Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Kiongozi jenga utamaduni wa kushughulikia chanzo cha tatizo au chanzo cha uvunjifu wa sheria/utaratibu nk nani aliwaleta hapo hao watoto, kwa vibali gani..lengo ni nini? nk ili isije rudiwa tena na wale walioanzisha hili jambo wachukuliwe hatua wao binafsi. Sasa fungeni kituo, halafu baada ya muda wanakwenda kuanzisha jambo hilo hilo sehemu nyingine!
Fikiria mara mbili juu ya ushauri wako

Hilo jambo ni jema shida hapo ni kwamba halikufanywa Kwa utaratibu maalum na Wala halikuwekewa mazingira mazuri katika utekelezaji wake.

Kitu cha kwanza ni kusitisha then kutoa maelekezo Kwa muhusika namna gani anaweza kufanya Hilo jambo Kwa utaratibu na kuweka mazingira salama Kwa wahusika na baada ya hapo anaweza kuendelea.

Mara nying penda kuangalia kitu kimefanywa Kwa Nia gan na ipi ni athari yake.

Wala sion shida juu ya uamuzi aliochukua wakufunga na kumtaka muhusika afuate utaratibu na kutengeneza mazingira salama Kwa wototo.

Hata leo ukienda kwenye baadhi ya shule za boarding za serikali utakuta vitanda vina kunguni, vyoo vichafu mazingira machafu kiujumla, je hili litakufanya uifute shule?

Angalia wapi pameleta tatizo, wakati mwingine njia isiyosahihi ikitumika kutatulia tatizo huleta tatizo zaidi.
 
Hapa Magoti pamoja na kamati ya ulinzi wapewe heko,hivi vitu ukivichekea linaweza kiharibu usalama wa taifa.

Wazazi wajibikeni hao watoto ni jukumu lenu kwalea na kuwaongoza, unamwacha mtoto hujui anafundishwa nini,hujui anakula vipi na analala vipi,yaani kizazi cha mbele sijui kitakuwaje.

Unaweza ukakuta vituo kama hivi vipo vingi sana,misako kama hii inatakiwa ifanyike kila Wilaya tena kwa kushtukiza.
Mzazi anajua mtoto anavyofundisha.
Kuhusu kula, hujaona hapo waneandika wazazi wanachangia chakula?
 
Magni...
Hayo ni mazingira ya kawaida sana kwa familia nyingi nchini petu.

Kuna picha nyingi za shule mbovu au hujaziona?

Shule hizi hazijavamiwa usiku wa manane na DC wala Kamati ya Usalama.
Hakika mzee ile mito ya pombe na wale mabikira 72 utazidishiwa wewe utapewa 100 kabisa kwa kumpigania Allah subhanau wataala
 
Surrat
Watoto kutoka Mtwara, Singida, Nairobi n.k wakutwa katika mazingira yasiyo rafiki ya malazi huku wakikosa elimu dunia msikitini Kiluvya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani nchini Tanzania wakipatiwa mafunzo ya kidini.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akiwa na Kamati ya Ulinzi wamefanya ziara kwenye Msikiti huo ili kujionea mazingira ambayo watoto hao wanaishi. DC Magoti amesikitishwa na mazingira aliyoyakuta na kusema siyo salama kwa watoto hao ambao wengine walipaswa kuwa shule.

DC amemtaka Sheikh wa Msikiti huo kusitisha huduma hiyo mara moja na kuamuru watoto hao kurudishwa kwa wazazi wao mara moja kufikia Jumamosi.

Sheikh wa Msikiti huo akijitetea amesema kuwa wanawalea watoto hao kwakuwa Msikiti huo pia unafundisha Kuhifadhi Quran hivyo wamekuwa wakiendesha programu hiyo. Akijibu kuhusu wanakopata watoto hao amesema kuwa wanatoka mikoa mbalimbali nchini na wamekuwa wakiletwa na wazazi kwa mapenzi yao.

Kuhusu huduma ya chakula, sheikh huyo amesema kuwa wamekuwa wakipata ufadhili wa wazazi wa watoto hao ambao huchanga kwa ajili ya chakula.

Watoto wakihojiwa na DC Magoti wameonesha kuwa na baraka za wazazi wao, wengine wamedai wanasoma huko lakini wengi wao wakionesha kuishia darasa la saba na kujiunga na mafunzo hayo

DC Magoti amemtaka Sheikh huyo kufika kituo cha Polisi Kisarawe ili kuandikisha maelezo ya kina kuhusu kilichotokea na kujifunga kuwa anaondoa huduma hiyo.

Surrat ......inamhusu kazikwenu
 
NI KAWAIDA KABISA HIZO NI BOARDING ZA ELIMU YA DINI YA KIISILAMU.

tatizo ni kwamba ikionekana watu wanalala katika misikiti watu hudhani wanafundishana ugaidi.

lakini kimsingi boarding kama hizo za masomo ya kiisilamu zipo nyingi sana Nchi hii katika mikoa mingi.

na boarding hizo hufundisha masmo ya kawaida kabisa katika uisilamu.

Kama vile kuhifadhi Qurani,kusoma hadithi,fiqhi,lugha ya kiarabu n.k

Japokuwa wstu wabaya hupitisha ajenda yao popote pale na hivyo hatà huko wapo wachache wanaweza kutumia huo upenyo.

Ila kimsingi Hapo hakuna viashiria vyovyote vya ugaidi.
Kwa hiyo watoto wanakuwa wanafundishwa elimu akhera tu? Vipi kuhusu elimu dunia??
 
Kape...
Unataka jamii ikuamini wewe kuwa utakuwa unajua hali ya usalama kushInda vyombo vya usalama?

Unataka tuamini kuwa hivyo vyuo kwa kuwa vinawatunza watoto na kuwasomesha na watoto hawazururi basi ni magaidi?

Nimesoma taarifa hiyo hapo chini kutoka kwa msomaji wangu kaniletea hivi punde:

''Kosa pale liko wapi, watoto kulala msikitini chini msikitini?

He! Mbona hospitalini tena hospitali za Serikali wagonjwa wakiwemo wazazi wanalala chini na vichanga vyao?

Waliomaliza shule wanakatazwaje kutufuta kazi/ujuzi wanaoutaka?
Yako mengi ya kuhoji.

Kuna Kanisa hapa jirani na nyumbani kwangu kuna godown limechukuliwa na mchungaji anaitwa Magembe, jumba hili limechakaa na mabati juu yanang'oka na hatari wakati wa upepo, cha ajabu kuna wakati watoto wanatumia vumba kama madarasa na mikusanyiko ya kidini kila siku.''
Hujaona shimo la kinyesi lililofunikiwa na turubai tu??
 
Volo...
Tujadiliane kwa heshima.
Hapana haja ya kutukana.

Kwani hauruhusiwi kulala msikitini?

Waislam kulala msikitini ni jambo la kawaida sana na limekuwa likifanyika karne kwa karne.
Watoto wadogo wanatakiwa wawe shule za kusomea elimu dunia, sio kushinda na kulala kwenye nyumba za dini.
 
Elimu ya mtoto wako unaiweka rehani kwa mtu usiyemjua? Halafu kesho kushinda kuandika jinsi mfumo kristu unavyowapendelea wakristu?
Nina hakika, huyo shekhe hana analolijua. Anawalea na kuwafundisha watoto ubabaishaji tu. If the parent does not want to hold the responsibilities of their own families, who else can bother or care?
Wenye watoto wamesema hawamjui?
Vipi wanaopeleka watoto wao shule za boarding?
 
Mzazi anajua mtoto anavyofundisha.
Kuhusu kula, hujaona hapo waneandika wazazi wanachangia chakula?
Kuchangia ndio kujua mtoto anakula chakula kipi? Vip unajua hao wakiumwa wanatibiwa vipi? Vp Mzingira yanayo wazunguka hao watoto? Kesho kukitokea mlipuko wa magonjwa wa kwanza kulaumiwa serikali kumbe uzembe wao wenyewe.

Hajakatazwa kuanzisha hiko kituo,ila kuna mamlaka,zipo kuna maafisa afya na ustawi wa jamii wapo na kuna chombo kinacho simarni imani yake kipo angenda huko halafu uone kama DC angemsumbua.
 
NI KAWAIDA KABISA HIZO NI BOARDING ZA ELIMU YA DINI YA KIISILAMU.

tatizo ni kwamba ikionekana watu wanalala katika misikiti watu hudhani wanafundishana ugaidi.

lakini kimsingi boarding kama hizo za masomo ya kiisilamu zipo nyingi sana Nchi hii katika mikoa mingi.

na boarding hizo hufundisha masmo ya kawaida kabisa katika uisilamu.

Kama vile kuhifadhi Qurani,kusoma hadithi,fiqhi,lugha ya kiarabu n.k

Japokuwa wstu wabaya hupitisha ajenda yao popote pale na hivyo hatà huko wapo wachache wanaweza kutumia huo upenyo.

Ila kimsingi Hapo hakuna viashiria vyovyote vya ugaidi.
Ustaadhi Dil limebuma!

Pia Tunataka kujua wanafundisha Nini
Je ni kuanana ugaidi?

Lakini wizara ya elimu Ina miongozo ya idada kwa afya mdugu
 
The Best,
Waislam wa kawaida siku zote wamekuwa masikini na ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa matumaini kuwa uhuru ukipatikana dhulma ya kubaguliwa itatoweka.

Uhuru umekuja na changamoto ñyingi kwa Uislam na Waislam.

Uislam ndiyo dini pekee iliyopata kufanya maandamano na si mara moja dhidi ya serikali.

Hakuna taasisi ya Waislam inayowanyonya Waislam na ikiwa una ushahidi huo ulete hapa.

Wala hakuna hicho unachodai kipo cha imani kali.

Hizi ni propaganda tu.
Wewe mzee umechanganyikiwa kabisa na dini, umekuwa muongo na mzandiki wa dini kupitiliza hata kwa mambo yanayoonekana wazi kabisa, pathetic.
 
Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.

Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.

Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.

Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.

Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)

Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.

Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.

Waislam kwa kuthamini elimu ndiyo wanawapeleka watoto wao katika shule hizi za ''kimasikini,'' kusoma.

Hatuna ubavu wa kushindana na shule za Wengine ambazo zinapewa ruzuku mabilioni ya kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM) katika ya Serikali na Makanisa.

Yapo mengi katika matatizo yanayowakabili Waislam moja wapo ilikuwa NECTA kuhujumu shule za Waislam.

Naamini unayajua maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.
Tutoke hapo.

Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?

Angalia ushahidi huo hapo chini:

View attachment 3039350

Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.

Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?
kaka Mohamed sipendi kubishana na wewe lkn kuleta picha nakuuliza Kwa Nini hazivamiwi usiku siyo sawa kabisa,hiyo ni shule ya msingi na inatumika mchana tu,ukivamia usiku hukuti mtu hapo.asubuhi iwe njema kakangu.
 
Bagamoyo,
Rejea kwenye hiyo video uitazame na usikilize ukiwa makini.
Hakuna mwanafunzi yeyote kutoka nje ya Tanzania.

Rejea usikilize tena hao wanafunzi wengi wameishia darasa la saba na wameletwa hapo na wazee wao waje wasome dini.

Tatizo labda liko hapa.
Nimetumia neno ''labda'' kwa makusudi ili ikiwa lipo tatizo lingine lisemwe.

Ikiwa wewe ni Muislam hutopata tabu unapambiwa watoto wengi wa Kiislam huishia darasa la saba.

Kitwana Kondo alipata kulizungumza hili Bungeni.
Nakuwekea hotuba yake uisome.

(Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999)

Waislam waliofanyiwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza majority yaani wengi walikuwa Waislam na Wengine walikuwa ndiyo wachache.

Waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza wengi walitoka katika wale Wengine na Waislam wakawa wachache.

Waislam kwa kuthamini elimu ndiyo wanawapeleka watoto wao katika shule hizi za ''kimasikini,'' kusoma.

Hatuna ubavu wa kushindana na shule za Wengine ambazo zinapewa ruzuku mabilioni ya kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM) katika ya Serikali na Makanisa.

Yapo mengi katika matatizo yanayowakabili Waislam moja wapo ilikuwa NECTA kuhujumu shule za Waislam.

Naamini unayajua maandamano ya Waislam mwaka wa 2012.
Tutoke hapo.

Kama tatizo la kuvamia msikiti usiku wa manane DC na Kamati ya Amani mbona kuna shule za mbovu kupita kiasi hazijavamiwa na wanafunzi kurudishwa makwao?

Angalia ushahidi huo hapo chini:

View attachment 3039350

Upo ushahidi mwingi lakini tuanze na huu.

Nipe jibu kwa nini shule hii haijavamiwa usiku wa manane na DC na Kamati ya Usalama?
Hapa tatizo sio moja mzee wangu. Matatizo na mashaka ni mengi ila tujiulize maswali haya:

1. Je, wana vibali halali kufanya hiyo programu?
2. Je, hiyo programu haiathiri elimu ya hao watoto?
3. Je, mazingira salama kwa mtoto ni mazingira ya aina gani?

Wakati tunajibu maswali haya tuyajibu kwa kuziangalia pia sheria zifuatazo

1. Sheria ya mtoto ya 2009
2. Sheria ya elimu (Marejeo ya 2019)
3. Kanuni ya Adhabu (Marejeo 2022)
4. Sheria ya vyama vya kijamii
5. Katiba ya JMT

Hapa hata ikiwa kuna sehemu zingine zenye mambo kama hayo, haihalalishi yoyote kuachwa afanye mambo hayo.

Ukiangalia hapo wanasema watoto hao wamemaliza darasa la saba. Wanaona kama huo ni utetezi kuwa hao watoto wamemaliza shule hivyo hawajakatisha masomo. Hii inaonesha ni namna gani hata viongozi hao hawafahamu mabadiliko ya sera ya elimu kuwa elimu ya msingi inaishia kidato cha nne.

Hao watoto mpaka hapo wamekatishwa masomo jambo ambalo ni kinyume na sera ya elimu, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya mtoto pamoja na Sheria ya elimu. Na swala hili ni kosa la jinai. Je, hapo tunatokaje? Sheria ikifuatwa watasema wanaonewa, busara ikitumika wanasema wanaonewa.

Kwanini programu hiyo isifanyike kwenye shule za seminari za kiislamu?

Kwani hao vijana wanaandaliwa kuwa wakina nani?, je, wanaandaliwa kuwa watu tofauti na wale wanaosoma seminari za kiislamu?

Sheria na taratibu za nchi zifuatwe.
 
Back
Top Bottom