Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Ukivunja sheria sharti ukamatwe na upewe adhabu,hakuna nchi duniani inakaa na kuvumilia wahalifu Wa sheria
 
Unavyonitukana kosa langu ni lipi?
Yaani kuwapa ushauri wa kuwa mimi pamoja na wengine ambao hatuna taarifa kamili kuhusu hili tusijielekeze kulaumu Bali tujipe Muda ili haki itendeke.
Hakuna haki, walimteka kwa style ya watu wasiojulikana baada ya kelele kuwa nyingi za ndani na za kimataifa ndiyo polisi/immigration wakajitokeza kusema wako naye, yaani wakawa wametuondelea utata wa kufahamu wasiojulikana ni akina nani.
Bila ya aibu baada ya ile ya uraia kubuma kwani wakaona ingebidi na ukoo(the whole extended family) wake wote ukamatwe ndiyo wakabadilishia gear angani kwa kuja na kesi feki za uhujumu,utakatishaji fedha na kujihusisha na magenge ya uhalifu/ujambazi na kituko zaidi yote hayo ameyaanza 2015(read between the lines).
Hivyo vyombo vinavyopaswa kutoa haki ni sehemu ya tatizo hapo basi jamaa kutendewa haki haiwezekani, and that's the painful truth.
 
Personally, hili sekeseke zima tangia nilione tweeter, lilioesha kabisa kuwa si salama Kwa huyu mwandishi.
Hajatendewa haki Maana alitekwa baada ya kelele nyingi Ndio akaibuliwa yuko polisi Na Ndio hiyo mchakato wa mahakamani.
Watawekwa wanasheria nguli ila kwa sheria kandamizi kama utakatishaj fedha, ataumia Tu gerezani, Maana hakuna dhamana.

So Mpaka hapo hawezetendewa Haki. MUNGU yupo Lakini. Naamini yatakwisha.[emoji120]
 
Kila zama zinaukurasa wake, yawezeana kabisa, anaonewa sawa, ila je karam yake aliitumia vzr? Je jamii inafaidika na mandiko yake? Tuseme sawa inafaidika je kwa nn anamgoror na sheria?

Rejea kumbukumbu ya wale wanamziki, ni vyema ukacheza na karam vzr ila usicheze na taasisi kubwa kama sheria,

Kila nchi watu kama hawa watu, ila inategemea wanashughulikiwaje, kunawngine huwekewa vikwazo vya kibiashra, wengine za kidiplomasia, kunavizuiz na wengine kupewa nyadhifa ila wakiona taratib haziruhusu, lile andiko linahusika Aheri mtu moja kunyamaza ili taifa lipone, kuliko kuruhusu mtu mmoja kusema taifa zima likapotea
...

Hyo ni sera ya dunia..
 
Kuna vipofu hawaoni huu uonevu unaoendelea na bado wanataka jamaa atawale miaka hata 20. Time will tell hakuna mengi ya kusema
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
Kuna mambo unayachkulia poa kwasababu yamemkuta mtu ambae hana msaada kwako. Ila usiombe yamkute mwenye msaada kwako ndo utaelewa mbivu na mbichi.
 
Gazeti lilikuwa linatumia lugha kali dhidi ya Magu kuna makala moja aliitwa foolish, pamoja na lugha nyingine kali tu, sasa huwezi andika vile halafu ukabaki salama mkuu, jamaa alikuwa mjinga hata kama alikua akikosoa kitu sahihi

Kwa bahati nzuri hiyo nililosoma na jina la Kabendera kama maandishi hazikuwepo! Nadhani Jarida la Economist hakuna utaratibu wa kuonyesha majina ya waandishi kwenye makala zake. Anybody could have written the article. Kwa jinsi nilivyouona uandishi wa Kabendera siyo Tahiti kutumia lugha kama hiyo.
 
Kwa bahati nzuri hiyo nililosoma na jina la Kabendera kama maandishi hazikuwepo! Nadhani Jarida la Economist hakuna utaratibu wa kuonyesha majina ya waandishi kwenye makala zake. Anybody could have written the article. Kwa jinsi nilivyouona uandishi wa Kabendera siyo Tahiti kutumia lugha kama hiyo.
Kuna articles nilioona ambayo kulikuwa na jina lake, hata kama hiyo article ya foolish haikuwa na jina lake inajulikana yeye ndiye mwandishi wake kwa hapa Tz so kwa namna moja ama nyingine hiyo article imetokana na yeye tu, anyway kuwa mwandishi wa hilo gazeti tu kunatosha kukufanya kuwa adui wa Magu kutokana na makala zake kwa utawala huu
 
Back
Top Bottom