Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Fikiria mara mbili juu ya ushauri wako

Hilo jambo ni jema shida hapo ni kwamba halikufanywa Kwa utaratibu maalum na Wala halikuwekewa mazingira mazuri katika utekelezaji wake.

Kitu cha kwanza ni kusitisha then kutoa maelekezo Kwa muhusika namna gani anaweza kufanya Hilo jambo Kwa utaratibu na kuweka mazingira salama Kwa wahusika na baada ya hapo anaweza kuendelea.

Mara nying penda kuangalia kitu kimefanywa Kwa Nia gan na ipi ni athari yake.

Wala sion shida juu ya uamuzi aliochukua wakufunga na kumtaka muhusika afuate utaratibu na kutengeneza mazingira salama Kwa wototo.

Hata leo ukienda kwenye baadhi ya shule za boarding za serikali utakuta vitanda vina kunguni, vyoo vichafu mazingira machafu kiujumla, je hili litakufanya uifute shule?

Angalia wapi pameleta tatizo, wakati mwingine njia isiyosahihi ikitumika kutatulia tatizo huleta tatizo zaidi.
 
Mzazi anajua mtoto anavyofundisha.
Kuhusu kula, hujaona hapo waneandika wazazi wanachangia chakula?
 
Magni...
Hayo ni mazingira ya kawaida sana kwa familia nyingi nchini petu.

Kuna picha nyingi za shule mbovu au hujaziona?

Shule hizi hazijavamiwa usiku wa manane na DC wala Kamati ya Usalama.
Hakika mzee ile mito ya pombe na wale mabikira 72 utazidishiwa wewe utapewa 100 kabisa kwa kumpigania Allah subhanau wataala
 
Surrat

Surrat ......inamhusu kazikwenu
 
Kwa hiyo watoto wanakuwa wanafundishwa elimu akhera tu? Vipi kuhusu elimu dunia??
 
Hujaona shimo la kinyesi lililofunikiwa na turubai tu??
 
Volo...
Tujadiliane kwa heshima.
Hapana haja ya kutukana.

Kwani hauruhusiwi kulala msikitini?

Waislam kulala msikitini ni jambo la kawaida sana na limekuwa likifanyika karne kwa karne.
Watoto wadogo wanatakiwa wawe shule za kusomea elimu dunia, sio kushinda na kulala kwenye nyumba za dini.
 
Wenye watoto wamesema hawamjui?
Vipi wanaopeleka watoto wao shule za boarding?
 
Mzazi anajua mtoto anavyofundisha.
Kuhusu kula, hujaona hapo waneandika wazazi wanachangia chakula?
Kuchangia ndio kujua mtoto anakula chakula kipi? Vip unajua hao wakiumwa wanatibiwa vipi? Vp Mzingira yanayo wazunguka hao watoto? Kesho kukitokea mlipuko wa magonjwa wa kwanza kulaumiwa serikali kumbe uzembe wao wenyewe.

Hajakatazwa kuanzisha hiko kituo,ila kuna mamlaka,zipo kuna maafisa afya na ustawi wa jamii wapo na kuna chombo kinacho simarni imani yake kipo angenda huko halafu uone kama DC angemsumbua.
 
Ustaadhi Dil limebuma!

Pia Tunataka kujua wanafundisha Nini
Je ni kuanana ugaidi?

Lakini wizara ya elimu Ina miongozo ya idada kwa afya mdugu
 
Wewe mzee umechanganyikiwa kabisa na dini, umekuwa muongo na mzandiki wa dini kupitiliza hata kwa mambo yanayoonekana wazi kabisa, pathetic.
 
kaka Mohamed sipendi kubishana na wewe lkn kuleta picha nakuuliza Kwa Nini hazivamiwi usiku siyo sawa kabisa,hiyo ni shule ya msingi na inatumika mchana tu,ukivamia usiku hukuti mtu hapo.asubuhi iwe njema kakangu.
 
Hapa tatizo sio moja mzee wangu. Matatizo na mashaka ni mengi ila tujiulize maswali haya:

1. Je, wana vibali halali kufanya hiyo programu?
2. Je, hiyo programu haiathiri elimu ya hao watoto?
3. Je, mazingira salama kwa mtoto ni mazingira ya aina gani?

Wakati tunajibu maswali haya tuyajibu kwa kuziangalia pia sheria zifuatazo

1. Sheria ya mtoto ya 2009
2. Sheria ya elimu (Marejeo ya 2019)
3. Kanuni ya Adhabu (Marejeo 2022)
4. Sheria ya vyama vya kijamii
5. Katiba ya JMT

Hapa hata ikiwa kuna sehemu zingine zenye mambo kama hayo, haihalalishi yoyote kuachwa afanye mambo hayo.

Ukiangalia hapo wanasema watoto hao wamemaliza darasa la saba. Wanaona kama huo ni utetezi kuwa hao watoto wamemaliza shule hivyo hawajakatisha masomo. Hii inaonesha ni namna gani hata viongozi hao hawafahamu mabadiliko ya sera ya elimu kuwa elimu ya msingi inaishia kidato cha nne.

Hao watoto mpaka hapo wamekatishwa masomo jambo ambalo ni kinyume na sera ya elimu, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya mtoto pamoja na Sheria ya elimu. Na swala hili ni kosa la jinai. Je, hapo tunatokaje? Sheria ikifuatwa watasema wanaonewa, busara ikitumika wanasema wanaonewa.

Kwanini programu hiyo isifanyike kwenye shule za seminari za kiislamu?

Kwani hao vijana wanaandaliwa kuwa wakina nani?, je, wanaandaliwa kuwa watu tofauti na wale wanaosoma seminari za kiislamu?

Sheria na taratibu za nchi zifuatwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…