Kisheria ni watu wangapi wanatakiwa kushiriki uchaguzi mkuu ili uwe halali kisheria?

Kisheria ni watu wangapi wanatakiwa kushiriki uchaguzi mkuu ili uwe halali kisheria?

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Tume ya uchaguzi ilitangaza Mgombea wa CCM, Mhe Rasi, Samia Suluhu kushinda uchaguzi kwa kura zaidi ya 30M huku ikisema ni zaidi ya asilimia 97 na pointi huko.

Mimi ni mmoja ya watu wanaoamini matokeo ya tume yanamakosa. Watu 30M kwangu naona ni uongo. Kutokana na kilichokuwa kinaendelea siku ya October 29 hasa kwenye majiji makubwa.

Sina Shaka na 98% kwa sababu kiwango hicho kinapatikana katika idadi yoyote iwe 1000, laki moja, au milioni moja.

Shida ipo kwenye idadi ya 30M.

Swali langu la msingi, kisheria ili uchaguzi uwe uchaguzi mkuu ni watu wangapi wanatakiwa kushiriki kupiga kura katika uchaguzi huo?

Je kuanzia 100k, 1M, 5M au idadi ipi?
Ukizingatia kupiga kura ni haki lakini sio Haki ya Lazima. Yaani mtu anahiyari ya kwenda kupiga au kutokupiga kura.

Mfano, nchi nzima wajitokeze watu laki moja kupiga kura, wakamchagua Rais, je huo nao kisheria utaitwa uchaguzi mkuu na utakuwa halali kisheria?

Kama msingi wa Uchaguzi mkuu ni Demokrasia, ambapo wengi wapewe, sasa watu laki moja wakapiga kura alafu milioni 60 wakagoma kupiga kura, hiyo kisheria na kidemokrasia imekaaje?

Mawazo ya Wanasheria
Mawazo ya Wanafalsafa,
Huu ndio uwanja wenu.

Karibuni

TaikonMaster
Kwa sasa Mbweni, Dar es salaam
 
hakuna idadi ya chini au asilimia fulani ya wapiga kura (quorum) mkuu, atakaeshinda wenzake hatakama wapigakura ni 10 sawa tu
 
Kwa maana hiyo CCM ya Samia ipo kihalali
Uhalali wa "kisheria" wa Rais Tanzania unatokana na yeye kutangazwa na tume tu, haitaji hata kushinda uchaguzi kwa sababu matokeo yake hayahojiwi mahakamani, yani hata kama hiyo kura moja alipigwa mtu mwingine halafu tume ikamtangaza mtu mwingine kuwa ni mshindi hapo tayari anakuwa halali kisheria. Nafikiri unaweza kuelewa sasa Lissu anaposema "Ni reforms, No Elections''
 
Hoooohoo!
Basi kazi ipo.
Kwamba kuna uhalali wa kushinda na uhalali wa kutangazwa.
Na katika halali hizo mbili, uhalali mkubwa ni ule wa kutangazwa, si ndio?
 
Unapaswa ujifunze kutofautisha kati ya "legality" na "legitimacy".
Legality ni kutambulika kisheria bila kujali madaraka yamepatikanaje au Sheria kama mbaya au nzuri, Legitimacy ni kukubalika na sehemu kubwa ya jamii, kuwepo kwa haki, uungawana na ustaarabu.

Mfano Serikali ya Makaburu wa South Africa kabla 1994 ilikuwepo na ikawa inatambulika kisheria(legality) lakini haikuwa na uhalali wa kijamii(legitimacy), ilikuwa ni illegitimate government.

Sheria za kutenganisha weusi na Wazungu Marekani zilikuwepo kisheria na watu waliozivunja walifungwa kweli, Sheria zilikuwa na legality ila zillikuwa illegitimate.
 
Hoooohoo!
Basi kazi ipo.
Kwamba kuna uhalali wa kushinda na uhalali wa kutangazwa.
Na katika halali hizo mbili, uhalali mkubwa ni ule wa kutangazwa, si ndio?
Legality Vs Legitimacy,
Kuna kuwepo na kutambulika kisheria mamlakani bila kuwa na uhalali, kibali au kukubalika na wale unaowatawala kwa wingi wao.
Kiswahili kina msamiati haba, kinachanganya legality (uwepo/ kukubalika kisheria) na legitimacy (uhalali kijamii).
 
Legality Vs Legitimacy,
Kuna kuwepo na kutambulika kisheria mamlakani bila kuwa na uhalali, kibali au kukubalika na wale unaowatawala.
Kiswahili kina msamiati haba, kinachanganya legality (uwepo/ kukubalika kisheria) na legitimacy (uhalali kijamii).

Sahihi kabisa.

Kwamba jambo linaweza kuhalalishwa kisheria lakini lisiwe halali kijamii
 
Andiko lina nia ya kuihalalisha haramu kwa kutumia mtindio wa "expansion joints"!Lakini,kiuhalali na kimantiki/kisheria halali hakuna kitu hapo.Ndiyo maana,mtuhumiwa anaweza kushinda shauri au kupatikana na hatia kwa "ushahidi wa mazingira" unaom-pin down!
NB; Maridhiano bado yanahitajika(?)Kwa nini yahitajike huku upande fulani "ulipewa" asilimia 98 ya ushindi?Kwamba "mshindi" ana huruma,upendo,utu na maadili sana kuhusu ushirikishaji?
 
Hamjambo!

Tume ya uchaguzi ilitangaza Mgombea wa CCM, Mhe Rasi, Samia Suluhu kushinda uchaguzi kwa kura zaidi ya 30M huku ikisema ni zaidi ya asilimia 97 na pointi huko.

Mimi ni mmoja ya watu wanaoamini matokeo ya tume yanamakosa. Watu 30M kwangu naona ni uongo. Kutokana na kilichokuwa kinaendelea siku ya October 29 hasa kwenye majiji makubwa.

Sina Shaka na 98% kwa sababu kiwango hicho kinapatikana katika idadi yoyote iwe 1000, laki moja, au milioni moja.

Shida ipo kwenye idadi ya 30M.

Swali langu la msingi, kisheria ili uchaguzi uwe uchaguzi mkuu ni watu wangapi wanatakiwa kushiriki kupiga kura katika uchaguzi huo?

Je kuanzia 100k, 1M, 5M au idadi ipi?
Ukizingatia kupiga kura ni haki lakini sio Haki ya Lazima. Yaani mtu anahiyari ya kwenda kupiga au kutokupiga kura.

Mfano, nchi nzima wajitokeze watu laki moja kupiga kura, wakamchagua Rais, je huo nao kisheria utaitwa uchaguzi mkuu na utakuwa halali kisheria?

Kama msingi wa Uchaguzi mkuu ni Demokrasia, ambapo wengi wapewe, sasa watu laki moja wakapiga kura alafu milioni 60 wakagoma kupiga kura, hiyo kisheria na kidemokrasia imekaaje?

Mawazo ya Wanasheria
Mawazo ya Wanafalsafa,
Huu ndio uwanja wenu.

Karibuni

TaikonMaster
Kwa sasa Mbweni, Dar es salaam
In fact,
it's very simple.

Ni watu wa3 tu wakishiriki kupiga kura inatosha.
kwasababu kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, the winners takes all.

Kwa mfano,
watu watatu watakapopiga kura kisha mgombea moja akapata kura moja, na mgombea mwingine akapata kura mbili.
Then mgombea aliepata kura mbili anatangazwa kua mshindi wa uchaguzi huo kwa mujibu wa sheria,

na kwa niaba ya umma,
atatakiwa kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea waTanzania wote maendeleo endelevu ya kiuchumi, kisiasa na jamii.

Majirani zetu Kenya,
ndio wana ile 50+1, yaani mshindi wa uchaguzi mkuu ni lazima apate kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote, ndipo atangazwe mshindi. Na akikosekana mshindi wa 50+1, uchaguzi unaridiwa baina ya washindi wawili wa kwanza.

Visingizio na hisia za walioshindwa uchaguzi au kususia uchaguzi kwa hiyari zao, daima hutumika zaidi hamasa ya kuwatia moyo wafuasi wao kanakwamba siku ya unyakuo imekaribia 🐒
 
Mi nazan ili uchaguzi uwe halali inatakiwa kufuata mchakato wote wa uchaguzi kama sheria na katiba inavyotaka

Ata mgombea uraisi akiwa mmoja ni sawa cha msingi ni sheria na taratibu za uchaguzi zimefuatwa

Asante
 
Uchaguzi huwa halali ili mradi tu umeitishwa na mamlaka husika, umefuata taratibu zilizowekwa, na matokeo yatangazwe kulingana na kura zilizopigwa.

Legality ni suala la sheria, lakini legitimacy ni suala la imani ya wananchi. Serikali inaweza kushinda kesi mahakamani kwa kutumia legal victory lakini ikashindwa kuongoza kwa ufanisi kwa sababu haina imani ya wananchi.
 
Andiko lina nia ya kuihalalisha haramu kwa kutumia mtindio wa "expansion joints"!Lakini,kiuhalali na kimantiki/kisheria halali hakuna kitu hapo.Ndiyo maana,mtuhumiwa anaweza kushinda shauri au kupatikana na hatia kwa "ushahidi wa mazingira" unaom-pin down!
NB; Maridhiano bado yanahitajika(?)Kwa nini yahitajike huku upande fulani "ulipewa" asilimia 98 ya ushindi?Kwamba "mshindi"98 ana huruma,upendo,utu na maadili sana kuhusu ushirikishaji?

98% kihesabu iko katika idadi yoyote.
Lakini 30M hapo ndipo utata ulipo.

Turudi kwenye hoja.
 
Back
Top Bottom