Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nilimpa demu wangu wa utotoni li baruti fulani lenye muundo wa mshumaa nikamdanganya kuwa ukiwasha kale kautambi zinatokea rangi nzuri aisee si akaenda nalo moja kwa moja hadi kwao akaingia jikoni ambapo wapangaji wote hupikia humo na mama yake yupo humo anapika si akaliwasha bwanaaa weeeee LIKAJIBU PWAAAAA kmmke daa wengine walizimia na kulazwa include mama yake ila mmoja aliruka mripuko uliposikika akatua kwenye maji ya moto.Jamani navyoongea hivi kuna mtu ana jeraha lilosababishwa na ujinga wangu MUNGU NISAMEHE.Mi baruti tuliipata kwa dada yangu ambae alikuwa anafanya kazi kwa WaINDI sio jambo la kujisifia ila kilichonikuta baada ya hilo tukio mixer na mapolisi waliingia mama yangu haelewi kwa nini nimekuja kukamatwa aisee.
Demu wako nae fala anapokea tu vitu asivyovijua[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Miaka mingi nyuma ya ujana nikiwa field ile kwenye halmashauri moja hivi mimi na mpenzi wangu/girlfriend kutoka chuo kimoja.

Tukagombana nikamnunia kwa wivu akaniomba tutoke out nikakataa yeye na marafiki zake wakaenda saa sita usiku napigiwa simu na rafiki yake njoo....

I wish nisingemkatalia kutoka out R.I.P my angel naamini asingekutana na yaliyomkuta, ulinipenda sana nakiri sikujali hisia zako.

Kifo ni fumbo kubwa.

Tuwajali Sana wanaotupenda, life is too short.

Duuuh, Nini kilimkuta Angel mkuu?
 
Nilimpa demu wangu wa utotoni li baruti fulani lenye muundo wa mshumaa nikamdanganya kuwa ukiwasha kale kautambi zinatokea rangi nzuri aisee si akaenda nalo moja kwa moja hadi kwao akaingia jikoni ambapo wapangaji wote hupikia humo na mama yake yupo humo anapika si akaliwasha bwanaaa weeeee LIKAJIBU PWAAAAA kmmke daa wengine walizimia na kulazwa include mama yake ila mmoja aliruka mripuko uliposikika akatua kwenye maji ya moto.Jamani navyoongea hivi kuna mtu ana jeraha lilosababishwa na ujinga wangu MUNGU NISAMEHE.Mi baruti tuliipata kwa dada yangu ambae alikuwa anafanya kazi kwa WaINDI sio jambo la kujisifia ila kilichonikuta baada ya hilo tukio mixer na mapolisi waliingia mama yangu haelewi kwa nini nimekuja kukamatwa aisee.
Duhh [emoji848][emoji16][emoji16][emoji16] huyo Manzi alikuonaje !?

Sad [emoji30][emoji20]
 
Nilibebeshwa mavi mkononi kwa sababu ya upole


Mimi ni mpole ila nilivyokuwa mdogo nilikua mpole kupitiliza ndo maana nilibebeshwa mavi ambayo sikunya mimi.


Kipindi nipo darasa la kwanza nilipelekwa boarding sasa hiyo siku tuko zetu tunacheza mida ya jioni akaja matron akatuita boys wote tulikua kama 30 hivi ambao tunakaa bweni na tulivyokusanyika akatuambia nifuateni tukaona anaelekea chooni basi tukamfwata tulivofika chooni ile sehemu ambayo ipo special kwa ajili ya haja ndogo tukakuta mavi yapo makimba matatu yamejipanga matron akauliza nani kanya hapa ina maana vyoo hamvioni mpaka mtumie sehemu ya haja ndogo nitajieni aliyekunya hapa.


Wote tulikua kimya mara ghafla kuna dogo mmoja mmasai anaitwa Lomnyaki akayasogelea yale mavi akayaangalia afu akanitaja akasema matron huyu Mafian cartel haya mavi yake kabisa yeye ndo kanya hapa mavi yake nayajua dah nilishangaa sana kumsikia Lomnyaki akinisingizia kosa ambalo sikufanya sijui alikua ana malengo gani kunichoma kwa matron


Basi Matron hakutaka maelezo akawaruhusu wenzangu waondoke akabaki na Mimi na kunihoji kwa nini nimekunya sehem ambayo siyo sahihi basi na Mimi na upole wangu ambao ulikua uboya nikawa nalia tu kwa kuonewa matron akasema wewe lia ila haya mavi uyazoe ukatumbukize Kwenye tundu la choo nikirudi nisikute mavi hapa afu akaondoka


Dah sasa nikabaki pale nahuzunika moyoni namlaumu Lomnyaki kwa kunichoma,basi nikachukua toilet paper nikaanza kuokota kimba moja napeleka kudumbukiza Kwenye tundu la choo nikachukua tena lingine hadi nikamaliza kuzoa makimba yote matatu kisha nikanawa na kumwambia matron nishamaliza kuzoa makimba yale.akasema sawa nenda ila usirudie tena.


watu walinicheka sana na kunitania pale shule mpaka Leo natafakari kwanini Lomnyaki alinichoma wakati mimi sihusiki labda yeye ndo aliyekunya n kuamua kuniuzia kesi

Mataccor yako Lomnyaki
 
Nilibebeshwa mavi mkononi kwa sababu ya upole


Mimi ni mpole ila nilivyokuwa mdogo nilikua mpole kupitiliza ndo maana nilibebeshwa mavi ambayo sikunya mimi.


Kipindi nipo darasa la kwanza nilipelekwa boarding sasa hiyo siku tuko zetu tunacheza mida ya jioni akaja matron akatuita boys wote tulikua kama 30 hivi ambao tunakaa bweni na tulivyokusanyika akatuambia nifuateni tukaona anaelekea chooni basi tukamfwata tulivofika chooni ile sehemu ambayo ipo special kwa ajili ya haja ndogo tukakuta mavi yapo makimba matatu yamejipanga matron akauliza nani kanya hapa ina maana vyoo hamvioni mpaka mtumie sehemu ya haja ndogo nitajieni aliyekunya hapa.


Wote tulikua kimya mara ghafla kuna dogo mmoja mmasai anaitwa Lomnyaki akayasogelea yale mavi akayaangalia afu akanitaja akasema matron huyu Mafian cartel haya mavi yake kabisa yeye ndo kanya hapa mavi yake nayajua dah nilishangaa sana kumsikia Lomnyaki akinisingizia kosa ambalo sikufanya sijui alikua ana malengo gani kunichoma kwa matron


Basi Matron hakutaka maelezo akawaruhusu wenzangu waondoke akabaki na Mimi na kunihoji kwa nini nimekunya sehem ambayo siyo sahihi basi na Mimi na upole wangu ambao ulikua uboya nikawa nalia tu kwa kuonewa matron akasema wewe lia ila haya mavi uyazoe ukatumbukize Kwenye tundu la choo nikirudi nisikute mavi hapa afu akaondoka


Dah sasa nikabaki pale nahuzunika moyoni namlaumu Lomnyaki kwa kunichoma,basi nikachukua toilet paper nikaanza kuokota kimba moja napeleka kudumbukiza Kwenye tundu la choo nikachukua tena lingine hadi nikamaliza kuzoa makimba yote matatu kisha nikanawa na kumwambia matron nishamaliza kuzoa makimba yale.akasema sawa nenda ila usirudie tena.


watu walinicheka sana na kunitania pale shule mpaka Leo natafakari kwanini Lomnyaki alinichoma wakati mimi sihusiki labda yeye ndo aliyekunya n kuamua kuniuzia kesi

Mataccor yako Lomnyaki
Ulikuwa na mazoea na shobo za kifala, thats why wakakufanya mbuzi wa kafara
 
Good.

Sasa mtoto wa kiume jifunze kutoka kwa mwanaume.
Chukua huo ushauri na funzo kutoka kwa mwanaume mwenye busara na hekima kabla wanaume wasio na busara hawajakufundisha kuheshimu cha mtu kwa nguvu then ukaja kujuta.
Mm point yangu ilikua mtoto kua mdokozi kipindi cha utoto sio utu uzima

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa nyumbani hautoshi kabisa.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules.

Sem ya kwanza ikaisha, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakasonga.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau, na ndio hapo unapoingia mtegoni unadakwa na kila kitu kinakua kichungu.

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Dah umenikumbusha mbali sana......sitasahau aiseh[emoji22]

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI


Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.

Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.

Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro[emoji2955][emoji2955][emoji2955].

Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.

Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.

Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.

Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.

Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91].
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.

Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.

Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.

Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.

Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.

Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.

Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kisa cha tatu......
Nilimaliza form four , nikafaulu kwenda advance mkoa fulani kwa division 1 , basi ndugu zangu kwa kunipenda na ukizingatia nililelewa na ndugu zangu upande wa mama , sababu ni yatima since then .

Ndugu wakaomba nisome dar nisiende mkoa niliopangiwa sababu ya hali ya kuhisi nitakuwa mpweke , dah walinipenda wajomba sana , basi ikatafutwa shule dar , mwisho nikapatiwa shule pale kimara mwisho, shule ya seminari chini ya dini ya Lutherani , dah na huku ni muisilamu , ila haya yote yalifanyika sababu upande wa mama huku ni wakiristo.

Ile hali sikupenda ila nilikubali kwenda tu maana hata msikitini sikuwahi kugusa, nikawa sina namna ila hiki kitu kilinifanya nianze kuona kweli bila wazazi hakuna haki, hivyo nikawa ni mtu napenda sana haki kwa yoyote hata kama hayaniusu ila tu haki ya mtu inavunjwa nilijihisi ni mimi.

Basi ile hali ya kupenda haki kwa yeyote mbele ya macho yangu ndiyo ikawa ni falsafa yangu, hakika mtu alikuwa akibuguziwa mbele ya macho yangu nahisi ni mimi vile .

Sasa basi ndani ya shule hii ya wanadini , nisharipoti na naendelea na masomo , nikaanza kuumizwa na mambo yanayoendelea pale shule, Ada tunayolipa ila haiendani na huduma tunazopata, kuanzia chakula na hata mazingira ya shule yenyewe, ila hata ratiba ya chakula haizingatiwi .

Dah nikajikuta nawaza ni vipi najikwamua na hili kwa kuitetea jamii ya wanafunzi wenzangu , dah nikaanza kwa kugombea ukaka mkuu hapo shuleni ila umri wangu , na pia umbile langu , vikaninyima ukaka mkuu , maana niliwaza ndiyo njia pekee ya amani ningeweza kukaa meza moja na walimu ili tuyajenge .

Basi walimu kwa udhubutu wangu wa kugombea wakaamua nipewe tu cheo cha kiongozi wa nidhamu , maana nilionekana mpole sana kumbe sio kweli mimi ni mpole wa sura ila mwingi wa fikra na hasira ukizingua.

Nikaanza majukumu yangu kama kiongozi wa nidhamu ila ndiyo nikaja kugundua ile shule mbali na kuwa ni ya dini ila imejaa ukabila maana kuanzia juu mpaka chini ni kabila fulani , ndiyo nikajakughamua kumbe hata viongoz wa wanafunzi wote ni kabila hilo isipokuwa mimi na jamaa mmoja kutoka kagera .

Basi miaka ilikata nikimaliza kidato cha tano , kuingia kidato cha sita , ndiyo jamaa yangu mmoja pale shule akaniita na kuniambia kuwa hawa walimu ni waoga sana, hivyo tukiamua kusimama mimi na yeye kupinga ujinga na ubwenyenye wote pale shule watapoa na watu watapata haki zao .

Nikamuuliza ni jambo zuri ila kwa njia ipi ni hapo akanipanga kuwa atajitaidi aombe ruhusa mwisho wa juma ili aende kwao , achapishe karatasi nyingi zenye orodha ya mambo ambayo sio Sawa yanayoendelea pale shule na akizileta mimi kazi yangu ni kuzisambaza usiku ili kupima upepo wa walimu wataamua nini?.

Basi kweli mwisho wa juma , alifanya hivyo na aliporudi alikuja na hizo karatsi zimeandikwa shida zote pale shuleni na vile ada tunayolipa ilivyo kubwa na mwisho akaeleza na baadhi ya vifungu vya haki zetu kupitia katiba na vile ni kipi kitafanyika wasipokuwa tayari kutusikiliza kupitia hizo , karatasi zetu .

Dah aisee , kulingana na makubaliano na jamaa yangu , huyo kwake alikuwa kazi kamaliza ilikuwa ni mimi nifanye kazi ya kuzitapanya zile karatasi eneo lote la shule.

Kweli siku ile baada ya kunikabidhi nilimuambia alfajiri ya jumatatu, nitafanya hiyo kazi na hatoamini .Kweli usiku wa jumapili , mida ya saa nane usiku , niliamka na kuchunguza walinzi wote wamelala na shule iko kimya sana .

Nikaanza kazi yangu kwenye milango ya wachungaji, madarasani, assemble, na kila kona baada ya hapo , nilirudi bwenini nikalala na asubuhi kwa kuwa nilikuwa kiongozi sikuijari kengele ya morning preparation, niliendelea kulala ndio nikasikia kengele ikigongwa kuwa ni dharura.

Haraka nikawahi assemble ndiyo nakuta wanafunzi wamebeba hizo, karatasi na walimu pia kila mtu haelewi ni nani kafanya vile .

Katika zile karatasi mimi na rafiki yangu kuna jina tulijiita ila kwa ajiri ya kuficha identity yangu sitalitaja .

Kabla ya kufikia maamuzi haya nilijithidi sana kuwahimiza viongozi wenzangu kuhusu haki za wanafunzi wenzetu ila hawakuwa upande wangu hata kidogo .

Hivyo baada ya mambo hayo wengi walinishuku japo hawakunitaja, ilipigwa kura ya siri kwa unaemdhania ila bado sikuwemo .

Mwisho hiyo wiki ilikuwa wiki ya vikao vya walimu na maaskofu na wachungaji , na hitimisho huduma zikarudi kuwa nzuri kuendana na Ada ya wanafunzi .

Ila baadaye jamaa tulieshilikiana naye aliuza ramani kwa rafiki zake wengine , na ile shule ilikuwa na vitoto vipelelezi vya walimu , hivyo wakazipata habari ila yeye kwenye story alijisema yeye tu basi alipoitwa na walimu alikiri ndiyo huko akanitaja na mimi .

Ila nilivyoitwa kuhojiwa nilimkana sana mpaka wakaniamini, jamaa mwisho alifukuzwa shule.
Kiukweli niliumia ila mwisho nikasema hakuna zaidi ya kifo kwa msaliti.

Ila baada ya mimi kuhisiwa hivyo basi na uongozi nikavuliwa nikaanza , kuandamwa na kesi kibao mara nina wasichana o_level na advance , yaani ikapandwa chuki dhidi yangu kwa wanafunzi , nikawa ni mtu mpweke sana , wanafunzi mda mwingine wakaanza niona mimi ni spy wao na walimu wakawa wananiona adui wa maendeleo ya shule .

Hatimaye muda ulifika nikahitimu kidato cha sita ila ile shule mahafali hufanyika kabla ya mtihani wa necta , hivyo tulifanya mahafali ila mimi sikumuita ndugu yeyote hivyo nilikuwa alone pia .

Dah kilichoniumiza katika mahafali yale kuna masomo na baadhi ya vitu nilistahili kupewa zawadi mimi maana nilkuwa bora mbali na harakati zangu ila bado nilinyimwa mpaka cheti cha kuwa niliwahi kuwa kiongozi sikupewa pia .

Mwisho nilimaliza nikaondoka zangu pale ila najuta kufanya vile japo niliwasaidia wanafunzi wenzangu ila niliishi kama niko jela nilitengwa na kila mwanafunzi pale shuleni .

Nawamiss sana walimu wangu japo shule ishaanguka kimasomo na kimuundo ila nawakumbuka sana na wanafunzi wenzangu nawamiss pia japo hamkujua shujaa wenu alikuwa nani? Ila ni yule mliyemtenga na kumsimanga sana .

Ina huzunisha kwa kweli
 
VISA NI VINGI,ILA ACHA NIANZE NA HIKI...

Ni 2010's niko form 4 shule ya kata hiyo mkoani Iringa huko. Nilikua mtoro sana,yani nikisema mtoro ni mtoro kweli. Kwa week naweza kuhudhulia shule mara mbili tu,siku nyingine zote nashinda Samora pale katika maroli ya mchanga,mawe fofali,n.k tunasubiri kazi za upakiaji. Au nakua Isakalilo nachimba zangu mchanga au mawe.

Licha ya mahudhulio yangu kuwa mabaya,ila walimu wengi wa ile shule walikua wananijua,haswa Headmaster. Huyu alinijua kwasababu alinisaidia sana kipindi naingia pale form 1.(Hili nilieleza katika ule uzi wa "Msoto")

Tatizo lilianzia hapa.Siku moja bila hata kutarajia alikuja ndugu yangu mmoja wa karibu kabisa akanichafua sana pale shule,wakati huo nimewekwa mtu kati ofisi za Walimu. Yani aliongea mambo mengi sana,kutokana nae ni mtu mzima na ana mwonekano wa busara busara! Basi walimuamini 100%.

Alisema mimi mhuni(Kibaka),MLEVI sana na nakunywa Ulanzi sanaaa! Nashinda na wahuni, sina nidhamu hata kidogo,n.k,n.k. Wakati huo kumbuka sijawahi kuishi nae tangu namaliza standard 7 huko,nikitelekezwa nikawa naishi tu kama mtoto wa mtaani. Nilikua Chokoraa ambae shule niliipenda ila nilikua nashindwa nijigawe vipi,huku nihudhurie shule au nitafute hela ya kula.

Basi ndugu zangu tuendelee, Headmaster na wale maticha hawakutaka hata kunipa nafasi nijitetee, na hata wangenipa nafasi ya kujitetea sidhani kama ningeweza,nilikua nacheka cheka tu kwa hasira. (Mimi nikikasirika sana huwa natabasamu sana na kakicheko kwa mbaliii).

Kama unavyojua shule zetu za kata,mimi nikadhani yanaishia pale,ajabu yule ndugu yangu akaamuru nichapwe viboko hadharani. Ikagongwa kengere pale,wanafunzi wakakusanyika pale,nikachafuliwa sana pale assemble,daah yani chafuliwa sanaaaa! Muda huo mimi hasira zimejaa level yake ila tabasamu limejaa usoni halikauki,ndio nilivyo.

Kama unavyojua wanafunzi, mashtaka yalikua kibao,ila points za msingi walizochukua ni "Mimi Kibaka" na "Mlevi,nakunywa sana Ulanzi".

Daah wakawa wananitania sana kila nikienda shule katika zile siku mbili zangu za week, nikawa nahisi karaha,basi nikapunguza mahudhulio kutoka siku mbili mpaka siku moja kwa week au siendi kabisa.

Basi kuna siku nikaenda shule ni kipindi tunakaribia kufanya mtihani wa Mock, Headmaster akaniita Ofisini. To be honest sijawahi kwenda shule nikiwa na "Majagi" kichwani,ila siku hiyo nilikua Majagi haswaa,ila nimekula majani ya mti wa limao ili kuzuia harufu. Daah kufika ofisi ya Headmaster si akaanza kunikumbushia yale ya siku zile,akawa kama ananisimanga na ule msaada ambao alinipa kipindi naanza form 1.

Siwafichi uvumilivu ulinishinda,nikawa natetemeka kwa hasira yule mzee yuko mbele yangu kakaa anaendelea kutema shombo zake. Nikagonga meza kwa hasira "Kaa kimya wewe mzee",...aah mzee akajaa upepo baada ya kuona kama namchimba mkwara,si akasimama tukawa tunatazamana ila yeye yuko upande wa pili wa meza.

Aisee! Nilimpa ndonga (Kichwa) moja matata sana mpaka akajikuta kakaa chini bila kutarajia,alafu kimyaa!. Nikajua nimeua wakuu,ila nikavaa roho ngumu nikatoka mle ndani kama hakuna kitu kimetokea,nikatimkia mtaani.

KITU NAJUTIA
Ni kumpiga kichwa mtu ambae anakaribiana na babu yangu. Yani najuta sana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Hii kitu iligharimu watu pia chuo cha Iringa!
Hatu chuo nilichosoma mimi.. mimi mwenyewe ilibaki kidogo tu niingie maana washkaji tulikuwa tunapigika wote ghafla nashangaa wenzangu wote lunch za maana peke yangu ndio nmebaki kwenye dona la buku dah.. sema baada ya msala tulimaliza wachache sana chuo, wengine hawakurudi kabisa
 
Back
Top Bottom