Kisa QNET, Walimu 8 wafukuzwa kazi Geita

Kisa QNET, Walimu 8 wafukuzwa kazi Geita

Hivi hawa QChandalua wanatumia mzizi gani maana watu wakishajiunga kuchomoka ni issue
Watu weusi sisi ni wavivu na tunapenda utajiri wa haraka bila kusumbuka sana sasa wazee wa "Fursa" wanapitia humo humo kwa kuwa washajua watu wanapenda utajiri wa haraka wanawatengenezea sinema la kitajiri watu wanajaa wanajipeleka.

Na kitu kingine hao jamaa wameshajua watu wana tabia ya uchoyo wa kushea infos hivyo wakishakupa "training" wanakwambia usishee na mwingine training ila shea tu "good news" juu ya fursa hio kama huyo mwingine atakua interested basi aende nae ahudhurie "training" hapo ndio wengi wasio na akili wanaenda kupigwa.

Nilishuhudia watu akiacha chuo kisa hiyo Q net na walikopa kila sehemu kufikisha 4 mil ya kiingilio. Ndoa nyingine zishavunjika kisa Q net ila watu bado hawaelewi.

Hivyo sio kwamba wana mizizi noo wanatumia tu ujinga wa watu ili kujineemesha na waendelee kuwapiga watu mpaka akili ziwakae.







20220705_144225.jpg
 
Tume ya utumishi wa walimu wilayani Geita mkoani Geita imewafukuza kazi walimu wanane kwa utoro kazini.

Walimu hao ambao sita ni wa shule za msingi na wawili wa sekondari, wanadaiwa kujishughulisha na biashara za Qnet badala ya kumtumikia mwajiri huku wengine wakidaiwa kuathiriwa na biashara hizo baada ya kujikuta wanadaiwa na wafanyakazi wenzao waliowaingiza kwenye biashara.

Katibu msaidizi wa tume ya utumishi wa walimu wilayani humo, Sitta Mussanga amethibitisha walimu hao kufukuzwa na kabla ya kufukuzwa tume iliunda kamati ya uchunguzi na kujiridhisha kuwa ni watoro kazini.

“Walimu waliofukuzwa kwa sababu utoro wao umesababishwa na Qnet wako wanane ambao walishatakiwa na waajiri wao kwa nyakati tofauti wapo wa halmashauri ya mji na wengine halmashauri ya wilaya waliacha kazi wakaenda Qnet ambako wanaamini kuna maslahi mazuri kuliko huku kwenye ualimu," alisema Mussanga.

Amesema licha ya kuacha pengo kwenye shule walizokuwa wakifundisha kwa kusababisha uhaba wa walimu pia walikokwenda walichotarajia hawakukipata na baadhi wamepata msongo kutokana na kukabiliwa na madeni.

Akitaja shule zilizoathiriwa kwa walimu wao kufukuzwa, Mussanga alizitaja kuwa ni Kivukoni sekondari walimu wawili, shule ya msingi Nyantorotoro(2), Kivukoni ,Lubanda, Mtakuja na mkoani ambazo zote zimepoteza mwalimu mmoja mmoja.

Chanzo: Mwananchi
 
Unaweza kuwalaumu walimu but Q-net
wakikufuma maisha yako ni hohe hae kama walimu hu ukiwa Una kiu ya hela , hawakuachi salama , Wana convincing power si ya nchi hii
Wanakutengenezea illusion ya kuona mafanikio yako ya kumiliki mihela na kuitwa bilionea kesho tu utayapata.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wanadhamini man-city 😁😁😁😁😁😁😁
 
KUTAPELIWA PIA NI KIPAJI.

SASA KAZI UMEKOSA
NA UBILIONEA UMEKOSA

🤣
NI MUDA WA KWENDA KWENYE MAOMBI NA UPAKO......... NASIKIA NI CHANZO CHA UTAJIRI.
 
Mkuu usifike uku kwasababu wamekutoa ujinga na kukufusha ngazi zote ulizopitia, sema tu wameonesha wanaudhaifu na ulimbukeni mkubwa
Sio wajinga,mshenzi sana huyo,
Kama watu serikali kuu wanalipwa milioni mbili lakini ndio wezi balaa na Wala Rushwa,unategrmea Mwalimu mwenye mshahara wa laki tatu aishi vipi!
 
kama mwalimu anaweza akakubali kununua heleni za shaba au saa kwa milioni tano ili aingizwe qnet, mishahara ya walimu ni kiasi gani?
 
Kama mpaka leo hujui qnet tuna jamii isiyo na taarifa ndo maana wanazidi kupiga watu
Sasa badala mumjibu mnampondea!

Me mwenyewe ni mwalimu wa msingi na siijui hiyo kitu pia. Si ajabu hata wewe mwenyewe hujui sawa na sisi tu
 
Sio wajinga,mshenzi sana huyo,
Kama watu serikali kuu wanalipwa milioni mbili lakini ndio wezi balaa na Wala Rushwa,unategrmea Mwalimu mwenye mshahara wa laki tatu aishi vipi!
sasa mwalimu wa lakini tatu, milioni nne ya kununulia saa au walter filter ili aingize Qnet, anaitoa wapi?....
 
Back
Top Bottom