Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Mi huwa najiuliza hivi Hawa polisi,wanaoendesha hizi kesi za hovyo kwa kufungua mashitaka yasio ya maana,huwa wanapataje usingizi usiku.
 
KKw
Kwa uwezo wangu mdogo Maza amepotea njia ndani ya chama chake,ndani ya wananchi wake na nje ya nchi.
 
Hii nchi bhana...aliyeturogaa sijui alizikwa wapi
 
Jaribuni mkuu tuwaone
Hivi wewe kwa akili yako ya kawaida kuna jeshi lolote katika dunia hii liliwahi kushinda nguvu ya umma pale walipoamua kufanya yao?

Kama hiyo nchi ipo nitajie. Sema watu bado hawajaamua tu ila huwa inaanza watu wachache then wanaungana mwisho wa siku viongozi wakuu wanatoroka wakiwa wamevaa baibui tena wanaume.

Nasema hivi acha kabisa kubeza nguvu ya umma usije ukafanya watu kuanza kuchukia wakaanza machafuko ukajuta.

Walikuwepo madikteta walioogopwa sana lakini waliondolewa madarakani na wananchi wasio na bunduki huku wao wakiwa na mabunduki na vifaru.
 
Hivi ni wewe!!? Au naota!! Hahahahahaha....!!
 
Kumbe unajua vizuri pale umma unapochafukwa hakutakuwa na utulivu tena.

Huu uonevu ndio unaowaamsha hata waoga kuvaa roho za kikatili nakubadilika pasipo watawala kuamini.
 
Samia ni rais wa miaka minne tu , tena mpaka Mungu apende
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…