Kishindo Mkutano Mkuu CHADEMA ; Mabalozi na Taasisi za Kimataifa wathibitisha kushiriki!

Itakuwa historia.Ndivyo tunavyoweza kusema kwani mkutano mkuu wa CHADEMA Desemba 18 utahudhuriwa na taasisi na mashirika makubwa ya ndani na nje ya nchi pengine kwa mara ya kwanza katika historia ya mikutano mikuu ya vyama.

Chanzo kimoja cha Taarifa kutoka ndani ya chama hicho chenye wanachama milioni 6 ni kwamba tayari mabalozi 14 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wamethibitisha kushiriki mkutano huo wakiwemo mabalozi wa mataifa makubwa duniani.

Pia inadaiwa Taasisi na mashirika mbalimbali zaidi ya 19 tayari yamethibitisha kushiriki katika mkutano mkuu huo ambao umekuwa gumzo ndani na nje ya nchi kwa Takribani mwezi mmoja sasa.Mojawapo ya Taasisi kubwa duniani inayotarajiwa kutuma wawakilishi wake ni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International

Pia wanazuoni,viongozi wa dini,wafanyabiashara wakubwa,vyama vya siasa na watu kadhaa mashuhuri wamepewa mialiko kuhudhuria mkutano mkuu huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe anatarajiwa kulihutubia Taifa kupitia mkutano mkuu katika hotuba inayotarajiwa kuchukua saa mbili.Katika hotuba hiyo Mbowe anatarajiwa kuhitimisha utawala wake wa miaka mitano na kutoa mwelekeo wa chama hicho kwa miaka ijayo.

Katika kuelekea mkutano mkuu wa Desemba 18 ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mlimani City ulipo ukumbi utakaotumika huku askari waliovalia kiraia na wenye sare wakionekana kurandaranda wakiwemo vijana wa ulinzi wa chama hicho Red Brigade.
Hakuna Vijana wa Ulinzi wanaoitwa Red Brigade katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo. (CHADEMA)
 
Tehetehe eti kishindo
Waalike waje kuwaaga,mwakani chama kikuu cha upinzani ni ACT.Sio mimi ni hesabu tu

Acha ACT, hata TLP likiwa chama kikuu cha upinzani hatujali,maana hatuna shaka na kukubalika kwa cdm.
 
Sorry Kawe alumni, HV Msomi Mbunge wa Ndanda ndg yetu Mwambe alihutubia ile tar 10 km ulivyotangaza? Nilikuwa shambani with data! Tell me man!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani Mwambe ameamua kufuata taratibu za chama.Anatakiwa asubiri uteuzi ndani ya chama siku ya Jumanne
 
Hahahaaaa......hahahaaaaa......hahahaaaaa.........!

Ruzuku ya CCM imeongezeka kutoka sh 12 bilioni mwaka 2015/16 hadi sh 13 bilioni mwaka 2018/19.....Unajua ni kwanini?

Maendeleo hayana vyama!
Na CDM kimeongeza wanachama kutoka milioni 4 hadi 6 kwa kipindi cha miaka minne
 
Itakuwa historia.Ndivyo tunavyoweza kusema kwani mkutano mkuu wa CHADEMA Desemba 18 utahudhuriwa na taasisi na mashirika makubwa ya ndani na nje ya nchi pengine kwa mara ya kwanza katika historia ya mikutano mikuu ya vyama.

Chanzo kimoja cha Taarifa kutoka ndani ya chama hicho chenye wanachama milioni 6 ni kwamba tayari mabalozi 14 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wamethibitisha kushiriki mkutano huo wakiwemo mabalozi wa mataifa makubwa duniani.

Pia inadaiwa Taasisi na mashirika mbalimbali zaidi ya 19 tayari yamethibitisha kushiriki katika mkutano mkuu huo ambao umekuwa gumzo ndani na nje ya nchi kwa Takribani mwezi mmoja sasa.Mojawapo ya Taasisi kubwa duniani inayotarajiwa kutuma wawakilishi wake ni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International

Pia wanazuoni,viongozi wa dini,wafanyabiashara wakubwa,vyama vya siasa na watu kadhaa mashuhuri wamepewa mialiko kuhudhuria mkutano mkuu huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe anatarajiwa kulihutubia Taifa kupitia mkutano mkuu katika hotuba inayotarajiwa kuchukua saa mbili.Katika hotuba hiyo Mbowe anatarajiwa kuhitimisha utawala wake wa miaka mitano na kutoa mwelekeo wa chama hicho kwa miaka ijayo.

Katika kuelekea mkutano mkuu wa Desemba 18 ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mlimani City ulipo ukumbi utakaotumika huku askari waliovalia kiraia na wenye sare wakionekana kurandaranda wakiwemo vijana wa ulinzi wa chama hicho Red Brigade.
Ndio maana chadema hii itaendelea kuwa chama cha upinzani dhidi ya chama chenye hatamu.
 
Back
Top Bottom