Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

kila nikiandika nafuta maana yanatisha hadi hapa nilipofika 🙌🏻
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.


Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Naitwa Analyse
 
Mimi nakumbuka kipindi nasoma darasa la tano na Dada yangu alikuwa kidato cha kwanza .siku moja Dada alitutoroka ndani akaenda kulala kwa mwanaume asubui saa 12 akarudi huku mzee hajui basi pale mimi so nikamsemelea kwa mzee aisee mzee alimtandika sister hadi akazimia Baadae akafufuka , kumbe Dada alikuwa na mimba kidogo Sasa kutoka na kipigo ile mimba ikaharibika Akapelekwa hospital daah aisee Dada akafariki hilo naumia hadi leo bora nisinge sema na Baba nae akafungwa Jela miak 9 bahati zuri alotolewa kwa msamaha wa Rais.
Huna kosa,ukupenda kuona dada yako anaharibika...
Mzee ndio kazingua.
 
Mimi nakumbuka kipindi nasoma darasa la tano na Dada yangu alikuwa kidato cha kwanza .siku moja Dada alitutoroka ndani akaenda kulala kwa mwanaume asubui saa 12 akarudi huku mzee hajui basi pale mimi so nikamsemelea kwa mzee aisee mzee alimtandika sister hadi akazimia Baadae akafufuka , kumbe Dada alikuwa na mimba kidogo Sasa kutoka na kipigo ile mimba ikaharibika Akapelekwa hospital daah aisee Dada akafariki hilo naumia hadi leo bora nisinge sema na Baba nae akafungwa Jela miak 9 bahati zuri alotolewa kwa msamaha wa Rais.
Aiseeeee wewe bhn weweee... Hii case ni nzito, ila poleni sana....
Mmmmhhh no comment kwa kweli
 
Nakumbka mara ya kwanza, nazamia ulaya nlikua nmelamalza 4m4 2016, nikatafta pesa hivo nkatafta namna nzur ya kusafr lengo kuu ilkua kwenda china , sababu Abroad is my hobby,

Nlipata nauli kamili ya kwenda china na nikaanza kwa kwenda Ethiopia, Addis Ababa,then nkakaa hapo sku chache then nkakutana na bint niliemuamini na ni mwenyeji sana huku china(Shenzhen)

Ikawa rahs kupata visa, lengo langu ilkua kwenda china kuchek Dili za biznez hasa ya nguo, so nlikua na mtaji mdg, na mm nlikua mzoefu wa mitumba toka mdg, had skul nlikua pumzko la sa4 nafunga kamba na kutandaza nguo zangu so nlikua nauzoefu wa ndan ya nchi.
Bas safar ikafana na nimara ya kwanza kusafr kwa chopa, Boeing ,

Bas tukafka nkafikia kwake,
Ofcoz Alikua mwenyj na alinishaur mtaji wangu niweke kwa mifumo ya china kweny mtandao hivo nkafata kila anacho nishaur, nakumbka tulilala ila skujua kesho nainza vp coz sjawah muona huyo bnt had now na Chinese police walinikamata kwa tuhuma ya kete,
Na bnt pia alikmatwa, story n ndef but nlipitia magum katka umr mdg ,

Kwa sasa nipo tz na chna naenda sana na china za uingereza nmeburuza sana, ile ilinifundisha kutoamn mtu na pia ilinipa chachu zaid, na nlijalaum mwnzo ila kwa sasa naona ilikua kama subtopic nzur kwangu, nkiwa na mda ntashusha story yote china na had kurd bongo.
Umeacha kipande muhimu sana
 
Niliwahi pita na nguruwe kwenye pikipiki mbele ya Msikiti dah tulichapana sana na madogo wa msikitini pale. Wakanizidia bahati raia wakajaa. Ila nilizongwa sana. Nilichapika sana
Kwamba hili ni kosa??
 
COUNTERFEIT MONEY

Wakati bado nipo chuo kabla ya msala wa Receipt fake.. ilikua ni mwaka wa pili kama sikosei sem ya pili.

Hii story kama mhusika yuko humu JF atanijua rasmi mimi ni nani. Ila hakuna shida, cha kuogopa ni kifo pekee na bado kidgo kingenikuta!

Jamaa yangu mmoja nilikua naishi naye hostel nje kidgo ya chuo. Yeye kama ilivyo mimi hatukuwa na mkopo, na kwao hawakua vizuri kama ilivyo kwetu. Sema yeye alikua mtoto wa mjini kushinda mimi na alikua ameniacha parefu ki umri. Sema kuna vitabia flani hivi huwa vinafanya watu wanakua marafiki. Kwa namna yeye na mimi tulivyokua, ungeweza kutuita wazee wa michongo katika rejesta za kileo.

Kwa vile tulikua tunakaa room moja, vitu vingi kuhusu mimi vilikua wazi. Sina hela. Nimefulia. Sikua hata na confidence ya kusimamisha mwanamke nimtongoze. Akitaka tutoke out nitampeleka wapi? Kwa hela ipi? Kwaiyo nikawa ni mtu wa kutulia sana ndani na kuishi kikamilifu ndani ya ratiba za chuo na hostel. So unaweza ku imagine vile maisha yangu yalikua Boring!

Siku moja wakati tunapiga story za hapa na pale na jamaa akaniambia kuna mchongo wa siri anataka kunishirikisha. Nikatega sikio vizuri. Akaniambia kuna jamaa anamjua tukimpa kiasi fulani halali anaweza kututumia hadi mara nne yake ya bandia. Kwaiyo sisi kazi yetu ni kutafuta changes (Chenchi) tu ili tupate za halali.

Duh, wakati ananiambia mimi natetemeka. Nikamwambia mwanangu hii issue si inaweza ikatufanya tufungwe kabisa? Akaniambia "Ufungwe na nani?" .. "Tulia nikuoneshe", na mimi nikatulia.

Jamaa akaagiza mzigo, ukafika. Ilikua kama Mil 1 hivi ya Bandia. Nikamuona kwenye zile pande mbili za kuwekea hela kwenye Wallets; upande mmoja kaweka pesa halali kama 30K, na upande mwingine kaweka bandia kama 100K (Laki). Kaoga kamaliza, huyoooo kasepa!


Alikua ni mtu wa viwanja sana, sikumsikia wakati anarudi usiku. Kwaiyo kesho yake ahsubui namuona kakaa kwenye angle ya kitanda anahesabu hela, Duh. Ni kaki na buku be za kutosha. Mshenzi kashikisha watu zaidi ya elf 90 za bandia. Kabaki na 10 tu. Mimi tamaa ikawa imeanza kugonga mlango, nikawa sitaki kuifungulia. Unajua ukiwa umefulia sana vishawishi ni rahisi sana kukuzidi nguvu. Nikaendelea kujikaza huku jamaa yangu anazidi kuagiza mizigo na anapiga hela vibaya mno.

Mimi nampiga tu vi mizinga vya hapa na pale mwisho wa siku nikajikuta na mimi kanigawia fungu la kuchekecha. Ilikua kama laki 5. Laki 4 bandia, laki 1 halali.

Kama uko viwanja pesa za kwanza unatoa halali, halafu unatafuta mhudum mmoja mwenye tamaa unampiga vi ofa vya Beer huku ukiandaa mazingira ya yeye tu kukuhudumia. Akianza kuchangamka unamsukumia hizo noti mdogo mdogo kama hatasanuka ndio imeisha hiyo. Kazi inakua imebaki kuhesabu changes(Chenchi) nikifika hostel.

Shetani ni mjanja sana. Huwa anakulinda ukiwa unaanza magendo halafu baadae anakutelekeza ukisha kolea. Ndio kilichonikuta mimi, sikumaliza hata mwezi kwenye huo mchongo. Mungu huyu ni wa kumshukuru sana! Nisingekua naandika huu uzi hapa sasa hivi.

Kuna mahali nilikuja kusoma kuwa "Katika magendo yoyote yale, daima epuka kuwafanyia watu wenye hali za chini [kama masikini na wenye disabilities] kwa sababu ina create a very bad luck".Mfano mzuri ni watu wanaoiba vipochi vya wa Mama barabarani au sokoni, nadhani mnajua kinachowakuta wakidakwa! Na ndio kilichoniponza, kwa sababu nilikua desperate sana kupata hela haraka haraka nikaanza kuwafanyia hako ka mchezo mpaka boda boda na dereva taxi. Eh bhana eeh. Kumbe walikua wakifika sheli wanakataliwa pesa zao, wengine mpaka wanaitiwa polisi mimi sijui.

Wakawa wamejipanga siku wakimkamata huyo anayetoa pesa za bandia wanamuua. Mimi sikua nafahamu, nilikuja kugundua baadae huko. Sasa kuna boda wawili ambao nilikua napenda sana kuwatumia katika mishe zangu ambao nilikua nawapa pesa halali, hao ndio walikuja kuniokoa siku nimebananishwa nataka kumalizwa.

Siku yenyewe ilikua hivi. Mida ya jioni nimetoka zangu misele nikapita kijiwe kimoja kipya cha toyo nika scan sura za wajomba nikamuona mmoja kama boya boya hivi nikamchagua anipeleke maeneo karibu na Hostel (Huwa napenda kushukia kwa nyuma kidgo). Sasa kosa la kwanza, sikuwa na pesa ya halali hata moja kwenye wallet.

Sijui ilikuaje nikatumia zote huko nilipotoka halafu sikukagua kabla sijapanda boda. Ile nimeshuka si nikampa jamaa ten. Akaanza kuikagua akakuta ni bandia, akanikwida shati faster. Akasema wewe ndio tulikua tunakutafuta. Nikawa nabishana naye pale kwani vipi, kama ni bandia huenda hata mimi nimeshikishwa nikatoa wallet nikachomoa ten nyingine kumpatia alivyoicheck nayo ni bandia. Mama yangu!

Akapigia simu washkaji wa kijiweni na wao wakapigiana simu na wengine wakajaa pale. Mimi najifanys sielewi nimepanick najisachi kila mahali. Akaja jamaa mmoja akasema huyu mnamuhoji wa nini nikapigwa kofi moja la maana mpka nikajikuta niko chini. Nikaanza kulia kwa huruma. Wahuni wengine wanasema litafutwe tairi nichomwe. Ghafla mmoja kati ya wale jamaa naowatumiaga mara nyingi akawa na yeye amefika eneo la tukio. Hapo nimesha shikwa shikwa sana mpaka shati limechanika. Sura yangu imeanza kufanana kabisa na ya mwizi. Moyoni mwangu nimeshakubali kuwa leo ndio mwisho wangu!

Jamaa kuniona si ndio akawambia mbona huyu ni mwanafunzi wa chuo namchukuaga sana. Boda wengine wakakataa kata kata kuwa hakuna huyu ni jambazi hakuna kutetea. Wengine wakataka ninyang'anywe pochi waangalie ID. Ndio wakaona kweli mimi ni mwanafunzi. Hapo nimeshalia nimechoka, nawambia mimi sio mwizi jamani, mtaniua bure tu, nawaelewesha kuwa nilikua na shida nikaamua kuuza simu yangu ya kupangusa nahisi wale jamaa niliyowauzia ndio wamenifanyia huo mchezo hata mimi sielewi kama ni bandia.

Wakanichukua wakanipeleka kituo kidgo cha polisi hakikua sana mbali na pale. Nikaandika maelezo yangu na wao wakaandika maelezo yao. Sikumaliza hata siku tatu jamaa yangu akaja na wenzake wawili kuniwekea dhamana. Mambo yalikuja kuisha lakini baada ya hilo tukio na jamaa yangu akaachana na hayo mambo kabisa.

Bado nakumbuka vile nilikua najuta na kusali kule kituoni. Kumbe kufa ni kitu kidogo sana. Nikasema nikitoka hapa naenda nyumba za ibada kutoa sadaka ya shukrani. Washkaji walivyoisikia issue yangu, waliniambia nina bahati sana. Lazima kuna kusudi la Mungu katika maisha yangu ndio maana nimeponea kwenye tundu la sindano.
Walipopekua wallet kuona ID hawakuziona noti bandia nyingine?
 
Mi najutia kurud bongo tuu.. tho niko mbion kusepa tena
Yaani weye sepa tu tena kimya kimya bana. haijalishi una umri gani, nenda kuree roho napenda! ukitaka nauri tutakupa!.....usiogope kuna kitu hukooo! ila hujajua!
 
Niliiba Matofali ya mwalimu Nyerere palee mwitongo wkt huo nikiwa na Mjomba wangu!!ila mjomba ndo aliniingiza mkenge Basi bana askari ana akili sana alijifanya haja tuona kabisaaa!!..... tukaenda tukarudia mara kibao!! kwa akili za utoto nilidhani ni kawaida.

kuumbe mwenzngu yule anaiba na mie namsaidia kuiba!! ........na uzuri ni kwamba Julius alikuwepo wakati huo!!! ...akatukamata kiulainiiii!!

tukapelekwa kwa julius Live.......mengi yalifanyika pale .........ila yule Mzee alikuwa ni wa ajabu sana narudia tena, sijakosea alikuwa wa ajabu mnoooo sana tuuu!!... .......lkn to cut long story short ndo ukawa mwanzo wa mie kusaidiwa shule tena nzuri sana abroad nilishangaa mpaka leo hapa nilipo bado nashangaa!! ......na marehemu kazi hii ilifanywa na Rais huyo huyo!..... hapo ni kwa kifupi sana nimeitoa hii!
Mzee hii kali..Nimempa vyeo zaidi JK wa ukweli
 
Wewe ndo hujui nn kinaendelea. ..kiufupi sina ac mbili ila nilibadili jina
Ooh! Ndio maana, kuna kipindi nilikuwa namtag to yeye lakini kwa bahati mbaya akawa hatagiki[emoji1787] Kumbe ndo wewe, haya bhana! Si ulisema utakuja Dar nikuchakate mbususu, au umehairisha[emoji41][emoji41]?
 
Mimi nakumbuka kipindi nasoma darasa la tano na Dada yangu alikuwa kidato cha kwanza .siku moja Dada alitutoroka ndani akaenda kulala kwa mwanaume asubui saa 12 akarudi huku mzee hajui basi pale mimi so nikamsemelea kwa mzee aisee mzee alimtandika sister hadi akazimia Baadae akafufuka , kumbe Dada alikuwa na mimba kidogo Sasa kutoka na kipigo ile mimba ikaharibika Akapelekwa hospital daah aisee Dada akafariki hilo naumia hadi leo bora nisinge sema na Baba nae akafungwa Jela miak 9 bahati zuri alotolewa kwa msamaha wa Rais.
Dah imeniumiza Mimi ambae smjui je wewe ambae unamjua,,duh.pole,
 
Kuna watu unaweza kujuta kuwafahamu au kukutana nao..

Anakudhulumu na jela anakufunga Kisha anakutoa kwa masharti .. ..
 
Niliwahi pita na nguruwe kwenye pikipiki mbele ya Msikiti dah tulichapana sana na madogo wa msikitini pale. Wakanizidia bahati raia wakajaa. Ila nilizongwa sana. Nilichapika sana
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu wote pale hamna aliyekuwa anajua kwann tunaitwa na tulivokusanyika tukambiwa tukae chini ndo maafande wakaja na majina ya waliochana magodoro na sisi tuliochana uniform ndo tukajumuishwa na pia hamna aliyekuwa anajua kwamba tungeenda kusulubiwa na mijeledi siku kama ile ya kumaliza shule[emoji23][emoji23]
Nakumbuka hii siku

Sitasema ni mwalimu au askari
 
Back
Top Bottom