Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Basi la Mwendokasi likiwa linatoka Kivukoni limeacha njia na kuparamia maduka na miundombinu mingine pembezoni mwa barabara ya Morogoro kwenye makutano ya Jamhuri St.
Eneo hilo ni viambaza vya maduka, njia ya waenda kwa miguu na limekuwa linatumika na watu wasio na makazi kulala
Ukiangalia picha kwa umakini utaona baadhi ya virago vya kulalia ombaomba. Tuombe Mungu pasiwepo na madhara ya uhai.
====
Basi la Mwendokasi leo February 22, 2023 limepata ajali eneo la makutano ya Jamhuri na Morogoro baada ya kugongana na gari ndogo kisha kuparamia ukuta wa duka likijaribu kulikwepa. Imeripotiwa kutokea majeruhi kadhaa.
------
Baada ya kuibuka sintofahamu ya mwanaume aliyeonekana akijaribu kulikwepa gari la mwendokasi wakati wa ajali (tazama video au picha hapo juu) kuwa amepona au amefariki dunia, Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia kitengo cha mifupa MOI walitoa taarifa kuwa mwanaume huyo hakufariki ila alipata majereha makubwa na kulazwa chumba cha wagonjwa mahututi.
Zaidi soma: MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU