Kishindo Mkutano Mkuu CHADEMA ; Mabalozi na Taasisi za Kimataifa wathibitisha kushiriki!

Kishindo Mkutano Mkuu CHADEMA ; Mabalozi na Taasisi za Kimataifa wathibitisha kushiriki!

Nimetoka muda huu Mlimani City....hali ya kawaida sana usiwadanganye wa mikoani.

Ataomba tena MARIDHIANO Kama alivyofanya Mwanza.

Mwenyekiti hana namna zaidi ya Kusarenda
Pole sana
 
Kwanini mnafanyia mkutano maeneo ya kifahari ili hali wapiga kura wenu ni maskini

Inaboa sana kwa kweli
Ni kama ccm walivyojenga ukumbi wa kifahari pale Dodoma ilihali nchi bado ni maskini na wananchi wake pia hasa wale wa mko ulioko jengwa huo ukumbi.
 
Kwan mkuu umetumia kigezo gan mpaka ukasema kuwa mlimani city ni eneo la kifahari?

Afu kumbuka kuwa unachokiona wewe ni cha kifahari, wenzako wanaweza kukiona ni duni!

Kwanini mnafanyia mkutano maeneo ya kifahari ili hali wapiga kura wenu ni maskini

Inaboa sana kwa kweli
 
Ni kama ccm walivyojenga ukumbi wa kifahari pale Dodoma ilihali nchi bado ni maskini na wananchi wake pia hasa wale wa mko ulioko jengwa huo ukumbi.

..wanapokea bil 13 kama ruzuku.

..halafu unakuta majimbo wanayoyaongoza shule zina upungufu wa madarasa, na hazina matundu ya vyoo.
 
Hahaha mkikutana nyumbu kwa nyumbu huwa mnajifariji sana

Naona unaniita nyumbu lakini nikikupa lugha chafu unaanza kulia unakosewa adabu. Si unajua mimi lugha chafu wala sio za kutafuta?
 
Itakuwa historia.Ndivyo tunavyoweza kusema kwani mkutano mkuu wa CHADEMA Desemba 18 utahudhuriwa na taasisi na mashirika makubwa ya ndani na nje ya nchi pengine kwa mara ya kwanza katika historia ya mikutano mikuu ya vyama.

Chanzo kimoja cha Taarifa kutoka ndani ya chama hicho chenye wanachama milioni 6 ni kwamba tayari mabalozi 14 wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wamethibitisha kushiriki mkutano huo wakiwemo mabalozi wa mataifa makubwa duniani.

Pia inadaiwa Taasisi na mashirika mbalimbali zaidi ya 19 tayari yamethibitisha kushiriki katika mkutano mkuu huo ambao umekuwa gumzo ndani na nje ya nchi kwa Takribani mwezi mmoja sasa.Mojawapo ya Taasisi kubwa duniani inayotarajiwa kutuma wawakilishi wake ni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International

Pia wanazuoni,viongozi wa dini,wafanyabiashara wakubwa,vyama vya siasa na watu kadhaa mashuhuri wamepewa mialiko kuhudhuria mkutano mkuu huo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe anatarajiwa kulihutubia Taifa kupitia mkutano mkuu katika hotuba inayotarajiwa kuchukua saa mbili.Katika hotuba hiyo Mbowe anatarajiwa kuhitimisha utawala wake wa miaka mitano na kutoa mwelekeo wa chama hicho kwa miaka ijayo.

Katika kuelekea mkutano mkuu wa Desemba 18 ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mlimani City ulipo ukumbi utakaotumika huku askari waliovalia kiraia na wenye sare wakionekana kurandaranda wakiwemo vijana wa ulinzi wa chama hicho Red Brigade.

Kabla ya Mkutano Mkuu Jumatano Desemba 18 siku ya Jumatatu Kamati Kuu ya Chama hicho itakutana hapo hapo Mlimani City huku Baraza Kuu likikutana siku ya Jumanne ikiwa ni siku moja kabla ya Mkutano Mkuu.Vikao hivi vya Kamati Kuu na Baraza kuu vitapitisha majina ya wagombea nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Binafsi nimekusamehe kwani hujui maana ya kulihutubia taifa...Ni mtu mmoja tu anayeweza kulihutubia taifa naye ni Rais wa nchi na ambaye ni Amiri Jeshi mkuu
 
Back
Top Bottom