Kisa QNET, Walimu 8 wafukuzwa kazi Geita

Kisa QNET, Walimu 8 wafukuzwa kazi Geita

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
By Rehema Matowo

Geita. Tume ya utumishi wa walimu wilayani Geita mkoani Geita imewafukuza kazi walimu wanane kwa utoro kazini.

Walimu hao ambao sita ni wa shule za msingi na wawili wa sekondari, wanadaiwa kujishughulisha na biashara za Qnet badala ya kumtumikia mwajiri huku wengine wakidaiwa kuathiriwa na biashara hizo baada ya kujikuta wanadaiwa na wafanyakazi wenzao waliowaingiza kwenye biashara.

Katibu msaidizi wa tume ya utumishi wa walimu wilayani humo, Sitta Mussanga amethibitisha walimu hao kufukuzwa na kabla ya kufukuzwa tume iliunda kamati ya uchunguzi na kujiridhisha kuwa ni watoro kazini.

“Walimu waliofukuzwa kwa sababu utoro wao umesababishwa na Qnet wako wanane ambao walishatakiwa na waajiri wao kwa nyakati tofauti wapo wa halmashauri ya mji na wengine halmashauri ya wilaya waliacha kazi wakaenda Qnet ambako wanaamini kuna maslahi mazuri kuliko huku kwenye ualimu," alisema Mussanga.

Amesema licha ya kuacha pengo kwenye shule walizokuwa wakifundisha kwa kusababisha uhaba wa walimu pia walikokwenda walichotarajia hawakukipata na baadhi wamepata msongo kutokana na kukabiliwa na madeni.

Akitaja shule zilizoathiriwa kwa walimu wao kufukuzwa, Mussanga alizitaja kuwa ni Kivukoni sekondari walimu wawili, shule ya msingi Nyantorotoro(2), Kivukoni ,Lubanda, Mtakuja na mkoani ambazo zote zimepoteza mwalimu mmoja kila moja
 
Pole zao; Qnet ni pyramid scheme, ukiingia huko kichwa kichwa haiwezi kukuacha salama! Pyramid schemes zinawafaidisha wary wenye pesa nyingi wanaoingia mwanzoni mwanzoni, wengine wengi ni maumivu!
 
Back
Top Bottom