Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Kisutu: Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road

Angalieni video hii ya chanzo cha ajali hapo dereva wa mwendokasi hana makosa aisee
Kwenye junction yoyote ambayo ni "blind" Yaani isiyokupa nafasi ya kuona kuwa kuna magari mengine yanatoka pande zinazokatiza na spidi zao, ni lazima uchukue tahadhari kwa kupunguza mwendo. Yule dereva wa mwendokasi hakuchukua hiyo tahadhari bado akawa na spidi ile ile ambayo haikupi nafasi ya kusimama ghafla bila kusababisha ajali.

Lazima hawa madereva wa mwendokasi wapewe utaratibu mpya wa spidi ya kuendesha mabasi yao kuanzia pale DIT mpaka Kivukoni.
 
Huwa tunaangalia percentages, katika hao wachache unaowajua, wangapi wamesababisha ajali, tafuta percentage yake; halafu uje kwa wanaume uone wangapi wamesababisha ajali, na utafute percentage yao. Mwishoni linganisha percentages hizi mbili; yaani percentage ya wanawake na ile ya wanaume.
Hii ndio moja ya faida ya kufahamu Hisabati.
 
Watu wapuuzi sana humu yaani wamesikia habari washajitungia chanzo kilikuwa Nini, kumbe mwendokasi hana kosa lolote lile. Hadi wanasingizia dereva alilewa
 
Huyu sheikh hapa aliyekuwa akienda pembeni hawezi kupona, halafu kuna huyu boya wa gari dogo anaingia barabarani kichwa kichwa bila hata kuchungulia. Mwendokasi haikuwa hata kwenye kasi. Huyu jamaa mwenye jinsi ndio aliyekuwa na reaction/muitikio unaotakiwa kwenye matukio kama haya.
 
Kwenye junction yoyote ambayo ni "blind" Yaani isiyokupa nafasi ya kuona kuwa kuna magari mengine yanatoka pande zinazokatiza na spidi zao, ni lazima uchukue tahadhari kwa kupunguza mwendo. Yule dereva wa mwendokasi hakuchukua hiyo tahadhari bado akawa na spidi ile ile ambayo haikupi nafasi ya kusimama ghafla bila kusababisha ajali.

Lazima hawa madereva wa mwendokasi wapewe utaratibu mpya wa spidi ya kuendesha mabasi yao kuanzia pale DIT mpaka Kivukoni.
HILO NALO KWELI MKUU
 
Wawaambie hao madereva wao wakiwa wanatoka ferry hadi DIT au Gerezani Mpaka Fire(Kimara/Ubungo BRT) au Muhimbili(BRT) wawe na speed ya kawaida then wakishavuka DIT/FIre hapo ndipo wafungua Turbo kama wanaenda Kimara/Ubungo/Mbezi.
Kuna umuhimu gani wa kuwa mwendokasi Kama unataka litembee taratibu ?
 
Kwenye eneo la ajali huwa watu wengi wanasema la kwao.

Kinachostua ni namna hiyo ajali ilivyotokea ambapo gari imehama upande kabisa na kuharibu miundombinu kabisa
Si kulikuwa na gari nyingine?
 
Kuna umuhimu gani wa kuwa mwendokasi Kama unataka litembee taratibu ?
"Mwendokasi" ni jina tu wala sio ruhusa ya kuendesha kwa spidi kama formula one. Kwa kifupi hiyo BRT yaani "Bus Rapid Transit" ni "njia ya haraka ya basi" . Haina maana basi litakimbizwa kama mashindano ya magari bali basi halitapoteza muda kokote pale kwa sababu ya foleni kama daladala. Ni sawa na wewe utumie gari yako binafsi kupita BRT, utawahi wewe kufika na kuwaacha wengine kwenye foleni.
 
Wakipewa Training ya kutosha na ya muda mrefu naamini wataweza. Usiwadhoofishe kiasi hicho afsa 😊
Hata Rais mlisema hataweza.. mbona anachochora tu?! Na madudu hata wanaume wenzetu walifanya yaleyale tu yanayofanana
Teua tengeu ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wakuu wa taasisi za umma wewe ungeshindwa!? Kusafiri huku na huko duniani, wewe ingekushinda hiyo!? Kutoa toa hotuba za nendeni mkaliangalie na hilo, nalo lingekushinda!?
 
Kuna umuhimu gani wa kuwa mwendokasi Kama unataka litembee taratibu ?
mkuu unajua maana ya bus rapid transit, haimaanishi kwamba gari liwe na mwendo wa kasi inamaanisha gari inawai kufika bila vikwazo vyovyote barabarani kama foleni nk na yale magali ukizidisha spid yanapiga alam kama umeishawai kupanda
 
Hapo ni bus sijui zingekuwa ni trams ingekuwaje
 
Back
Top Bottom