Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Waislam badilikeni vinginevyo kila wakati mtasema mnaonewa.

Mtoto akifeli darasa la saba siyo mwisho wa dunia au kumpeleka kwenye mafunzo ya dini , anapaswa kuendelezwa kwa mfumo mwingine wa elimu, kwa mfano kupitia mafunzo ya VETA au shughuli zozote zitakazoweza kumpatia Ujuzi ambao utamsaidia kujitegemea na kuendesha maisha yake, sasa hao watoto mnaowaficha huko misikitini na mabwenini mwisho wa siku mnataka wafanye shughuli gani za kuendesha maisha yao ikiwa hawana ujuzi wowote.?
 
Hao hapo hawajafuata sheria. Iko wazi kabisa, na MAZINGIRA ni hatarishi
 
From...
Unawafananisha Waislam masikini ya Mungu na Wakatoliki wanaopewa ruzuku ya mabilioni na serikali?

Unaijua Memorandum of Understanding (MUM)?
Si umeona hapo Kuna neno foundation unakuta inapokea mabillioni ya pesa mipesa kutoka kwa wafadhili zinaingia mifukoni mwenu huku mkiwatumia watoto kama chambo na kuhusu wakatokiliki kupewa fedha za uendeshaji wa taasisi zake ni zile taasisi zinazahudimia jamii kwa ujumla Sasa jiulize kama hospital kama bugando waislam hawatibiwi?
 
MUM au MoU ?
N
Na peponi hawaendi kwa sababu ya mtihani mkubwa wa umaskini walionao Waafrika.


Mpaka karne hii watu wanafungiwa kufundishwa dini tena kwa kukaririshwa sio kupanua maarifa ya kuhoji na kubaini ukweli na uhalisia wa hizi dini ambazo wale waliozipokea mwanzo hawana habari nazo zaidi ya kuhangaika na mali ili waondoe umaskini kwenye jamii zao
 
Pia ni vyema kuwasikiliza lengo na nia ya hao kuanzisha hicho kituo kama haitishii usalama sioni shida kwa maana tunatafutiana mitazamo na matarajio ya mbeleni, wengine hawana mpango na hii elimu ya darasani tayari wana mifumo yao ya jinsi ya kupata maisha uona kama inawapotezea mda tu.
 
Shekhe wangu Mzee Mohamed Said, kwa hili la Bagamoyo,ungeliacha tu lipite. Si jema kwa afya za watoto.
Kosa la mmoja halimhalalishi muovu
 
Ni kweli......lakini hapa mazingira ya kuishi vijana sio rafiki kabisa.......bila shaka umeona video fupi juu ya hayo mazingira. Ni bora kufunga na kufanya marekebisho ila vijana waishi maisha rafiki kwa elimu yao.
 
Huyo DC toka apelekwe huko ameonesha chuki za waziwazi kwa wenyeji wa huko na ni kama anajiona yeye ndiye anawaweza na atawakomesha,wacha tuone mwisho wake utakuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…