Kisheria ni watu wangapi wanatakiwa kushiriki uchaguzi mkuu ili uwe halali kisheria?

Kisheria ni watu wangapi wanatakiwa kushiriki uchaguzi mkuu ili uwe halali kisheria?

Unapaswa ujifunze kutofautisha kati ya "legality" na "legitimacy".
Legality ni kutambulika kisheria bila kujali madaraka yamepatikanaje au Sheria kama mbaya au nzuri, Legitimacy ni kukubalika na sehemu kubwa ya jamii, kuwepo kwa haki, uungawana na ustaarabu.

Mfano Serikali ya Makaburu wa South Africa kabla 1994 ilikuwepo na ikawa inatambulika kisheria(legality) lakini haikuwa na uhalali wa kijamii(legitimacy), ilikuwa ni illegitimate government.

Sheria za kutenganisha weusi na Wazungu Marekani zilikuwepo kisheria na watu waliozivunja walifungwa kweli, Sheria zilikuwa na legality ila zillikuwa illegitimate.
Hii imekaa vizr sana. Asante kwa somo
 
Back
Top Bottom