Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Bantu...
Kwa nini watotowatoroshwe?

Wangekuwa wametoroshwa kungekuwa na ulinzi hapo msikitini kuwalinda wasikimbie.

Volo...
Tujadiliane kwa heshima.
Hapana haja ya kutukana.

Kwani hauruhusiwi kulala msikitini?

Waislam kulala msikitini ni jambo la kawaida sana na limekuwa likifanyika karne kwa karne.
Kupumzika baada ya swala sawa, ila si kufanya Msikiti kuwa bweni la kulala wanafunzi.
 
Kapeace,
Mahakama zipo endapo kuna kosa wapelekwe mahakamani.
 
Si mshutumu mtu ina naongea kwa kutumia experience ya Boko Haram,ukitizama Documentary walianza hivi hivi, leo Nigeria kuna maeneo haya tawaliki.

Halafu hilo darasa ni la serikali, hata content ya kinacho fundishwa serikali ndio wanakiandaa na kukimonitor,wana mifumo inayo tambulika ya kuandaa walimu.Halafu hapo wakimaliza kila mtoto anarudi kwa wazazi wake,still bado wazazi wanammonitor na kumlisha vizuri na hata akiumwa wanajua wamtibie vipi. Hivi kwa kuwaona tu inamaana ndio wanakula vizuri au wanatibiwa vizuri? Huwezi fananisha treatment ya mtu baki na ya mzazi kwa mtoto.

Leo nikikuambia silabasi wanayo tumia kufundisha watoto unayo/unaijua. Haya kama yasipo angaliwa yakitokea hayajali,ww ni dini gani,Boko Haram wanateka na kuwaangamiza mpaka wale wenye imani sawa na wao.
 
Kupumzika baada ya swala sawa, ila si kufanya Msikiti kuwa bweni la kulala wanafunzi.
Babuu.

Waislam hawana mabilioni wanayopokea Makanisa kutoka serikalini kupitia Memorandum of Understanding (MUM).

Waislam tunatumia kile kilicho chetu kujisaidia wenyewe na ndiyo hii misikiti ambayo tunayo mingi.

Tungekuwa na fedha kama hizo wanazopewa Wengine tungejenga mabweni mazuri kama wenzetu.
 
Joseph,
Soma historia ya Waislam wa Tanganyika achana na historia ya Nigeria.
Historia ya Nigeria ni tofauti sana na historia ya Tanzania.

Unaujua mchango wa Waislam wa Tanganyika katika kupigania uhuru wa Tanganyika?

Soma historia hii utaongeza maarifa yako.
 
Mkuu MS
Hehima yako mkuu

Hoja na picha uliyo ambatanisha kwangu mimi naona Haina mashiko Kwa sababu

1. Hii shule( s/m mlevo) sio ya bweni kwahiyo hata ikivamiwa usiku wa manane na kamati ya ulinzi na usalama hakuna kitu/watu watakuta hapo shule ni uchakavu tu wa jengo Lakini shughuli za ufundishaji na utekelezaji wa mtaala zinafuatwa

2. Hoja ni kitu gani kinafundishwa hapo ambacho kimewafanya wachukue watoto 90+kutoka kwa familia zao?je ni elimu ya Dini au kuna ajenda za Siri (chuki) zinapenyezwa apo?

3. Je mazingira yanaruhusu kuwaudumia hao watoto 90+ malazi mavazi na chakula ukizingatia hapo sio shule na Wala hakuna mabweni ya kuwalaza hao watoto?
 
Mohamed Said unajitahidi sana kuutetea Uislamu lakini ni dhahiri shahiri hoja nyingine hazina utetezi.
Babuu,
Unajitia hofu isiyokuwa na sababu.
Waislam wamefanya makubwa katika nchi hii.

Soma historia yao.

Soma historia ya Mtwa Abdallah Mkwawa, Abushiri bin Salim, Hassan Omari Makunganya, Khadija Mkomanile, Abdulrauf Songea Mbano, Kleist Abdallah Sykes na mwanae Abdulwahid Abdallah Kleist, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Haidar Mwinyimvua kwa kuwataja wachache.

Soma historia za watu hawa utawajua Waislam na mafunzo yao na alama walizoacha.


 
Ya Nigeria ni real example ya Boko Haram ilivyo anza ilianza hivi hivi,tatizo wao hawa kuyakemea na gundua mapema.

Kweli kiimani ni mkrisho,ila ukiniambia nichague amani ya nchi yangu na dini yangu,nitachagua amani ya nchi yangu,sababu kwenye amani hata ule utulivu wa kusali unaupata.

Sasa nikishaujua huo mchango wa dini yako,then .......... inahusiana nini na hiki kikicho tokea Kisarawe.
 
Hatari sana hii...
 
DC alifanya uchunguzi kutafuta content ya mafundisho yanayotolewa hapo?
DC alifanya uchunguzi kujua kwanini hao vijana wapo hapo?

Maeneo mengi ya Pwani huu ni utaratibu wa kawaida Kwa baadhi ya misikiti kuwa inatoa elimu ya kidini na uwepo wa wanafunzi kwenye shule hizo muda wote mpaka watakapohitimu.
 

Joseph,
Katika uandishi unaweka dot 3 ... zinatosha.
 
Lup...
Unajua kuwa Makanisa yanapokea ruzuku ya mabilioni kutoka serikalini na Waislam hawana firsa kama hiyo?
 
Hivi Mzee wangu unajua baadhi ya rejea hupoteza uhalisia wake baada ya muda mrefu kupita kutokana na mabadiliko kadhaa ambayo huwa yanatokea?
Kitendo cha kutumia rejea ya 1999 ambayo kiuhalisia kwasasa kuna mabadiliko makubwa kwenye baraza la Taifa la Mitihani na kuongezeka kwa ufaulu kutokana na ongezeko la shule nyingi za Sekondari kunapoteza credibility ya andiko lako.
Kinacholalamikiwa si uchakavu wa majengo wala vijana kukosa fursa ya kwenda Sekondari, bali Mkuu wa Wilaya ana detailed information kuwa kuna vijana wamefaulu na hawajaenda sekondari ila wamesafirishwa na wazazi wao kupelekwa hapo kupata hiyo elimu ya dini.
Huoni kuna kitu cha kufikirisha hapo juu ya kinachoendelea maana ukiachilia mbali shuleni kuwa na somo la dini na huko walipotoka kuna misikiti na madrasa, kwanini wakatishwe masomo walipotoka na kuletwa hapo ilihali hiyo elimu ya dini walikuwa wana uwezo wa kuipata hata huko walipotoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…