Kisayansi matembele sio mboga ni majani pori, tunayala sababu ya shida tu, kitaalumu mchicha ndiyo mboga halisi

Kisayansi matembele sio mboga ni majani pori, tunayala sababu ya shida tu, kitaalumu mchicha ndiyo mboga halisi

Wasukuma hawayapendi maana hawajui kuyapika wanaweka mchuzi,hiyo ni mboga ya pwani,tuachieni wana pwani
Tatizo wanachuma majani ya viazi halafu hawajui kuyapika matokeo yake wanapata mlenda halafu sio wasukuma tu makabila mengi huko vijijini wako hivyo,.wakija mjini siku ya mwanzoni hawali tembele.[emoji3][emoji3]
 
Mmejipata kidogo tu mmeanza kuona matembele sio mboga.

Infact matembele ni mboga nzuri sana ya asili yenye virutubisho na faida kwa mwili.

Matembele ni mboga yenye virutubisho vingi, na yanajulikana kwa kuwa na:
  1. Vitamini A - Inasaidia kwa afya ya macho na kinga ya mwili.
  2. Vitamini C - Inasaidia katika kuimarisha kinga ya mwili na afya ya ngozi.
  3. Madini ya chuma - Hii husaidia katika kuzuia upungufu wa damu.
  4. Nyuzinyuzi (Fibers) - Husaidia kuboresha mmeng'enyo wa chakula na kudhibiti uzito.
  5. Antioxidants - Husaidia kupambana na uharibifu wa seli na magonjwa mbalimbali.

Matembele pia yana faida katika kupunguza uchovu na kuimarisha afya ya mifupa.

Kisayansi matembele ni mboga.

NB: Acha kupotosha watu, Acha kudharau mboga za asili.
 
Ni mboga ya Majani niipendayo pia baada ya mlenda

Kuna Siku nilimsaidia waifu kupika hayo matembele, nikachanganya na dagaa wa Mwanza na ile pilipili inayonukia

Ni mboga nzuri sana, kama upo Mkoa wa Morogoro jaribu kuchanganya matembele na nguruka

Unaweza kusahau bei ya nyama January hii 🤗
 
Hizo mboga sili kabisa kwasababu zinanikumbusha nyakati ngumu sana tulizopitia na familia yangu nikiwa mdogo.
Nyakati ngumu?

Hizi mboga haitakiwi kula sababu ya nyakati ngumu, inatakiwa kula muda wote sababu ya virutubishi.

Ndiyo maana wazee wa zamani walikuwa Strong!!
 
Kumbe we ni wa Pwani?!
Ndo maana kila kitu una mention wasukuma tu!
Mtani huyo hana maana, tulikwenda.kuzika Kisaraweil miaka ya nyuma Sana, driver msukuma.tukafika sehemu wanapiga kelele dereva kuna mlima mrefu kweli.hapo mbele punguza mwendo [emoji3][emoji3] kumbe kamwinuko tu sikuwaacha salama [emoji3][emoji3] driver kapandisha na kushusha Sekenke ya zamani wanamwambia mlima Kisarawe!! Sina hamu nao
 
Kama tembele linaliwa na halina madhara basi ni chakula swaffi hizi Mambo za kisayansi mara ingine zisituvuruge... Zipo hoja za kisayansi zitakuduwaza zaidi.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Tafakuri ya kina kwa wenye hekima

Fuatilia kwa wataalamu wa tiba utathibitisha

Poleni mlioumizwa
......tafsiri yako tu mbaya....pori na mjini ...kwenye mboga ? Kupanga ni kuchagua rndelea tu utakavyo....mnafu no badala mchicha...kuna mchicha wa asili nao mzuri zaidi ule wako wa kizungu.....sasa wajua ugali wetu mahindi unadumaza akili ?? Inatakiwa tule ugaki ngano au muhogo mm nachanganya muhovo na ngano ndio ugali wangu past 10yrs nimeacha srmve kavu.....
 
Yanakwepana sana na mashine ya tumbo yanatoka kama yalivyoingia tofauti ladha!
 
Back
Top Bottom