Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Hii mitaa hua ni Mungu tu anaepusha ajali,ni hatari sana,nyumba ziko karibu sana na barabara,jioni hasa kuanzia saa moja kuna ombaomba wegi sana,tena vingine ni vitoto vidogo vinazurura ovyo,sasa kibaya mabasi ya mwendo kasi kwakua ni barabara yao mwendo wanotembea kwakweli si rafiki kabisa,yaani kama una ma stress yako ya familia usipende sana kukatiza hayo maeneo...
Pia jioni watu hutumia viambaza hivyo kwa dinning out. Wazee wa mutton, tandoor, sekela, sechwan rice na indian recipes hujazana maeneo hayo kujinafasi
 
Wanaolala nje mara nyingi huwahi kuamka,labda kama alienda kugonga waenda kwa miguu.
20230222_073050.jpg

Hii picha ni ya leo pale mbele ya jengo la UVCCM Lumumba.

Concept ya kuwahi kuamka ni nadharia.

Na huwa wanachelewa sana kulala
 
usimamizi na uangalizi kwenye miradi hii ya umma ni tatizo sugu.

WATAFUTWE WAHINDI AU WACHINA KUENDESHA HIYO MIRADI.

SISI TUBAKI NA KUHAKIKISHA CCM INATAWALA MILELE

Serikali wameshindwa kuendesha miradi yao ila angalia wanavyowasumbua wenye miradi binafsi:

LATRA hili la ving'amuzi ni uonevu uliopitiliza

Unaweza fikiria ni wahalifu kumbe ni wahanga wa wanaolazimisha kula kwa urefu wa kamba zao.
 
Basi la Mwendokasi likiwa linatoka Kivukoni limeacha njia na kuparamia maduka na miundombinu mingine pembezoni mwa barabara ya Morogoro kwenye makutano ya Jamhuri St.

Eneo hilo ni viambaza vya maduka, njia ya waenda kwa miguu na limekuwa linatumika na watu wasio na makazi kulala

Baadhi ya mashuhuda wanatuhumu kuwa dereva alikuwa amelewa.

Ukiangalia picha kwa umakini utaona baadhi ya virago vya kulalia ombaomba. Tuombe Mungu pasiwepo na madhara ya uhai
View attachment 2525759View attachment 2525762View attachment 2525764
Serikali ipige marufuku mabasi kusafiri asubuhi.
 
Back
Top Bottom