Watoto kutoka Mtwara, Singida, Nairobi n.k wakutwa katika mazingira yasiyo rafiki ya malazi huku wakikosa elimu dunia msikitini Kiluvya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani nchini Tanzania wakipatiwa mafunzo ya kidini.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akiwa na Kamati ya Ulinzi wamefanya ziara kwenye Msikiti huo ili kujionea mazingira ambayo watoto hao wanaishi. DC Magoti amesikitishwa na mazingira aliyoyakuta na kusema siyo salama kwa watoto hao ambao wengine walipaswa kuwa shule.
DC amemtaka Sheikh wa Msikiti huo kusitisha huduma hiyo mara moja na kuamuru watoto hao kurudishwa kwa wazazi wao mara moja kufikia Jumamosi.
Sheikh wa Msikiti huo akijitetea amesema kuwa wanawalea watoto hao kwakuwa Msikiti huo pia unafundisha Kuhifadhi Quran hivyo wamekuwa wakiendesha programu hiyo. Akijibu kuhusu wanakopata watoto hao amesema kuwa wanatoka mikoa mbalimbali nchini na wamekuwa wakiletwa na wazazi kwa mapenzi yao.
Kuhusu huduma ya chakula, sheikh huyo amesema kuwa wamekuwa wakipata ufadhili wa wazazi wa watoto hao ambao huchanga kwa ajili ya chakula.
Watoto wakihojiwa na DC Magoti wameonesha kuwa na baraka za wazazi wao, wengine wamedai wanasoma huko lakini wengi wao wakionesha kuishia darasa la saba na kujiunga na mafunzo hayo
DC Magoti amemtaka Sheikh huyo kufika kituo cha Polisi Kisarawe ili kuandikisha maelezo ya kina kuhusu kilichotokea na kujifunga kuwa anaondoa huduma hiyo.
Pia soma;
DC wa Kisarawe, Petro Magoti achangia Mifuko 300 ya Saruji Ujenzi wa bweli la Msikiti, ahimiza na wengine wachangie ili Watoto Warudi mapema kusoma