Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nakumbuka mwaka 2018 nlipewa ada 3M ili nikaanze chuo PASIANSI MWANZA
Mhuni nkaweka ada mfukoni, nkafka mwanza nkapanga geto,nunua godoro, gesi na mahitaj mengne kama milioni ikaisha, nkabaki na 2M
Nkaanza kubet naweka stake ya lak 5 kwa game 4 tofauti, nakumbuka nlishinda shinda had mtaji kufika 4M, nkanunua pkpk King lion 1,nkawa napga boda pale buzuruga shule, kipind cha likizo nkawa naenda home kama kawa, sasa ikafka hatua mda wa kumalza chuo ukafka maana cozi ni mwaka mmoja, mzee akaniambia niende kuna mkubwa mmoj yupo ngorongoro anahitaj chet changu, hapo mhuni sijui ata definition ya elephant, kilichotokea mungu pekee ndo anajua, nlibadili line ya sim, had mwaka 2021, ndo nkaenda home nkiwa nipo stable financially, matusi hadi kupelekwa polisi,ila saiv mamb yameisha japo naumia maan mdgo angu alisoma pasiansi na saiv n askar game ngorongor ila mm bado nakomaa na mtaa, USIJARIBU KULA ADA,,, sorry kwa uandish mbovu
Naomba unisaidie kumwambia baba yako anielekeze na mm nipeleke Cheti mahala na Mimi nipate kazi.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.


FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Pole sana Mkuu, nishawahi kufanya hiyo kitu o level na advance na pia kwa mdogo angu nishawahi fanya kuanzia kidato cha tatu na cha nne, Sizani kama kuna mashine ya kufyatua hizo receipts labda alikudanganya ili uone ni shughuli pevu, ni uhuni mdogo tu unaofanyika na matokeo yake baada uchunguzi huo yanakuwa kama yalivyokuwa kwako

Makaratasi ya ofisi yanakuwa na pesa nyingi lakini bank pesa inakua ndogo

OVER!
 
Mimi ada nlikua napewa mwenyewe na mzee nikalipe bank nilikua nikipewa laki tano , hapo ada nalipa elfu 20 nyingine yote ni Bata , walikua walikua wanazani natokea family ya kitajiri kumbe dooh! Wazazi wanahangaika , sometime wanauza mpaka viwanja nipate ada

Ila walinishukur sana nilipo jipa jukumu la kumlipia ada mdogo wangu ilihali wanajua sijaajiliwa naunga unga tu mtaani na kazi za kusafisha taa za magari ya watu na kuondoa scratches
 
Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six

Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa

Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa, tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza

Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)

Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)

Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea

Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani

Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana

Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform

Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika

Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)

Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa

Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
Sena mlikua wazembe sana , mshajua kimenuka mkawekwa uwanjani na mkashindwa kukimbia.
 
Sasa nn nawee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hatar
FB_IMG_16669656087892494.jpg
 
Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.


Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Nimecheka sana ilikua Njos nini
 
Haha, sio poa kabsa yan nkipita pale pasiansi hua naumia sna, kuna time mamb yanagoa nashndwa hat kupata msaada kutok kwa wazaz, yan nmetengwa na familia nzma

[emoji23][emoji23][emoji23] ulijifanya unaweza sio
 
Back
Top Bottom