kubwa nataka nilale na mchuchu wangu , dah kweli baada ya mechi nilikuwa very frustrated sababu chama langu , man u tulikula nyingi .
Nikasema Ngoja nikamalizie hasira kwa mpangaji wetu bila kuwaza kuwa tayari nina ngoma toka kwake , lahaura , kumbe masikini mbibi wa watu hajalala anawaza mjukuu wake mbona harudi ?
Mida ya saa saba nikasikia mlango wa nyumba kubwa umefunguliwa mda huo nipo juu ya kifua cha dada mpangaji , sasa nikawaza mda huu bibi anatafuta nini ?kumbe mbibi hajalala anamuwaza mjukuu wake , saa ngapi asimgongee mpangaji mmoja hivi amuulize wapi tunaangaliziaga mpira , mda huo nawasikia.
Mara ghafla nikawa siwasikii tena , kumbe yule mpangaji kauza ramani ya vita , kamchana bibi kuwa mpira ulishaisha ila anadhani nitakuwa chumba cha dada mpangaji maana uwa ananiona naingia usiku .
Bibi wa watu , upendo kwa mjukuu ukamzidi uwezo akagonga hodi kwenye chumba chetu, mdada akaanza kutetemeka ni nini afanye, mimi nimeinama nawaza aibu , naiweka wapi?
Mara mdada kafungua mlango , Bibi kaingia anafoka kwanini unataka kumuua mwanangu , mara akague huku mara kule, muda huo nimejificha kwenye vyombo , Bibi aliponiona akaanza kumpiga mdada na ndala kwanini unataka kumuua mwanangu, akitamka hivyo , mdada alivaa kanga tu , mara akakimbia nje
Mda huo nimevaa boksa na shati tu , Bibi alivomfuata nikavaa suruali Chapu, nikavaa sendo nikatoka nakimbia huku aibu , maana watu wameamka ili kuona ni nini kimetokea.
Nikawaza sana njiani sijui wapi naelekea mwisho nikasema siwezi kufa kizembe, nikaenda moja kwa moja mpaka sitende ya mabasi ya mkoani , pale nikakuta kama mchana hivi , fasta nikauliza kama naweza mpata wakala wa mpesa , nikampata.
Nilitoa elfu themanini, maana ilikuwa kwenye simu , nikakata tiketi kwa elfu hamsini na tano , bukoba kwenda dar , baada ya kupewa hela na nikaoneshwa basi, nilienda mle nikakaa nawaza mengi mpaka najionea aibu mwenyewe mda huo , Bibi anapiga simu sipokei mara nikazima.
Nilifika dar baada ya safari , nikakuta bibi alipiga simu anasema hajui alimuudhi nini mjukuu wake maana amekimbia nyumbani hayupo na hajaaga , dah bibi bwana ila hakusema nimefanya nini ?
Dah nilivoambiwa hivyo , nilijikuta nalia tu , nikaishia kusema nilimiss kurudi dar tu , ila moyoni najua bibi aliamua kuvunga ila baada ya siku kadhaa bibi , alinitafuta akanisihi nisirudie hiyo tabia na pia akaomba niende nikapime UKIMWI , alafu nimpe majibu , kweli nilipima nikajikuta negative .
Dah nilipomwambia bibi alifurahi sana , mpaka nikamsikia analia kwenye simu Ila yule Demu sikumtafutaga tena .
Dah bibi yangu mpaka leo ananipenda sana na hajawahi kunitobolea siri hii
Dah wewe mdada kama uko humu nisamehe bure ulikuwa ujana ndiyo maana sijawah kukutafta