Kisingizio cha kutuletea maendeleo isiwe sababu ya kutunyima katiba itayoleta haki kwenye Taifa letu

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Hivi kwa akili ya kawaida tu kuna tatizo gani kufanya implementation ya rasimu ya katiba ya Jaji Warioba kisha taifa likawa na katika ambayo itaondoa manug'uniko katika taifa.

Kila kitu kipo tayari kimeshapikwa ni suala la kupakua tu na kuweka mezani. Rasimu ipo na ilishatoa mapendekezo mazuri sana ili tuwe na katiba ambayo itamnufaisha kila Mtanzania.

Hili mnalotuambia kuwa mnakomaa kutupatia maendeleo kwanza ili mkikamilisha ndio mje mtupatie Katiba mbona haliingii akilini? Kwamba kama msipokamilisha kutupatia maendeleo na katiba mpya hatupati?

Kuna ugumu gani kukamilisha ile rasimu ya katiba ya Warioba ili tupate katiba mpya huku mkitupatia maendeleo? Nini kitakwamisha?

Maadam tunataka taifa lenye kutoa haki basi hatuna budi kuwa na katiba kama ilivyopendekezwa na tume ya Warioba. Maana bila ya kuwa na katiba kama iliyopendekezwa na Warioba basi tunajidanganya kusema Tanzania kuna haki.
 
Nafarijika nikiona watu kama wewe mliokuwa mmekunywa maji ya bendera ya kijani mnaandika vitu kama hivi.

Pamoja sana.
 
Back
Top Bottom