Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Siku niliyodhurumiwa 100,000.

Baada ya kumaliza chuo jijini mwnza mwaka 2016 nkaamua nibaki mwanza nijichanganye mtaani coz nyumbani hakuna dili na ukichek ajira hakuna kabisaa.

Nilikua na dogo langu moja linafanya kazi geita aliniagiza nimnunulie betri ya laptop yake, dogo alinipa laki moja, betri 70 na 25 ya usumbufu na nauli. Siku hyo nkatoka magetoni na sh laki moja na elf moja sikutaka kuchenji ile laki aliyonipa.

Nimefika zangu mitaa ya lumumba niasema ngoja Nile kwanza misele naweza kupata dili koz kwa kipindi kile life lilikua gumu full kujichanganya. Nkapita mitaa ya soko kuu kwa nyuma huku nkaona watu wanejazana nkasema ngoja namim nisogee naweza pata hata dili hapa. Kufika pale nkakuta wamejaza mavitu ndani ya jukwaa yana namba juu yake nkasema ngoja nisome mchezo hapa wanafanyaje

Kulikua na mdada pale alitoa sh 2000 akanunua tiket 2 akawapa pale wakachanganya changanya akashinda moja, moja akakosa. Alishinda begi, Duh! pole mzee.
 
Duh! Uzi mrefu kiasi

Mwishoni mwa mwa mwaka 2011 karibia na kipindi cha msimu wa sikukuu nikiwa nasubiri majibu ya mtihani wa kidato cha nne. Nilikuwa naishi na bibi yangu katika moja ya mikoa ya nyanda za juu kusini.

Nilikuwa napenda sana kujifanya msela na kuiga uhuni kampani yangu kubwa ilikuwa ni masela kwahiyo bangi, viroba na sigara vilikuwa vinahusika sana pale tunapokuwepo kijiweni

Siku moja tukiwa kijiweni tulikuwa raia wawili tu siku hio alikuja mama mmoja akatupa tenda ya kumsaidia kupakia chupa, vinywaji na mazaga mengine ,(huyo mama alifiwa na mmewe miezi kama miwili nyuma mmewe alikuwa anafanya biashara ya kuuza vinywaji vya kawaida na vileo baada ya kufariki mmewe huyo mama alimua kufunga biashara).

Baada ya kumaliza kupakia kuna vitu vingine aliviacha ambavyo hakua na uhitaji navyo. Katika vitu alivyoviacha kuna boksi moja lilikuwa limejaa viroba vilikuwa vinaitwa double punch (sio double kick) walimfanyaje mkuu?
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.

FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Pole sana laskaboza
 
Back
Top Bottom