Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Ajali ambayo chanzo chake ni pombe inatafakarisha sana
Inafakarisha zaidi kwa sababu;
amelewa saa Moja asubuhi,
Nani alimkabidhi funguo akiwa kwenye hali hiyo, dereva anayeendesha abiria zaidi ya 75?,
Nini Utaratibu wa DART kuhusu kudhibiti ulevi na mienendo hatarishi kwa madereva wao?
 
Basi la Mwendokasi likiwa linatoka Kivukoni limeacha njia na kuparamia maduka na miundombinu mingine pembezoni mwa barabara ya Morogoro kwenye makutano ya Jamhuri St.

Eneo hilo ni viambaza vya maduka, njia ya waenda kwa miguu na limekuwa linatumika na watu wasio na makazi kulala

Baadhi ya mashuhuda wanatuhumu kuwa dereva alikuwa amelewa.

Ukiangalia picha kwa umakini utaona baadhi ya virago vya kulalia ombaomba. Tuombe Mungu pasiwepo na madhara ya uhai
View attachment 2525759View attachment 2525762View attachment 2525764
Halafu nasikia kumbe 85% ya Madereva ni Wajeda na Jana Wajeda wote wamepokea Mishahara yao hivyo yawezekana Usiku aliutwika sana na kaamka nazo hivyo bado kuwa na Usingizi na kufanya hiki alichokifanya.
 
Basi la Mwendokasi likiwa linatoka Kivukoni limeacha njia na kuparamia maduka na miundombinu mingine pembezoni mwa barabara ya Morogoro kwenye makutano ya Jamhuri St.

Eneo hilo ni viambaza vya maduka, njia ya waenda kwa miguu na limekuwa linatumika na watu wasio na makazi kulala

Baadhi ya mashuhuda wanatuhumu kuwa dereva alikuwa amelewa.

Ukiangalia picha kwa umakini utaona baadhi ya virago vya kulalia ombaomba. Tuombe Mungu pasiwepo na madhara ya uhai
View attachment 2525759View attachment 2525762View attachment 2525764
Ukute hakulewa bali ni kolo.
 
Laana ya mwendazake kwa wanaojisafisha kwa kutokuwepo kwake waendelee kupata ugali wa uchawa huku madudu yakiendelea kukithiri. Kama angekuwepo huyo bwana dereva mnadhani angethubutu kunywa kilauli na kuendesha hicho chombo.

Ifike mahali tuweke chuki, ubishi na ushamba pembeni tukubali kipindi chake nidhamu ya kazi na uendeshaji shughuli za nchi ilikuwa kwenye kiwango chake! Sasa hivi kujiamini kwa kipumbavu kumekithiri na madudu yamerudi kwa kasi ya 5.5G+ LTE

WENYE AKILI WATANIELEWA... VICHWA MCHUNGWA WATANIVURUMISHIA MITUSI NA MAJIBU YA KEBEHI. 😊👍🏾
 
Nimekuwa nikifuatilia madereva wanaosababisha ajali, hasa za usafiri wa uma, nimegundua kuwa wote ni wanaume. Wanawake wapo makini sana wawapo kazini, huwezi kukuta mwanamke anakunywa pombe na kuendesha. Ningependekeza madereva wa usafiri wa uma wawe wanawake
 
Kuna wanawake wangapi kulinganisha na wanaume kwenye hii fani ya usafiri wa umma?
 
Nimekuwa nikifuatilia madereva wanaosababisha ajali, hasa za usafiri wa uma, nimegundua kuwa wote ni wanaume. Wanawake wapo makini sana wawapo kazini, huwezi kukuta mwanamke anakunywa pombe na kuendesha. Ningependekeza madereva wa usafiri wa uma wawe wanawake
Sio usafiri wa UMMA tu... hata usafiri binafsi. Wanawake wapo makini labda kwa sababu ni waoga na ni watunzaji wa mali. Wana madudu yao mengine ila katika hili wanastahili pongezi na nafkiri fursa ya ajira kwa upande wa usafiri wa UMMA wapewe wanawake tu. Sisi tubaki na upumbavu wetu.

Na wimbi la jobless kwa upande wa ME husababishwa na wapumbavu wachache wa aina ya huyo jamaa. Inapelekea kuponza wenzake wengine.

Wazo lako ni zuri sana kiongozi. Ni vyema wahusika wakaliona na kulipeleka.
 
Back
Top Bottom