Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu


MKuu umesahau ya Kitlya? imeisha kwani?
vipi ya IPTL ? Imeisha?
 
Dola ili isimame lazima iwe na uwezo wa kuchukua hatua kali dhidi ya wahalifu.

Hata hivyo dola lazima iwe na huruma,kwa sababu kuna baadhi ya wale walio ndani ya dola (baadhi ya wananchi) ,hukosea kwa bahati mbaya ,hivyo huitaitaji uangalizi ili wajifunze.

Kabendera kahurumiwa na serikali kwa kiwango kikubwa sana ,ashukuru kwa mikono miwili.
Kosa alilolifanya alistahili kupigwa risasi hadharani tukishuhudia .

Japo mahakama haijathibitisha hatia yake ,tukubali tukatae serikali imejiridhisha ni muhalifu ,ila imeachia mkondo wa sheria ufuatwe.
Ingekua china pumzi yake ingekua imekata kwa sasa .
Kwasasa kabendera yuko mikono salama ni jukumu lake kutafakari matendo yake kwa taifa.

Tanzania yenye watu millioni sitini ni muhimu sana kuliko kabendera na wanaomtumia kipumbavu.

Mwisho , serikali iache huruma ,kuna wengine hawastahili kuhurumiwa kwa matendo yao.
 
Ni kweli kaka hata kesi yake hii ni kwa sababu tu na maandishi yake kwenye gazeti la The Economist.Nadhani aliona kama risk alokuwa anachukua.Unakumbuka yule mwandishi wa Saudi Arabia alivyokatwa katwa vipande vipande kule Uturuki?Basi mimi naona ukiwa kwenye serikali kama hizi zilizo tayari kufanya lolote kwa kulinda maslahi yao lazima uwe care sana unless upo tayari kwa lolote.Cha kusikitisha familia yake ndiyo itakayohangaika.
 
Pascall Mayalla Mungu anakuona ujue, wakati haka kajamaa kamekazana na viarticle vile wewe ulikuwa umekazana kuvipandisha humu Jamvini kwa mbwembwe.
Ona sasa kametiwa nyavuni. Mungu anakuona Pascall Mayalla.
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.

Kama lini Mkuu ,la Mh Lissu ni mfano tosha kuwa Haki hamma na inavunjwa kwa Makusudi na waliopewa Dhamana.
 
duh! aisee
mleta uzi bando haitoshi kuelezea mkasa huo maana kama umebanwa vile way to maliwato
 
Nina shida na misingi ya utungaji wa sheria zetu. Jambo linalofanyika sehemu nyingine duniani sio lazima tulibebe kama lilivyo maana mazingira ya dunia yanatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine

South Africa kosa la mauwaji (murder) linadhaminika. Sasa hapa kwetu mazingira ni tofauti kwasababu kwanza usalama wa mtuhumiwa umezingatiwa katika suala zima la kumnyima dhamana

Sasa sioni ugumu uko wapi wa shitaka hili la utakatishaji lisiwe na dhamana maana mazingira ya huko "duniani" tulipoikopi sheria hii ni tofauti na yakwetu na maranyingi fursa hii hapa kwetu hutumiwa na waendesha mashtaka kuwaadhibu watu kabda hawajkutwa na hatia

Nahoji misingi ya utungaji wetu wa sheria kwa sababu wakati mwingine utaona haziko reasonable

Leo hii mtu akikamatwa anasafirisha kilo hamsini za miraa/mirungi na akipatikana na hatia adhabu yake ni KIFUNGO CHA MAISHA!!!

Mirungi ambayo hapo nchi jirani ni biashara halali lakini sisi tumeweka capital purnishment huku jambazi wa kutumia silaha anaadhibiwa miaka 30 tu!!!
 
Mkuu embu nitag makala zake mbili tatu
 
Limsiba hili
 
huyu jamaa anaumiza watu wengi sana Erick siyo mharifu tusingepiga kelele angepotezwa wako wapi viongozi wa dini waliokuwa natoa waraka enzi za jk
 
alifanya nini kiasi kuwa tuone kuwa tuna haki na Damu yake iwe mikononi mwetu.
hebu tueleze tuelewe vizuri inaelekea kuna kitu unajua sisi wengine hatujui ili itusaidie katika kumuhukumu na kumuonea huruma kwa makosa aliyotenda kwa kuwa na yeye ni mwanadamu dhaifu tu kama wengine.
 
Wewe ni mpumbavu mwingine tu unayedhani uhai wa mtu ni kitu kidogo. Damu ya mtu iliyomwagwa bila hatia kamwe haitaenda bure. Kama mtu ni mhalifu ashitakiwe kwa kosa halisi alilofanya. Sio unamkamata kwa shida ya uraia unapokosa ushahidi unamshtaki kwa kosa la kutakatisha pesa. Wekeni wazi. Kama ni zile makala za kukosoa jiwe, semeni sio unasema kutakatisha pesa tu ili umkomoe mtu kwa kumnyima dhamana. Malipo yake yanakuja na wala hayatakawia.
 
Wewe Ndiyo mjinga aka stupid kwa kuandika mbupu! MTU shujaa huyu.
 
Kumbe kuna watu ambao mnaijua kesi hii nje ndani. Maoni yangu yalikuwa, kama hatuna habari au taarifa kamili, hatuna haja ya kulaumu vyombo husika, kwa maaa wao wamejiridhisha mpaka wakampeleka mahakamani kwa mashtaka hayo.
Mashtaka yepi
Mara uraia mara uchochezi
Leo kesi ya kubambikizwa
Yana mwisho haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…