Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Hapa Magoti pamoja na kamati ya ulinzi wapewe heko,hivi vitu ukivichekea linaweza kiharibu usalama wa taifa.

Wazazi wajibikeni hao watoto ni jukumu lenu kwalea na kuwaongoza, unamwacha mtoto hujui anafundishwa nini,hujui anakula vipi na analala vipi,yaani kizazi cha mbele sijui kitakuwaje.

Unaweza ukakuta vituo kama hivi vipo vingi sana,misako kama hii inatakiwa ifanyike kila Wilaya tena kwa kushtukiza.
 
Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.

Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.

Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.

Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.

Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)

Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.

Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.

Tutoke hapo.

Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?

Angalia ushahidi huo hapo chini:

View attachment 3039350

Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.

Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?
Tatizo si ubovu wa jengo, ni mazingira ya kulala pamoja kwenye mkeka zaidi ya vijana 100.
 
Ghafla Cabo Delgado itahamia hapo Kisarawe Serikali iwe Macho na kama Wazazi wanataka kusomesha Dini Watoto wao wawapeleke Shule za Dini zilizosajiliwa na Serikali.

Cabo Delgado ikihamia hapa Nchini Magaidi kutoka pande zote za Dunia watakuja hapa tutakuwa Wageni wa nani sisi Watanzania?!
 
Hapa Magoti pamoja na kamati ya ulinzi wapewe heko,hivi vitu ukivichekea linaweza kiharibu usalama wa taifa.

Wazazi wajibikeni hao watoto ni jukumu lenu kwalea na kuwaongoza, unamwacha mtoto hujui anafundishwa nini,hujui anakula vipi na analala vipi,yaani kizazi cha mbele sijui kitakuwaje.

Unaweza ukakuta vituo kama hivi vipo vingi sana.
Joseph,
Ikiwa kuna ushahidi kuwa watoto hawa wanafunzwa ugaidi hili ni kosa la jinai.
Walimu wakamatwe wafikishwe mahakamani.

Haipendezi kuwa unatoa shutuma zisizo na ushahidi.

Hawa watoto wangekuwa hawali waingekuwa kama wanavyoonekana kwenye video.

Una la kusema kuhusu shule hii hapo chini?:
1720695733998.png
 
Kuanzia 2021-2024 nimebahatika kuishi mikoa 3-4 tofauti, 1 ukanda wa pwani ambapo nipo kwa sasa na hapo mtaani ipo na kote zilikuwepo madrasa zenye hao watoto wanaishi na kutunzwa humo kutoka ni kwa nadra sana, ni km wanajificha hivi, kinachofanyika humo hakijulikani hata kwa majirani kati ya hizo sehemu ni madrasa 2 nilikuwa jirani wa karibu,

ukichimba sana hizi ishu huwa zinaibuka pindi tu rais akiwa muislam,, kuna nini?
 
Naby...
Mimi niko tayari kufanya mjadala ambao utakuwa na manufaa kwetu sote na hata kwa viongozi wetu wa serikali.

Kuniita mimi Al Shabab ni kunivunjia heshima.

Acha hayo tufanya mjadala wa kiungwana na kuheshimiana tutawavutia wengi ama kuchangia au kuwa wanakuja kusoma na kuelimika.

Kwani DC na Kamati ya Amani wamevamia Msikiti usiku wa manane kwa kuwa wana taarifa kuwa wanetu pale hawasomi Qur'an ilia ugaidi?

Mimi nilichomsikia DC akisema ni kuwa mazingira wanayosomea watoto ni hatarishi hakusema lolote kuhusu ugaidi.
Nionavyo mimi sijui wengine, tatizo ni uongozi wa kituo kutowajali hao wanafunzi kwa kutanguliza maslahi yao mbele ya kutokujenga mabweni ya kulala hao wanafunzi kama yafanyavyo baadhi ya Makanisa na vituo vyao na badala yake wanawalaza Msikitini ilihali wazazi wao wanalipa ada, hata Shehe Mohamed Said hutokubali mjukuu wako akasome kwenye kituo kama hicho.
 
Kuanzia 2021-2024 nimebahatika kuishi mikoa 3-4 tofauti, 1 ukanda wa pwani ambapo nipo kwa sasa na hapo mtaani ipo na kote zilikuwepo madrasa zenye hao watoto wanaishi na kutunzwa humo kutoka ni kwa nadra sana, ni km wanajificha hivi, kinachofanyika humo hakijulikani hata kwa majirani kati ya hizo sehemu ni madrasa 2 nilikuwa jirani wa karibu,

ukichimba sana hizi ishu huwa zinaibuka pindi tu rais akiwa muislam,, kuna nini?
Kape...
Unataka jamii ikuamini wewe kuwa utakuwa unajua hali ya usalama kushInda vyombo vya usalama?

Unataka tuamini kuwa hivyo vyuo kwa kuwa vinawatunza watoto na kuwasomesha na watoto hawazururi basi ni magaidi?

Nimesoma taarifa hiyo hapo chini kutoka kwa msomaji wangu kaniletea hivi punde:

''Kosa pale liko wapi, watoto kulala msikitini chini msikitini?

He! Mbona hospitalini tena hospitali za Serikali wagonjwa wakiwemo wazazi wanalala chini na vichanga vyao?

Waliomaliza shule wanakatazwaje kutufuta kazi/ujuzi wanaoutaka?
Yako mengi ya kuhoji.

Kuna Kanisa hapa jirani na nyumbani kwangu kuna godown limechukuliwa na mchungaji anaitwa Magembe, jumba hili limechakaa na mabati juu yanang'oka na hatari wakati wa upepo, cha ajabu kuna wakati watoto wanatumia vumba kama madarasa na mikusanyiko ya kidini kila siku.''
 
Hii dini ni ya ajabu sana
Hiyo ni sawa na boarding tu,Cha ajabu nini!?..wamekua wakifanya hivyo tangu ikulu ni madrasa,wakilala palepale ocean road,mzee mwinyi alipopelekwa Zanzibar kusoma alipelekwa kwenye shule Kama hizo!..na akaja kuwa rais asiyewatia dhiki watu aliowaongoza Wala kuwazuwia kutoa maoni
 
Kuanzia 2021-2024 nimebahatika kuishi mikoa 3-4 tofauti, 1 ukanda wa pwani ambapo nipo kwa sasa na hapo mtaani ipo na kote zilikuwepo madrasa zenye hao watoto wanaishi na kutunzwa humo kutoka ni kwa nadra sana, ni km wanajificha hivi, kinachofanyika humo hakijulikani hata kwa majirani kati ya hizo sehemu ni madrasa 2 nilikuwa jirani wa karibu,

ukichimba sana hizi ishu huwa zinaibuka pindi tu rais akiwa muislam,, kuna nini?
Kusema hizi issue huwa zinaibuka tu rais akiwa muislam ni kuli potofu, haya mambo hayanantime line? Why not kipindi cha jk, why not kipindi cha mwinyi?

Why now?
 
Kape...
Unataka jamii ikuamini wewe kuwa utakuwa unajua hali ya usalama kushunda vyombo vya usalama?

Unataka tuamini kuwa hivyo vyuo kwa kuwa vinawatunza watoto na kuwasomesha na watoto hazururi basi na magaidi?
Sitafuti kuaminiwa nimechangia mada kuwa hizo madrasa zinazolea watoto zipo sio hiyo ya kisarawe tu huenda hiyo ikawa na idadi kubwa ya watoto tu, lakini hizo madrasa zipo sehemu nyingi tu tatizo ni usiri unaoendelea ndani ya hizo madrasa!

Habari za ugaidi umezileta wewe kumbe ndo kinachofundishwa?
 
Kusema hizi issue huwa zinaibuka tu rais akiwa muislam ni kuli potofu, haya mambo hayanantime line? Why not kipindi cha jk, why not kipindi cha mwinyi?

Why now?
Fatilia hizi story uzuri hatuna awamu nyingi kihivyoo
 
Mimi nina wasiwasi majority ya hawa watoto wanatokea Mtwara, Lindi na Pwani kunani? Na huyo sheikh hakumpa taarifa Sheikh Mkuu wake wa wilaya na alikuwa tayari kukubali kosa haraka sana kuliko kawaida kama vile kuna kitu anaficha! Naomba uchunguzi jamani!
 
Huyu nae badala ya kujiuliza nani kawaleta hapo na je wazazi wanajua hilo?
Na kama wanajua wameangalia maisha wanayoishi watoto na je wanafundishwa nini hapo?

Lazima kuangalia chanzo na kama wamevunja sheria wachukuliwe hatua ila kama ni child slavery lijulikane pia wanalimishwa na nani?

Kabla ya kufika maamuzi ya kuwaondoa hapo ingebidi awajuishe wazazi pia kuwa waje wawachukuwe watoto wao

Tatizo letu hatujui kutatua matatizo
Serikali igharamie watoto kwa kuhakikisha wanachukuliwa salama

Je kama wakipelekwa kwingine na kufichwa tena
Au Magoti anataka kuona hakuna watoto hapo kwa masaa 24 bila kujua watapelekwa wapi

Tumieni akili basi
 
Mimi nina wasiwasi majority ya hawa watoto wanatokea Mtwara, Lindi na Pwani kunani? Na huyo sheikh hakumpa taarifa Sheikh Mkuu wake wa wilaya na alikuwa tayari kukubali kosa haraka sana kuliko kawaida kama vile kuna kitu anaficha! Naomba uchunguzi jamani!
Sheik mkuu wa wilaya ni bakwata, waislam hawana time na bakwata,wanajua ni mkono wa serikali,Kuna taasisi nyingi za kiislam zinafanya mambo yao bila kumtaarifu sheikh mkuu wa wilaya
 
Huu ni muito kwa serikali kuongeza umakini hasa mkoa wa pwani na misikiti yake bila kusahau wahubiri wa kiislamu wenye msimamo mkali lakini wasiishie huko tuu yawezekana zipo sehemu nyingine nyingi kama hizo wanuse na kumulika kote, Msumbiji walidharau vitu vidogo vidogo kama hivyo mwisho kila kitu kimeharibika
 
Yaani nimesoma haraka haraka, nikajua imeandikwa kamati ya uzinzi. Kumbe ni bwana Magoti kawashtukiza Msikitini, waongee nao na kupata maelezo, hata watoto wahojiwe je wako hapo kwa kupenda ama wametoroshwa makwao. Jibu litapatikana tu.
Bantu...
Kwa nini watotowatoroshwe?

Wangekuwa wametoroshwa kungekuwa na ulinzi hapo msikitini kuwalinda wasikimbie.
 
Back
Top Bottom