Kisheria, Spika wa Bunge anaweza kuondolewa. Je, Job Ndugai aondolewe?

Kisheria, Spika wa Bunge anaweza kuondolewa. Je, Job Ndugai aondolewe?

1641112277300.jpg
 
Spika akileta maloloso, anaweza kuondoloewa kwa azimio la wabunge.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kifungu 84,7(d)


(d) ikiwa mtu huyo ataondolewa kwenye madaraka ya
Spika kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na
Wabunge amabo idadi yao haipungui theluthi mbili ya
Wabunge wote; au.........

Haya wabunge jipimeni na mumpime Spika.
Anatosha?
Naamini wabunge wengi hawakubaliani na Spika kwa sababu nyingi tuu ,moja ikiwa ni kwamba kwa sasa mama anaitekeleza ahadi kwa Kasi sana huko majimbono.

Kuanzia madarasa, barabara hadi vituo vya afya na maji ,masuala ambayo ni kero kubwa kwa wananchi Vijijini.

Akitokea mtu akawasilisha hoja fasta anaondolewa .Naunga mkono hoja.
 
Wanabodi,

Niliposema Rais wa JMT anaweza Kuondolewa madarakani na Bunge, wengi walibeza kuwa nilikuwa nazungumzia hypothetical situation, yaani kitu ambacho hakipo, nikauliza hakipo vipi wakati kipo kwenye Katiba yetu?, sema haijatokea tukapata rais wa kulazimika Kuondolewa.

Leo ninazungumzia Kuondolewa kwa Spika wa Bunge la JMT. Kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa Spika wa Bunge, basi anageuka mungu mtu, anaweza kufanya lolote na asiguswe!. No!. Nafasi ya Spika ipo kwa mujibu wa Katiba, na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, akikiuka na ikathibitishwa amekiuka, Spika anaondolewa!. Swali ni Jee Spika Mhe. Ndugai amekiuka Katiba, sheria, taratibu na kanuni kustahili Kuondolewa? .
Paskali
Wanabodi, hili ni swali nililo liuliza miaka 5 iliyopita, sikumbuki vizuri nilijibiwaje humu, ila kwa kinachoendelea sasa, hili swali bado liko very valid, jee aondolewe?.
P
 
Paskali; una hoja nzuri sana lakini bado hata kwa hoja hii naweza kusema ni "too hypothetical "! but sir, get me right; Kikatiba uko sahihi, spika anaweza kuondolewa lakini ukirudi upande wa hali halisi na jinsi siasa za Tanzania zilivyogeuka maigizo; mtu mzima yuko tayari kusema haya maziwa ni meusi wakati anayaona kwamba ni meupe! Kinachofanyika hapa kwa sasa ni political expediency, kulindana, party caucus politicking, kutetea maslahi ya kikundi badala ya maslahi mapana ya taifa; kwa mantiki hiyo itakuwa ndoto wabunge wa ccm kwa wingi na umoja wao wakubali na kuipitisha hoja ya kumuondoa spika Ndugai!
Hii ni hoja ya kufikirika tu kwa maana hiyo, though in an ideal scenario; ndio spika anaondosheka vizuri kabisa, lakini sio kwa siasa za Tanzania kwa sasa where the rule of big numbers is the norm rather than the exception instead of LOGIC and broader national interests.
Mkuu MTK , huwezi amini, hii posti yako ya April 10, 2019, mimi ndio naiona leo
Je kwa the current situation, kwa maoni yako, something like bado ni hypothetical situation tuu or this thing can happen?.
Happy New Year
P
 
Wanabodi,

Niliposema Rais wa JMT anaweza Kuondolewa madarakani na Bunge, wengi walibeza kuwa nilikuwa nazungumzia hypothetical situation, yaani kitu ambacho hakipo, nikauliza hakipo vipi wakati kipo kwenye Katiba yetu?, sema haijatokea tukapata rais wa kulazimika Kuondolewa.

Leo ninazungumzia Kuondolewa kwa Spika wa Bunge la JMT. Kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa Spika wa Bunge, basi anageuka mungu mtu, anaweza kufanya lolote na asiguswe!. No!. Nafasi ya Spika ipo kwa mujibu wa Katiba, na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, akikiuka na ikathibitishwa amekiuka, Spika anaondolewa!. Swali ni Jee Spika Mhe. Ndugai amekiuka Katiba, sheria, taratibu na kanuni kustahili Kuondolewa? .

Declaration of interest.
Mimi ni muumini wa Katiba, unauhusisha uendeshaji wa nchi kwa mujibu wa Katiba kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni.

Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kufuatia bandiko hili

Tundu Lissu apinga vikali adhabu ya Mdee na Bulaya,


Tanzania ni nchi inayofuata Katiba kwa kuzingatia misingi ya haki, kuwa "no one is above the law" kumaanisha Katiba ndio the supreme law, hakuna yoyote aliye juu ya Katiba na sheria.

Chini ya Katiba hiyo, tunayo mihimili mitatu, ya Serikali, Bunge na Mahakama ambayo yote inapaswa kuwa huru kwa kutenda bila kuingiliwa na mihimili mingine (independently) lakini wakati huo huo kila mihimili ukiwa na majukumu ya kutenda kwa mujibu wa Katiba, ikitokea mihimili mmoja umekiuka mamlaka yake, then hii mihimili mingine ina jukumu la kuufanyia checks and balance.

Hii inaitwa "the doctrine of separation of powers".

Bunge lina jukumu la kutunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na Serikali inatekeleza sheria.

Serikali inatakiwa kuliwezesha Bunge na Mahakama ikiwemo kulidhibiti Bunge kupitia mamlaka ya rais kuteua mtendaji mkuu wa Bunge ambaye ni katibu wa Bunge.

Serikali inaidhibiti Bunge kwa kuridhia sheria zinazotungwa na Bunge haziwi sheria hadi mkuu wa serikali aridhie, na asiporidhia rais ana mamlaka ya kulivunja Bunge.

Serikali pia inawajibu wa kuihudumia Mahakama kwa kuiwezesha ila pia kulidhibiti kwa kuteua Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Jaji Mkuu lakini haiwezi kumuondoa, ila pia serikali inaidhibiti Mahakama kwa kusaini hati za capital punishment.

Bunge kwa upande wake lina jukumu la kuisimamia Serikali na Mahakama kwanza kwa kuitungia sheria, kupitisha bajeti zao, na kuisimamia matumizi yake.

Serikali inapokosea kwa kukiuka mamlaka yake, inashitakiwa Mahakamani au bungeni, na mkuu wa mihimili huu wa Serikali akienda kinyume cha Katiba, anashitakiwa na Bunge na kufukuzwa kazi kupitia "impeachment process"

Kama serikali inaweza kushitakiwa Mahakamani, Mahakama inashitakiwa Bungeni na Serikalini, Jee Bunge haliwezi kushitakiwa Mahakamani?.

Serikali imewahi kushitakiwa mahakamani mara kibao tuu na ikashindwa. Sina kumbukumbu ya Mahakama kushitakiwa nje ya Mahakama, nakumbuka zile kesi za Mtikila, lakini Bunge la Tanzania halijawahi kushitakiwa mahakamani.

Hii ya Bunge kutokushitakiwa kumemfanya Mkuu wa Mhimili huu Bunge, kujisahau, kujiiunua na kujiona kama mungu mtu hivyo kutaka kuabudiwa, kuigopwa na kunyenyekewa hadi kujiona anaweza kufanya chochote, kusema chochote na kutoa maamuzi yoyote hata yaliyo kinyume cha sheria, taratibu na kanuni na asiguswe!.

Adhabu kwa Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya now goes down to history books za Bunge letu kwa mara ya kwanza kushitakiwa mahakamani if at all kesi itafunguliwa kweli.

Kwa kumbukumbu zangu mtu pekee mwenye kinga ya kisheria ya kutokushitakiwa mahakamani ni Rais wa JMT pekee, hivyo serikali Inashitakika, Mahakama Inashitakika swali ni Jee Bunge nalo pia Linashitakika?!.

Mihimili hii ya dola inaongozwa na binadamu ambao sio malaika na wanaweza kukosea, ikitokea wakuu wa mihimili hii kukosea, sheria imeweka utaratibu wa jinsi ya kumuondoa rais, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge. Swali ni Jee Spika wa Bunge Job Ndugai aondolewe?.

Kwa vile utaratibu wa kumuondoa spika ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kwa vile mimi sio mwanasheria, naomba niwakabidhi kwa mmoja wa wanasheria wetu humu jf,
Mkuu The Learned Brother
Petro E. Mselewa
ili muweze kupata vifungu vya sheria, kanuni na utaratibu was kumuondoa spika .
Spika anaondolewa hivi...


Paskali
Rejea
Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Vurugu za Jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.

Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of Separation of Powers is it Nothing, Just a Myth? ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi? | Page 15 ...
Ndugae must GO! Amefanya bunge kuwa dhaifu sana ( rubber stamp ya serikali).

Pili ni ubaguzi wa vyama na matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa ( C-19).
 
Naamini wabunge wengi hawakubaliani na Spika kwa sababu nyingi tuu ,moja ikiwa ni kwamba kwa sasa mama anaitekeleza ahadi kwa Kasi sana huko majimbono.

Kuanzia madarasa, barabara hadi vituo vya afya na maji ,masuala ambayo ni kero kubwa kwa wananchi Vijijini.

Akitokea mtu akawasilisha hoja fasta anaondolewa .Naunga mkono hoja.
Hiyo hoja ataiwasilisha kwa spika yupi?
 
Wabunge tunampima Raisi na hatoshi , soon tunapiga Kura ya kutokuwa na Imani nae
Ila maisha haya jamani , kweli kwa sasa hivi NDUGAI, ni wakuonekana hivi?kama mtoto yatima wakati kama mwaka mmoja nyuma alikuwa ni wakuogopwa vile?!!yaani yeye na meko ndio walikuwa wanajiona ndio miungu wa nchi hii!!!ukishakuwa una chukiwa na jamii, siku yakikukuta ndio utaona kumbe ..nilikuwa cjui!!na sasa hivi jamaa hana hata watetezi wa maana zaidi yenu nyie MWENDAZAKE MASALIA.
 
Siku hizi hatununui wapiga kura tunanunua Mawakala wao na walinda kura wao!

Bahati yake sana kazaliwa katikati ya nchi…angetokea Mpakani kazi ingemalizwa na Makamishna wa Uhamiaji kama tulivyofanya kwa Kihelehele Jenerali Ulimwengu miaka ile au Marehemu Ally Nabwa ambae ilibidi marehemu Baba Yake avuliwe Uraia akiwa tayari Kaburini kwa miongo kadhaa ili ipatikane sababu ya kudai na mwanae sio Raia

Kuipata hiyo 2/3 siyo jambo la kitoto!
 
Back
Top Bottom