Kishindo cha DP WORLD: Tozo na Kodi mbalimbali kufutwa au kupunguzwa mwaka wa fedha 2023/2024. Tutarajie mazuri zaidi miaka ijayo ya fedha

Kishindo cha DP WORLD: Tozo na Kodi mbalimbali kufutwa au kupunguzwa mwaka wa fedha 2023/2024. Tutarajie mazuri zaidi miaka ijayo ya fedha

Kama
  • Usijiondoe ufahanu kuwa wameongeza gharama kwenye mafuta na cement! Wajinga ni wengi!
  • Bandari mpaka za kwenye viziwa zimetekwa hivyo, ni marufuku kukuta mtu hata anaota jua bila idhini ya DP.
  • Akina Mkwawa wangefufuka leo wangeanzisha farangati za kufa mtu kuliko hata walivyofanya kwa Wajerumani
Kama umechunguza vizuri bidhaa nyingi ambazo zinachafua mazingira sana zimewekewa tozo na sababu ni kulinda mazingira ambayo ni ajenda ya dunia
 
Kwenye mapendekezo ya bajeti Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 baadhi ya tozo kama ile tozo ya kwenye miamala ambayo ni kilio Cha wanyonge wengi na Ile Kodi ya 'store' iliyopelekea mgomo Kariakoo zitaondolewa kabisa. Ukiachana na hizo Kodi, tozo na ushuru mbalimbali wa bidhaa zitapungua kabisa.

Kodi ni muhimu sana na Kwa vyovyote zisingeweza kuondolewa ikiwa mbadala wake haujajulikana ila Kwa kuwa mbadala umepatikana basi Serikali sikivu ya mama Samia imetupatia unafuu.

Tusipepese macho, mbadala wa tozo hizo ni matokeo na faida za uwekezaji zitakazopatikan katika bandari Kwa ushirikiano na DP WORLD. Makubaliano na DP WORLD yatakuja na fursa lukuki ikiwepo kuongezeka Kwa mchango wa mapato yanayochangiwa na bandari mpaka 67% kutoka 37% ya Sasa.

Hizi ni faida za mwaka wa kwanza tu, Sasa tufikirie mbali Zaidi faida zitakazokuwepo mwaka wa fedha 2024/2025-2025/2050. Naamini zitakuwa za kufurahisha.

Wanaopinga makubaliano haya watuambie kama hili sio jambo jema Kwa wananchi?

Je, Kuna mwananchi wa kawaida anayepinga makubaliano ikiwa yanampa faida za Moja Kwa Moja kama hizi?

Rai yangu, tumwache mama afanye kazi ,mipango na mikakati yake Kwa Taifa ni mikubwa Zaidi ya tunavyowaza au kufikiria.
yaani wewe mkiwekwa pamoja na mbuzi, mbuzi itaonekana ina akili kuliko wewe.
 
Tigo na Airtel hawataki koundoa tozo wakati vodacom washaziondoa hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom