Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Huko kwingine umezunguka sana nafurahi hata wewe umeona shida ilipo hapo ndo penye point ya msingi katika andiko lako

Hivyo basi utakatishaji ni kwa namna wanavyoweza kuitumia hiyo nafasi kumtesa jamaa

Ukiwa na makandokando unapaswa kuwa mwangalifu katika mambo mengi ya msingi kwenye maisha yako.

Hii ni kanuni muhimu sana.

Pili, hakuna serikali yoyote duniani ambayo itakuachia ukimtusi kiongozi wa nchi iwe Marekani, UK au kokote kule.

Wao wana mbinu zao nyingi tu za kukunyamazisha, nafikiri umesikia walokutwa na mbinu hizo kwenye hizo nchi.
 

Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera amefikishwa Mahakama ya Kisutu leo

Anashtakiwa kwa makosa matatu chini ya sheria uhujumu Uchumi ambayo ni...

1. Kujihusisha na mtandao wa uharifu, 2015-2019 katika maeneo ya Dar Es Salaam aliongoza kundi la uhalifu kwa lengo la kupata faida au manufaa mengine

2. Kukwepa kulipa kodi. Katika tarehe tofauti kati ya 2015 hadi 2019 katika jiji la Dar es Salaam alikwepa kulipa kodi zaidi ya Tsh milioni 173

3. Kutakatisha fedha haramu.

View attachment 1172905
View attachment 1172906
View attachment 1172907
ya kumkashifu RAIS yamepotelea wapi!? Actually no sense.Mara hili Mara lile. Mungu yupo!?
 
Huna lolote wewe, kumbe una-judge mwenzako kuwa chequebook Journalist na inaonekana wewe mlamba viatu vya hao unaowata wakuu wa nchi. Wakuu wa nchi wasiotaka kukosolewa ni dictators. Kwa hiyo ukiwa mkuu wa nchi hukosei na kukosolewa. Haya wewe endelea kulamba viatu vya hao wanakupa kiburi cha kuwahukumu watu ukizani wewe mwema.

Mimi sina mda wa kulamba viatu ni nyie na kundi lenu kutwa mwashinda kuwatafuta wazungu wa kuwalamba viatu.

Nina kazi yangu ya kujiajiri na yaniingizia mapato ya uhakika 24/7

Nina nina kipato kuliko wewe.
 
Ukiwa na makandokando unapaswa kuwa mwangalifu katika mambo mengi ya msingi kwenye maisha yako.

Hii ni kanuni muhimu sana.

Pili, hakuna serikali yoyote duniani ambayo itakuachia ukimtusi kiongozi wa nchi iwe Marekani, UK au kokote kule.

Wao wana mbinu zao nyingi tu za kukunyamazisha, nafikiri umesikia walokutwa na mbinu hizo kwenye hizo nchi.

Hii picha ya Kabendera itatumika sana huko tuendako hasa kwa watu sugu kama kina sugu et al...mwendo utakuwa ni kutakatisha pesa/uhujumu uchumi halafu kabatini kwa muda usiojulikana hivyo inabidi waanze kujiandaa kwa hilo kwani hamna jinsi bali ni kizuizini kiaina
 
Pole Kaka jamani kabla ya kufanya upumbavu muwage mnafikiria na watoto wenu. Sasa watoto wanateseka kisa ujuaji wa baba yao. Yaani huyu hana tofauti na Victoire wa Rwanda aliecha familia yake Uholanzi kisa kwenda kumpinga Kagame. If you cant beat them,then join them.
Lazima uambulie mapovu hapa kutoka kwa wild beest migrant huko Serengeti na maasai Mara
 
Usimfananishe Maxence Melo na waandishi uchwara kama Kabendera.

Max anaendesha JF na imesimama kwelikwekli na kila mara yupo tayari kukabiliana na misukosuko yoyote ile.

Kama Kabendera angakuwa mwandishi makini na anaejiamini basi asingetumiwa na watu kama Zitto na hilo Jarida la "The Economist".

Kuwa mwandishi makini ni pamoja na kuwa na vyanzo vya habari zako na vigezo au facts zote ili siku ys siku uwe tayari kupambana hoja kwa hoja facts kwa facts.

Wengine wamegusia kwamba pia usiwe na makandokando maana kuna watanzania wengi tu wanabeba pasi za kusafiria za nchi zingine ilhali wana pasi za kitanzania.

Erick Kabendera kwa sasa ni mtuhumiwa ambae anakabiliana na kesi ngumu sana itayomweka ndani kwa muda mrefu kidogo, kutokana na ujinga wake wa kutumika na hata maadui wa nje wa serikali ya awamu ya tano.

Watu wa aina ya Kabendera wanaishusha sana hadhi ya uandishi wa habari khasa zile za kiuchunguzi kwa kuendekeza bahasha za haki au "Chequebook Journalism."

Mtu mzima na akili yako tena una familia na wategemezi wengi bado unakuwa waendekeza ubahau bila kufikiri kwanza madhara ya matendo yako.

Now, he has to face the consequences of his actions.
Hizi ndio zile akili za jalalani (kwa Propesa Kalamaganda).

Ni rahisi kusema anatumika bila kuwa na ushahidi. Uandishi wake ungekuwa na upotoshaji angeshtakiwa kwa makosa yanayohusiana na uandishi wake. Kwenda kumbambikia kesi isiyohusiana na uandishi wake unathibitisha uandishi wake, japokuwa hawakuupenda, haukuwa na dosari.

Hizi kesi za utakatishaji wa fedha ni kichaka cha watawala kuweka watu ndani na kuwanyima dhamana bila uthibitisho wowote. Wameshindwa kumpoteza, wameshindwa kwenye uraia, wameshindwa kwenye uchochezi na hili pia watashindwa.

Wenye makandokando wote ni wanafiki kama wewe na makunguru, huwezi kuwa na makandokando and speak against this regime.

The only reason he has been a target is because of his journalism.

Freedom comes with a price and some are willing to pay it.
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
Waiii acha kujifanya kondoo, kuna vyombo vya haki hapa nchini!?
 
Lazima uambulie mapovu hapa kutoka kwa wild beest migrant huko Serengeti na maasai Mara
Yaani when i speakout my mind,yaani hayo mapovu yao nayaona ni manukato tu halafu mimi wala siwatukani naandika ideas zangu tu.
Kama wao kweli wana msuli kwa nini wasijirecord walau wanamuunga mkono ERICK?Unafki tu kumtetea kwenye ID Fake.Huwezi shindana na dola peke yako lazima uwe na kundi kubwa nyuma yako.Erick kajitoa mhanga yupo peke yake leo celo kama kweli wapo na yeye si waende nae lupango?Hawa wala hawanisumbui.
 
Kesho tutasikia anashitakiwa kwa ubakaji, au ujambazi wa kutumia silaha au mauaji. Who knows?
 
Gazeti lilikuwa linatumia lugha kali dhidi ya Magu kuna makala moja aliitwa foolish, pamoja na lugha nyingine kali tu, sasa huwezi andika vile halafu ukabaki salama mkuu, jamaa alikuwa mjinga hata kama alikua akikosoa kitu sahihi
Mjinga sana yule.Kina Zitto walikuwa wanampa macomfo kumbe wanampoteza tu.
 
Yani hizo kesi haziihitaji utaalamu kivile kujua ni za namna gani...
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
Siwezi kamwe kuiamini serikali hii ya awamu ya tano imelaaniwa.
 
Back
Top Bottom