Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

🤣🤣🤣

Gaidi nakusubiri utulize jazba za kutaka kujilipua ili tuendelee na mjadala....

Umesikia bwana gaidi ?!!

#NchiKwanza
#JMTMilele
Magaidi yote yapo ccm

E7IZJOUWUAA0OoX.jpeg
 
Mi huwa najiuliza hivi Hawa polisi,wanaoendesha hizi kesi za hovyo kwa kufungua mashitaka yasio ya maana,huwa wanapataje usingizi usiku.
 
KKw
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kusomewa mashtaka mawili likiwemo la Ugaidi.

Mbowe amefikishwa katika Mahakama hiyo leo July 26, 2021 na kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Tulimanjwa Majigo amesema kuwa Mbowe anaunganishwa na Washtakiwa wengine watatu waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka mengine yote ya ugaidi wanayodaiwa kuyatenda mwaka 2020.

Katika kosa la kwanza, Mbowe anadaiwa kula njama ya kutenda kosa hilo kati ya Mei na Agosti 2020 akiwa katika Hoteli ya Aishi Mkoani Kilimanjaro, kosa la pili la Mbowe ni kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi kinyume cha sheria ya ugaidi kati ya tarehe hizo tajwa.

Baada ya kusomewa maelezo Mbowe hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka.

Kesi imeahirishwa hadi Agosti 5, 2021 na upelelezi umekamilika ambapo zinasubiriwa nyaraka ili ihamishiwe Mahakama
Kwa uwezo wangu mdogo Maza amepotea njia ndani ya chama chake,ndani ya wananchi wake na nje ya nchi.
 
Hii nchi bhana...aliyeturogaa sijui alizikwa wapi
 
Jaribuni mkuu tuwaone
Hivi wewe kwa akili yako ya kawaida kuna jeshi lolote katika dunia hii liliwahi kushinda nguvu ya umma pale walipoamua kufanya yao?

Kama hiyo nchi ipo nitajie. Sema watu bado hawajaamua tu ila huwa inaanza watu wachache then wanaungana mwisho wa siku viongozi wakuu wanatoroka wakiwa wamevaa baibui tena wanaume.

Nasema hivi acha kabisa kubeza nguvu ya umma usije ukafanya watu kuanza kuchukia wakaanza machafuko ukajuta.

Walikuwepo madikteta walioogopwa sana lakini waliondolewa madarakani na wananchi wasio na bunduki huku wao wakiwa na mabunduki na vifaru.
 
Mbona mnashangaa sana Mbowe kushatakiwa? Hakuna mtu mwenye crime history ndefu kama Mbowe ila mfumo ulikuwa unammezea tu. Miaka ya 1985- 1990s alikuwa ni drug trafficker. Kuanzia 1990 amefanya biashara kwenye nyumba ya NHC kwa kutapeli mpaka 2016 Magufuli alipovunja Bilcanas.
Hivi ni wewe!!? Au naota!! Hahahahahaha....!!
 
Ndugu....

Toka Kongo itumie Silaha za jadi na bunduki ,lini ilipata AMANI?!!!

Huko kwengine ni wapi mtutu wa bunduki ulitumika kuleta usalama ?!!!

Ethiopia inaendelea kuteketea......

Miaka 20 waliyotumia MAREKANI na NATO ndani ya AFGHANISTAN haikutuliza MAPIGANO....leo US wameondoka huko na hali imerudia upyaaaaaa.......

Kumbuka inapotokea Vita baina ya makundi mawili huwa mwanzo wa makundi mengine(kumeguka ama kupandikizwa).....

TULIZA KICHWA WEWE

#NchiKwanza
#JMTMilele
#KaziIendelee
Kumbe unajua vizuri pale umma unapochafukwa hakutakuwa na utulivu tena.

Huu uonevu ndio unaowaamsha hata waoga kuvaa roho za kikatili nakubadilika pasipo watawala kuamini.
 
Kwenye hili nasema hapana, hapana, natofautiana sana na samia na serikali yake, kwenye hili hapana. hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa dhidi ya serikali hii.
Tundu Lissu na John Mnyika hiki ni kipimo cha uongozi wenu na umakini wenu kwa chama.
Kesi hii itamfanya mwenyekiti Mbowe akae mahabusu miaka na miaka. je chama kinachukua hatua gani dhidi ya serikali dhalimu kuwahi kutokea nchini kwetu?????
Tundu Lissu na John Mnyika itisheni mkutano mkuu wa chama , from there tekelezeni yale mtakayokubaliana, kuitangazia dunia tu kwamba serikali ya huyu mwanamke ni serikali ya kidkiteta hakufanyi mwenyekiti atoke.
Samia ni rais wa miaka minne tu , tena mpaka Mungu apende
 
Back
Top Bottom