Kishindo cha Awamu ya Tano katika muhula wa pili kiko wapi?

Kishindo cha Awamu ya Tano katika muhula wa pili kiko wapi?

Tulitegemea amsha amsha tulizozizoea tangu JPM aingie madarakani, tumbua tumbua, vamia vamia maofisi ya wizara na ziara za kushutukiza na kutumbua majipu.

Lakini tangu JPM aingie madarakani tunashuhudia ukimya wa ajabu, baraza la mawaziri kimya, hatusikii tumbua tumbua,hatusikii ziara za kushutukiza. Hali kwa wananchi bado ni mbaya sana sio kwamba kero zao zote zimetatuliwa wakati wa awamu ya kwanza ya JPM.

Ukitaka kuamini hili tembelea na fanya tafiti juu ya maisha ya wananchi wa kawaida bado ni mbaya sana. Wengi wanaishi kwa mlo mmoja, uonevu unaofanywa na vyombo vya dola, watumishi wa umma kwa wananchi bado ni tatizo kubwa.

Kishindo cha awamu ya Tano awamu ya pili kiko wapi? Au Ccm mnadhani mmetatua kero zote za wananchi?
Ndio
 
Wapo bussy kujadili ni jinsi gani watalipa madeni ya mikopo kwaajili ya kupambana na Covid-19. Pamoja na kuficha sura zao kwa aibu.

Mikopo yenyewe ya kupambana na Covid-19 kama ifuatayo;

1) € 27 Million - Kutoka kwa EUROPEAN UNION.

2) $ 14.3 Million - Kutoka kwa INTERNATIONAL MONETARY FUNDS (Mwezi June).

3) $ 3.4 Million - Kutoka kwa WORLD BANK (Mwezi September).

4) $ 50.7 Million - Kutoka kwa AFRICAN DEVELOPMENT BANK (Mwezi October).

5) $ 11 Million - Kutoka kwa GLOBAL FUND.
Kumbe ilikuwa mkopo, who msaada?
 
Aibu kubwa sana, leo wamekopa pesa mradi wa umeme malagarasi. Sasa unajenga JNHPP malaragarasi ya nini? Wacha1

Nahisi hii account yako leo wameihack. Tumesema hiyo project ya JNHPP tuna mashaka kama itiasha, ndio maana wanasema mradi wa SG utaisha 2022 lakini wanaweka kijimradi kingine.

Huu wizi wa kura uliofanyika utawekwa hadharani tu hivi karibuni. Na nyie praise team mtapoteana lazima.
 
we hujaona kishindo kimeanza kwa kutoa majina hewa ya ualimu?
Kweli safari hii tumepatikana. Niliposikia tu ajira za waalimu nikajua tu ni uongo. Nilipokuja kupitia ile list hapo nikapata ukweli wote.
 
Wapo bize kutengeneza ishu ya hawa wabunge 'Covid 19'. Na diliishabuma Chadema wameteketeza Covid 19!
Tumasubiri Ndugai awarudiahe bungeni kama wagombea binafsi au awasajili rasmi kwake.
 
Kishindo cha nini na uchaguzi umeshaisha dola imeshakamatwa? Huu ni muda wa kula sasa, kishlndo subiri awamu ya sita nitapogombea.
 
Tulitegemea amsha amsha tulizozizoea tangu JPM aingie madarakani, tumbua tumbua, vamia vamia maofisi ya wizara na ziara za kushutukiza na kutumbua majipu.

Lakini tangu JPM aingie madarakani tunashuhudia ukimya wa ajabu, baraza la mawaziri kimya, hatusikii tumbua tumbua,hatusikii ziara za kushutukiza. Hali kwa wananchi bado ni mbaya sana sio kwamba kero zao zote zimetatuliwa wakati wa awamu ya kwanza ya JPM.

Ukitaka kuamini hili tembelea na fanya tafiti juu ya maisha ya wananchi wa kawaida bado ni mbaya sana. Wengi wanaishi kwa mlo mmoja, uonevu unaofanywa na vyombo vya dola, watumishi wa umma kwa wananchi bado ni tatizo kubwa.

Kishindo cha awamu ya Tano awamu ya pili kiko wapi? Au Ccm mnadhani mmetatua kero zote za wananchi?
Aibu ya kukaa Ikulu bila kura halali za Wananchi, He knows He is a thief...hana legitimacy ya kumsumbua mtu mwingine yeyote
 
Nahisi hii account yako leo wameihack. Tumesema hiyo project ya JNHPP tuna mashaka kama itiasha, ndio maana wanasema mradi wa SG utaisha 2022 lakini wanaweka kijimradi kingine.

Huu wizi wa kura uliofanyika utawekwa hadharani tu hivi karibuni. Na nyie praise team mtapoteana lazima.
Bro upo sawa? Mimi sio praise team ni mtu ambae nahoji mambo ya msingi. Kama JNHPP inaweza kuzalisha Mw 2115 kwa akili ya kawaida hakuna ulazima wa kukopa pesa kwa ajili ya miradi midogo midogo. Haya ni matumizi mabaya ya pesa za umma.
 
Back
Top Bottom