Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.
Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.
Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.
Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.
Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.
(
Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)
Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.
Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.
Waislam kwa kuthamini elimu ndiyo wanawapeleka watoto wao katika shule hizi za ''kimasikini,'' kusoma.
Hatuna ubavu wa kushindana na shule za Wengine ambazo zinapewa ruzuku mabilioni ya kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM) katika ya Serikali na Makanisa.
Yapo mengi katika matatizo yanayowakabili Waislam moja wapo ilikuwa NECTA kuhujumu shule za Waislam.
Naamini unayajua maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.
Tutoke hapo.
Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?
Angalia ushahidi huo hapo chini:
View attachment 3039350
Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.
Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?