Kisiasa Bi Sara alifanya kosa kubwa la kimkakati na aliponzwa na Moyo wake huruma

Kisiasa Bi Sara alifanya kosa kubwa la kimkakati na aliponzwa na Moyo wake huruma

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni

Ni hoja ya Kisiasa ukiamua kuijadili hivyo
Ni hoja ya kidini ukiamua kuijadili hivyo
Ni hoja mchanganyiko pia ukiamua iwe hivyo


Ni mada inayomuhumu Bi Sara mamake na Isaka

Kwangu Mimi naileta kama hoja ya Kisiasa

Uamuzi wa Sara uliompatia haki Mumewe ya Kufanya kile alichofanya ulikuwa ni kosa kubwa sana la kihistoria

Sara hakutakiwa kuwa na haraka bali subira
Sara alikuwa na moyo wa huruma mno

Yaliyotokea yametokea na majuto Ni mjukuu
 
Sara Unayemzungumzia ni Yupi? Yule jirani Yetu huku Kwa Mtogole...!
Poa kwanza unapotaka kuwakilisha Mada..!
 
Aliasisi kuliwa kwa wajakazi (beki tatu) na kazi hiyo tunaiendeleza kwa uadilifu mkubwa, nami nasema kazi iendelee.
 
Mkuu umeeleza kana kwamba kila mtu yupo ndani ya akili yako.
Hujaeleza ni kosa lipi alilolifanya Sara.
1. Je! Ni kuhusu kumkubalia mumewe atambulishe kama dada katka nchi ya kigeni?
2. Je! Ni kutilia mashaka kuhusu ya kauli ya malaika kuwa atajifungua mtoto ijapokuwa alikua ni bibi kizee?
3. Je! Ni kuruhusu mumewe alale na mjakazi wake?
4. Je! Alipopata wivu kwa bi mdogo na kisha kushinikiza mumewe amfukuze Ishmaili na mama yake Hajiri?
5. Au je! Kuna kosa lingine lolote lile alilofanya lenye kuweza kubeba dhana za kisiasa na kijamii ambalo limetajwa katika maandiko matakatifu?

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Aliasisi kuliwa kwa wajakazi (beki tatu) na kazi hiyo tunaiendeleza kwa uadilifu mkubwa, nami nasema kazi iendelee.
... huyo beki tatu wako uhakikishe unaomba ruhusa kwa mkeo, unamzalisha, na unamwandalia yeye na mwanaye maisha mazuri na sio kuwatelekeza. Hicho ndicho alichofanya Mzee Ibrahim.
 
Simjui huyo sara, wala sijui alichofanya! Sijasoma vitabu vya dini.

Nikijaribu kulichambua kisiasa km mleta mada, nahisi hapa kuna harufu ya kumsema mama yetu (raia namba 1) kama ambavyo uzushi mwingi uliwahi kusambazwa na wahuni kuhusu yeye na jk........hapa huyu anapita humohumo kwenye huo uzushi. Kwamba wapo karibu na anafuata ushauri wake (jk). Hilo ndilo nilionalo katika mada hii.
 
Sara hakumuonea Huruma Hajiri, Ila alichokifanya ilikuwa ni kumdhihaki Ibrahim Kama ndiye mwenye Tatizo na sio yeye(mwanamke) hivyo kumwambia Ibrahim amuingilie Hajiri ni kumuumbua kuwa yeye ndiye mwenye Tatizo.

Hivyo baada ya Hajiri kupata mimba ikadhihirika na kuthibitika wazi kuwa mwenye Tatizo ni Yeye(Sara) ndio hapo Akawa Duni Kwa Mjakazi wake, Hajiri kuwa yeye ndiye mgumba na sio Mumewe Ibrahim.

Ili uone Kama Hakuwa na huruma Kama ulivyoiita, angalia baada ya yeye kupata mimba baada ya miaka Saba iliyofuata anamfukuza Hajiri Kwa kisingizio cha Urithi ilhali kuna manabii kibao walioa mke zaidi ya mmoja na hawakufukuza wake zao
 
Back
Top Bottom