Kishindo cha Awamu ya Tano katika muhula wa pili kiko wapi?

Kishindo cha Awamu ya Tano katika muhula wa pili kiko wapi?

Tulitegemea amsha amsha tulizozizoea tangu JPM aingie madarakani, tumbua tumbua, vamia vamia maofisi ya wizara na ziara za kushutukiza na kutumbua majipu.

Lakini tangu JPM aingie madarakani tunashuhudia ukimya wa ajabu, baraza la mawaziri kimya, hatusikii tumbua tumbua,hatusikii ziara za kushutukiza. Hali kwa wananchi bado ni mbaya sana sio kwamba kero zao zote zimetatuliwa wakati wa awamu ya kwanza ya JPM.

Ukitaka kuamini hili tembelea na fanya tafiti juu ya maisha ya wananchi wa kawaida bado ni mbaya sana. Wengi wanaishi kwa mlo mmoja, uonevu unaofanywa na vyombo vya dola, watumishi wa umma kwa wananchi bado ni tatizo kubwa.

Kishindo cha awamu ya Tano awamu ya pili kiko wapi? Au Ccm mnadhani mmetatua kero zote za wananchi?
Mzee baba alikuwa anauguza moyo wake
 
Back
Top Bottom