Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Brave and patriotic? angeweza kuandika makala kama zile under a false ID, pia unaweza kufuatilia kila kitu bongo ukiwa nje, dunia ni kijiji hiki, zile makala zake zilikuwa zinachambua tu hotuba za magufuli, miradi anayoifanya na sera zake ambazo hata ukiwa Australia huko ukifuatilia utafahamu tu, au unaweza kuniambia ni vitu gani aliandika ambavyo mtu ukiwa nje huwezi kuvijua? vyote vipo wazi tu, sema yeye ameandika katika kuvikosoa

pia unaweza kuwa na watu wako bongo wanaokupa taarifa za ndani ambazo haziwekwi kwa waandishi, akina Mange kimambi, Ngurumo wanapata intel nzuri tu na wapo nje, hivyo ndivyo waandishi pragmatic, wanavyoishi kulingana na uhalisia wa hali, sio kujifanya unakufa kishujaa, kesho wanakusahau, unaacha familia inateseka na hakuna mabadiliko yoyote uliyofanikiwa kuyaleta sababu ulienda kiboya


Nyie vijana mngekuwa ndo mko enzi za kupambana na mkoloni, uhuru ingekuwa ndoto
 
Sijasoma makala zake zote lakini zile nilizosoma niliona ni za kawaida tu ingawa ni critical kiasi. Labda tatizo lake ni kuandikia wasomaji wa nchi za nje!
Gazeti lilikuwa linatumia lugha kali dhidi ya Magu kuna makala moja aliitwa foolish, pamoja na lugha nyingine kali tu, sasa huwezi andika vile halafu ukabaki salama mkuu, jamaa alikuwa mjinga hata kama alikua akikosoa kitu sahihi
 
Waandishi mjifunze huu utawala hautaki kukosolewa.unaweza kujikuta unaingia matatizoni ukaipa tabu familia yako.toroka kaandikie ulaya huko
 
Ok...sawa...Hapa kuna vyombo vvya dola vingi...Kuna usalama wa taifa, polisi, JW, Magereza na kadhalika...Through my experience naamini kuna chombo kilimkamata kisheria ingawa siyo Magereza...Soma sheria zinazoongoza vyombo hivi vya dola..Kwa mfano soma sheria ya TISS ya mwaka 1996..ACT No. 15 of 1996.

Man! Mie nakuuliza tukio lilivyoenda wewe unanipa nadharia? We are in the country where law does not apply
 
Kwa stament hii unaungana na wote wanaosema mliemchagua huyu mtu mmeiletea laana kubwa nchi hii kiasi kwamba vizazi vyenu vitaiishi hii dhambi so kwa mtazamo wako watu wawe wapole waunge juhudi za mateso Mimi nadhani ikiwa unakubali now tuna watawala dhalimu naww huna ujasiri wakusema kitu nivyema uka Support wenye huo ujasiri huo naww ubakie kwenye keyboard ukiamini iko siku dhulma itakoma bila kujali ni lini maana doctors wengi kutoka mamlakani nivile Mungu aamue refer hotuba ya uzinduzi wa Terminal 3
Kwa nini nisupport vitu ambavyo mimi mwenyewe nimejificha kwa ID fake. Mtu anafanya kitu cha hatari. Kama kweli unamsupport speak out openly siyo kujificha kwenye jina fake. Unafki tu. Mtu upo na ID fake then unamwambia well done unampamp aendelee. Kama upo serious muunge mkono asilimia mia kwa kuisema serikali ukiwa unafahamika.
 
Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha fedha. Kisheria, kosa la utakatishaji fedha halina dhamana. Ni kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake tu mahakamani. Yajayo yako vyema sana...
Kuna umumihu wa ku-challenge haya mambo mahakamani, watupe constitutional review ya huu utaratibu. Nini ni special sana kuhusu kutakatisha pesa mpaka kumnyima mtu uhuru wake?

The state imepewa power kubwa sana hapa. Am not a lawyer, lakini najua wenzetu wana angalau utaratibu wa mahakama kufanya evaluation ya evidence (Preliminary hearing) kama sikosei, ili kujua kama kuna walau probable cause ya kuendelea. What's the remedy hapa? Kama ikija kuonekana charges were frivolous, Erick anapataje haki yake kwa muda wote aliopoteza uhuru wake? Do we have any remedy? Kuna mfano wowote wa Serikali kubanwa baada kushindwa mashitaka yasiyo na maana?
 
Kwahiyo Mandela alikuwa mjinga mpaka kuwekwa miaka 27 jela. Alitakiwa akimbie nchi yake!
Ukiwa mpiganaji au mwanaharakati au yoyote unaefanya kazi ya hatari, first and most important ni kukwepa kukamatwa na unaowapiga

Ila kuna situation ambazo huwezi kukimbia, unaweza kuta lazima ubaki na wafuasi wako ili kuwahamasisha na kuendesha chama n.k hivyo inakulazimu kubaki

Lakini kwa case ya Kabendera ilikuwa tofauti, ni kitu kilichokua kinakwepeka kabisa, mfano angetumia tu hata fake ID ingemgharimu nini? Kuna waandishi wengi wanafanya hivyo
 
Nakuonea huruma Erick
Wamekuweza na wamekupata
Lakini kwa hii dhuluma unayofanyiwa Mungu atakulipia.

Nchini Ethiopia kuna watu sasa wanaolipwa fidia na serikali mpya ya nchi hiyo baada ya kuonekana walitendewa mambo mabaya na serikali iliyopita!
 
Mimi mtu poa sana na sina hayo unayofikiria.

Ila nasisitiza nimetoa maoniyangu na maoni yanaweza kuwa ya aina tofauti.

Haya tusiende mbali nje ya mada.
Basi Richard hacha ukatili. Mwenzako anapoonewa au kuteseka usifurahie bali muonee huruma na umwombee faraja. Hivi kwa mazingira ya tangia kukamatwa kwa Erick, taarifa zote za polisi/uhamiaji za kimagumashi bado ujaona kama kuna uonevu wowote. Hata kama wakubwa hawakukipenda alichoandika Erick, basi wawe wawazi wamkamate kwa utaratibu unaotumiwa katika kukamata watu wengine wa kariba yake na waseme wanamkamata kwa kosa hili au lile. Siyo kutuletea maigizo wakati mwenzetu anateseka na familia yake inasoneneka. Halafu eti mtu kama wewe uoni tatizo unashangilia mwenzako kuteseka kwa kisingizio eti umetoa maoni. Hacha roho mbaya muonee binadamu mwenzako uruhuma anapoteseka/anapoonewa tafadhali.
 
Hawa huitwa "auxiliary force" na hufanya kazi na wote TISS, Polisi na Uhamiaji.

Sisi twawaita "watu wasojulikana" na wengi tunao mitaani wakipewa taarifa za mlengwa basi hujiandaa kukuzungushia wigo.

Kama umemsikiliza kwa makini jamaa ya Uhamiaji amesema kwamba ilibidi wavae kiraia ili kuweza kumkamata mhusika.

Hamna lolote, hakuwa wa kitisho hivyo. Lengo lilikuwa ni kumalizana naye nje ya uwanja, maana hawana grounds za kumshtaki mahakamani zaidi ya kesi za kuchomekea. Walipoona haijakaa vizuri ndio ikabidi wajifanye ni uhamiaji. Watanzania wajinga waliisha enzi za Nyerere, kwa sasa watu wanajua nini kinaendelea. Ww poteza muda wako kujifanya unatoa maoni sana sana unaonekana juha unayetetea uovu.
 
Ukiwa mpiganaji au mwanaharakati au yoyote unaefanya kazi ya hatari, first and most important ni kukwepa kukamatwa na unaowapiga

Ila kuna situation ambazo huwezi kukimbia, unaweza kuta lazima ubaki na wafuasi wako ili kuwahamasisha na kuendesha chama n.k hivyo inakulazimu kubaki

Lakini kwa case ya Kabendera ilikuwa tofauti, ni kitu kilichokua kinakwepeka kabisa, mfano angetumia tu hata fake ID ingemgharimu nini? Kuna waandishi wengi wanafanya hivyo

So kwa maelezo haya unakubali hakuna kesi hapo bali matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya wakosoaji?
 
Back
Top Bottom