Kisasi ni haki, Yanga dhidi ya Rivers moto utawaka

Kisasi ni haki, Yanga dhidi ya Rivers moto utawaka

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Nakumbuka yanga waliondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa na Rivers baada ya kuchapwa goli moja bila kwa mkapa na kisha kufungwa tena moja bila kule Nigeria, Yanga walipoteza mechi zote mbili ktk mazingira tofauti.

Rivers walikutana na yanga iliyokuwa bado inajitafuta, ilikuwa ndio imesajili idadi kubwa sana ya wachezaji wapya na nakumbuka mashindano yale yalianza mapema sana ivyo yanga walikosa ata pre season inayoeleweka ili kuiunganisha timu kwa haraka, ni timu ambayo ilikuwa bado haina muunganiko mzuri walikuwa wanapambana kupata muunganiko kwenye kikosi kipya.

Na bado walipata shida nyingine ya key prayers wake kina Djuma shaban, Fistoni mayele na kharid aucho kukosa I.T.C ivyo walizikosa mechi zote 2 dhidi ya Rivers, Walienda Nigeria wakabambikiwa corona kitendo kilichofanya mchezo uchelewe kuanza lakini kwa busara za match kamishna wachezaji waliokuwa wamebambikiwa waliruhusiwa kucheza, Sasa kwa mara nyingine tena Rivers ametua mikononi mwa yanga.

Ametua kwenye kipindi ambacho yanga ile iliyokuwa inajitafuta imeshajipata, Wametua mbele ya yanga iliyo kwenye ubora wake kwa sasa, wametua mbele ya yanga yenye kiu kubwa ya mafanikio ktk mechi za kimataifa, Wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wana hasira kubwa dhidi ya rivers kutokana na kile kilichotokea nyuma, kwa maana iyo na kwa kuangalia vikosi vya timu zote mbili na aina ya uchezaji wa timu zote mbili kwa sasa sioni Rivers wakichomoka mbele ya timu ya wananchi safari hii, Njia ya kwenda nusu fainali kwa yanga na kuandika rekodi yake mpya ni nyeupe, jeuri ya yanga ni kikosi walichonacho na benchi lao la ufundi wakiongozwa na Master Nabi, Kila la kheri wananchi!

NB: Mashabiki wa Rivers wajitokeze mapema tuwajue wasijifiche kusubilia matokeo ndio waibuke.
 
TP Mazembe Congo Kuna Vita

Rivers Nigeria Kuna Boko Haram

Mpewe Nini Tena Utopolo?

Watani zetu wafundisheni tuu Amani huko muendako.
 
Mkipasuka sipati picha sura zenu mtaweka wapi
 
Mchezo hata hujachezwa MAKELELE meeengi mno.

Kila lakheri timu zote za Tanzania
 
Wakristu tunaamini.

Kisasi ni juu ya Mungu Mwenyewe

WARUMI 12:19.

Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Warumi 12:19
 
Nakumbuka yanga waliondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa na Rivers baada ya kuchapwa goli moja bila kwa mkapa na kisha kufungwa tena moja bila kule Nigeria, Yanga walipoteza mechi zote mbili ktk mazingira tofaut...
Na mashabiki wa yanga tuna hasira pia...
 
Niseme tu River United sio wepesi wepesi, cha msingi Yanga ikapate goli la ugenini, wakija kwa Mkapa timalize
 
Hawa Rivers wasipojichunguza vizuri watakula Hamtha kwao na kwa Mkapa,,,
Kama ni Rivers naiona Yanga hii ikipata njia nyeupe ya kuandika History kubwa ndani ya Africa hii
 
Endeleeni kuja na matokeo kama kawaida yenu,hamtaamini nawaambia,hao rivers walimnywa waydad 2 watashindwa kumlala utopolo,YANGA HAMTOI RIVERS.
 
Endeleeni kuja na matokeo kama kawaida yenu,hamtaamini nawaambia,hao rivers walimnywa waydad 2 watashindwa kumlala utopolo,YANGA HAMTOI RIVERS.
Ni mbili kwa moja halafu akapigwa goli sita marudiano
 
Back
Top Bottom