Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Kisutu, Dar: Mbowe afikishwa mahakamani kwa Ugaidi. Akosa dhamana na kupelekwa rumande. Kesi kuendelea Agosti 5, 2021

Kukusanya watu wakati wa janga(epidemic) kama korona ni ugaidi, acha ashughulikiwe!

Na zile hela wanazopokeaga Nairobi baada ya Lissu kuzisomba toka ulaya wanadhani vipepeo hawazionagi? Vipepeo wako katika inner circle ya Chadema,mnakaa mnapanga, zinavujishwa!

Angalia kiwango kikubwa cha usaliti wa viongozi wakuu wa CDM, Mashinji, aliyekuwa katibu mkuu Bavicha sasa waziri, angalia wabunge wa COVID, chama kimeingiliwa siafu,wametoka baadhi tu,wengi wamo bado
Hahahaha mashinji ni waziri ? Doooh
 
Makamanda haraka Sana tuanze kuchanga pesa ya gharama ya kuendesha kesi na kumlipa wakili wa chama peter kibatala
 
Tabia chafu za wapinzani ni zipi hizo?
Matusi mliyotukana baada ya zile kauli za Rais siku kakutana na wahandishi wa habari yalikuwa madogo? Yale maswali yalikuwa ya papo kwa papo, bado mlikuwa na room ya kuhoji majibu aliyoyatoa kistaarabu, na angeweza kubadilisha majibu yake, nyie mkaopt njia ya matusi
 
Mama D najua hu smart, Sana , ila Zungumza na Mungu wako , mh Mbowe na UGAIDI ni wahongo, ebu KWA imani YAKO amka usiku wa leo saa 9, na dakika 47 , Kama kweli upo na Mungu ,tulia takika 15 then wakati huo muombe Mungu akupe tafakari ya taifa Hili , utaweza Kama upo na Mungu na hutoweza Kama hauna, ila ukiweza ,nasema ipo siku utanishukru badae ,thanks mama d


Nitakuamsha huo muda

Siwezi kumtetea mwenyekiti sababu binadamu wana mengi mioyoni mwao.... Ila naweza kusema kuwa mwenyekiti huwa hakemei maovu kabisa





Ni kama baba asiyeweza kukemea watoto wake wakorofi na hii inaweza kuwa utekelezaji wa mipango ya familia yake



Uongozi ni kutimiza wajibu na kuwajibika na Hakuna litakalofichika milele hata yale mengi tusiyoyajua yatakua wazi tuu
 
mandela na hii issue ni tofauti kabisa, wala usichanganye. mandela alikuwa kwenye apartheid, cdm mpo kwenye vyama vingi mnaruhusiwa hadi kuwa na mikutano ya ndani (mama alisema), matokeo yake ninyi mkamwona mpole mkaanza kuleta fujo na njama za kumzengua, matusi kibao (mdude na mbowe), ishini mkijua kuwa nchi hii sio ya wanachadema peke yake, kuna watu wengine wenye mawazo tofauti na imani tofauti na ninyi ambao pia mnatakiwa kuyaheshimu kama kweli nini ni wanademocrasia. hivyo mnapofanya yote hayo jueni kuna watanzania wengi tu hawayataki na serikali ina wajibu kuwawekea mazingira mazuri ya kuishi hao nao pia kwasababu ninyi ni fungu mojawapo tu la watz walio wengi, na hamuwakilishi watz wote.
Ni vitu vinavyofanana. Tofauti ni wakati na ki jinsi gani ya ukanamizaji. Hata RSA, ANC kilikuwa ni chama halali na kilikuwa na viongozi wake na walifanya mikutano pia. Kwetu ni mbaya zaidi kwa kuwa unyanyasaji unafanya kwenye nchi huru na ndugu kwa ndugu.
 
Kuwa Tanzania ni ya CCM? Huo umefika pasipo shaka, learned person usiyejua kuandika.

Amandla....
ninyi mnasema 10 ni cdm, waliobaki ni 50m ambao ndani yake ondoa watoto 20m approximately na 2m wa ACT an NCCR. wanabaki ishirini na ngapi hapo wa chama cha kijani? hesabu ndogo ya mtu mwenye ubongo wa kawaida kabisa.
 
Wanaosambaza taarifa kwamba Mbowe amefikishwa mahakamanj kwa Ugaidi nadhani wanapotosha ili kuvifanya vyombo vya dola vitoke adharani kueleza kwanini afikishwi Mahakamani. Leo kwenye vyombo vya habari tumeona dreva tax aliyepewa kesi ya MO ameachiwa, vyombo vilivyoripoti habari hii vilikuwa Kisutu, je Mbowe amepitushwa Mlango gani waandishi wasimwone? Gaid kwa namna tulivyozoea kuona walivyokuwa wanalindwa mashekkhe wa uhamsho si escort ambayo unaweza ukaificha.

Lakini pia hii nikuichafua mahakama, maana hakuna makosa yanayoonekana ya mtuhumiwa. Means mahakama inarudi kulekule ambako ilijaza watu mahabusu wasio na kosa kwa kisingizio imefungwa mikono.

Tatu nikumchafua Mhe. Rais, kwamba yeye anahusika na hiki kilichotokea. Mwenyekiti wa chama Cha siasa kuwekwa ndani kwa Ugaidi ambao Watanzania milioni 60 awauoni na ambao hakuna ufafanuzi nikumuhusisha moja kwa moja Mhe. Rais kwenye Jambo ambalo hata wananchi wasipoandamana Wala kuingia mtaani, hakuna namna ambavyo utaweza kuwaaminisha watu wa ndani na wageni kwamba ni sehemu salama.

Hii itatoa picha kwamba ipo siku dangote atakamatwa na kuitwa Gaidi Kisha Mahakamani to gerezani, wamiliki wa viwanda na biashara watakamatwa na kuitwa magaidi Kama ambavyo dola ilitumia neno uhujumu uchumi kuwafilisi watu na kuwanyang'anya Mali zao.

Sidhani Kama Rais aliapa kuifanya hii nchi isiwe sehemu sahihi pakuwekeza na kuhifadhi fedha iwe sehemu sahihi yakuchuma na kupeleka kwenye mabenki nje.

Katika Hali ya kawaida kabisa tutakuwa tunashika namba moja Duniani kwa kukiuka haki za binadamu na kuwa na Taifa ambalo hakuna sheria.

Japo sikatai kwamba kwa akili za watu wasiofikiri sawa sawaswa na kwa akili za watu ambao wameakikisha wanarithishana madaraka Kama wafalme sioni Kama haiwezekani kuwaweka watu ndani wanavyojisikia kwa sababu wamejimilikisha nchi.

Wanaopaswa kushauri haya sidhani Kama wataweza kwa sababu JK mke na mtoto wapo bungeni si kwa sababu Wana sifa Bali kwa sababu wamepewa nafasi na utawala uliopo, ataanzaje kuhoji? Mzee Mwinyi naye akihoji haya mwanaye ni muhusika mkuu. Mzee Lowasa mwanaye yupo Dodoma, Warioba mwanaye yupo kwenye mfumo so sidhani kama yupo wakuyapinga haya yasitikee Tanzania.

Ushauri tu ni kwamba, kwa Hali ya Dunia ya Sasa upo uwezekano tutashindwa hata kulipa mishahara au tukauza nchi kwa wachina kulipa mabilioni na matrilioni tunayokopa kufanya mambo ambayo Taifa lingekuwa la haki yangefanywa na wananchi wenyewe.

Mbowe naamini yupo mahabusu osterbay na hana Ugaidi ndani yake.
Beatrice Kamugisha kuwa mpole, subiri uone charge sheet ndiyo urudi kusoma ulichoandika.

Mbowe anaishi nyumba ya vioo halafu anarusha mawe nje. Lazima watakurudishia.

Maisha ya Mbowe kiuchumi na kibiashara kafanya kazi zote halali na chafu. Siku zote Deep State ipo kazini. Huwezi kuwa drug trafficker ukataka uje ututawale Watanzania.

I hope umenielewa
 
Nitakuamsha huo muda

Siwezi kumtetea mwenyekiti sababu binadamu wana mengi mioyoni mwao.... Ila naweza kusema kuwa mwenyekiti huwa hakemei maovu kabisa


View attachment 1869264


Ni kama baba asiyeweza kukemea watoto wake wakorofi na hii inaweza kuwa utekelezaji wa mipango ya familia yake



Uongozi ni kutimiza wajibu na kuwajibika na Hakuna litakalofichika milele hata yale mengi tusiyoyajua yatakua wazi tuu
watu kama hawa nao wakiwa segerea watalalamika. hata heshima hawana.
 
Ni vitu vinavyofanana. Tofauti ni wakati na ki jinsi gani ya ukanamizaji. Hata RSA, ANC kilikuwa ni chama halali na kilikuwa na viongozi wake na walifanya mikutano pia. Kwetu ni mbaya zaidi kwa kuwa unyanyasaji unafanya kwenye nchi huru na ndugu kwa ndugu.
unasemaje kuhusu kauli za kichochezi za mdude na Tundulisu? unaziunga mkono? mbowe anaziunga mkoni? mna agenda gani?
 
Haki nimekasirishwa sana na kitendo cha serikali kuonea wapinzani na kuwatisha kwa kumfunga mbowe. Wa ajua wanaweza kukaa naye kwa muda wanaotaka na tusifanye chochote, hii siyo sawa.
 
Haki nimekasirishwa sana na kitendo cha serikali kuonea wapinzani na kuwatisha kwa kumfunga mbowe. Wa ajua wanaweza kukaa naye kwa muda wanaotaka na tusifanye chochote, hii siyo sawa.
pasuka basi, au nenda burundi.
 
Muda sio mrefu tumeanbiwa kuwa anaumwa sana hajiwezi na polisi wamekataa kumpeleka hospitali, kuna ukweli wowote au zilikuwa ni tetesi tu kama ilivyokawaida ya BAVICHA?
Bavicha huwa wanajaribu kupima upepo wa mtaa. Mtaa nao uko busy na mambo yake. Ukipita vijiweni watu wanajadili Yanga na Simba.
Hawajui hata Mbowe kakamatwa.

Wakipita panapouzwa magazeti wakisoma habari ikionekana hiyo ya Mbowe wanasonya tu nakusema"huyu nae amezidi".
Wengine wanadai anamuonea mama,mbona kipindi cha Magu hawakuthubutu?

Chadema tengenezeni sera mbadala,hii ya katiba imebuma. Nadhani wananchi wanauelewa sana kuliko mnavyofikiri ninyi.

Mbowe na group lake,hawataamini pia uchaguzi wa 2025 watakula za uso kama 2020.

Wajipange.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom