Kisayansi matembele sio mboga ni majani pori, tunayala sababu ya shida tu, kitaalumu mchicha ndiyo mboga halisi

Kisayansi matembele sio mboga ni majani pori, tunayala sababu ya shida tu, kitaalumu mchicha ndiyo mboga halisi

Wadau hamjamboni nyote?

Tafakuri ya kina kwa wenye hekima

Fuatilia kwa wataalamu wa tiba utathibitisha

Poleni mlioumizwa
Mboga ya Matembele ni nzuri kiafya kuliko mboga ya mchicha haifai kabisa mchicha ni mboga yenye asidi haifai kuliwa na watu wanakula pasipo kuijuwa faida ya mboga ya mchicha. Mboaga ya matembele hata kama imejiotea porini inafaa kuliwa kwa sababu aliyeoteshani Mungu na kitu kijiotea mwenywe ni kizuri zaidi kuliko kilichopandwa na binadamu.

1737790649693.png

FAIDA ZA MBOGA YA MATEMBELE KWA UFUPI
1: Matembele yana madini ya chuma. Madini haya ndiyo muhimu katika utengenezaji wa damu, kwa hiyo mtu anapotumia matembele anakuwa anaongeza kiwango cha damu mwilini. Watu wenye upungufu wa damu na mama wajawazito wanashauriwa kula matembele kwa wingi.
2: Matembele yana vitamini A ambayo husaidia kuimarisha macho na hivyo kumsaidia mtu kuona vizuri hasa hasa nyakati za usiku.
3: Matembele yana vitamini C Ambayo humlinda mtu asipate kiseyenye (scurvy). Vitamini C huimarisha ngozi na fizi.
4: Matembele yana protini ambayo husaidia katika kuimarisha misuli na kusaidia katika ukuaji wa mwili.Watoto wanaokula matembele huwafanya wakue vizuri.
5: Matembele yanasaidia kuongeza damu kwa wingi mwilini ikiwa utayachemsha maji yake na kunywa kila siku.
6: Matembele yanasaidia kuongeza nuru na kuboresha afya ya macho
7: Matembe yanasafisha damu na kutoa mafuta machafu
8: Kamba lishe zilizo kwenye matembele ni chanzo cha kupata choo kikubwa vizuri
Kwani zinaboresha mfumo wa usagaji.
 
Wasukuma hawayapendi maana hawajui kuyapika wanaweka mchuzi,hiyo ni mboga ya pwani,tuachieni wana pwani
Umesema kweli wasukuma hawayawez matembele asee! Wanayaita MALANDO
 
Wala mchicha wengi haswa wa Dar mnalishwa chembechembe za samadi ya mwanadamu...
 
Back
Top Bottom