Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Nani aliwahitoka mahabusu kwenda kwenye mazishi ya mama ama baba yake ama mtoto wake? Kwani watu wangapi waafiwa wakiwa magerezani lini wakaachiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app

We acha kuongea kamlevi wa gongo…!
Kumbuka Mahabusu bado siyo mfungwa mpaka pale MAHAKAMA itakapo thibisha vinginevo!
Juzi kule Kenya tulishuhudia yule mama Sarah aliyemwua mmewe wa Kizungu akiruhusiwa na Mahakama kwenda kushiriki mazishi ya mmewe! Je huyo hakuwa mahabusu?Au Wakenya ni wajinga sana kuliko Watz?
 
wanasiasa walipaswa kukaa kando sasa hivi wanachukulia msiba wa Mama Kabendera kama turufu yao kisiasa wakati anayeathirika ni kabendera kwanza kwa kufiwa na mwanae na pili kuendelea kukaa ndani wanapoanza kutoa kauli za kuishambulia dola anayeathirika ni Kabendera na sio wao
 
January 3 , 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Ujumbe mzito wa Kabendera, wasomwa Kanisani Changombe Dar es Salaam

Erick Kabendera, Mwanahabari aliyeko Mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es salaam, ametoa ujumbe mzito kufuatia kuzuiwa kutoa heshima za mwisho, kwa Marehemu Mama yake, Verdiana Mujwahuzi. Mwanahabari huyo anayetuhumiwa kwa mashtaka ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi, amesema uchungu wa kuondokewa na mama ni mkubwa, hasa kwa mtu aliyekosa fursa ya kutoa heshima za mwisho, kama ilivyotokea kwake.
Source: MwanaHALISI TV
 
Nani kakwambia akili imewarudia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unauliza au unapigia jibu mstari?
Embu nisaidie kupiga mstari kwa kunielezea akili imewarudi kiaje, wamehama chama? La hasha, wametangaza kushindana nae urais ticket ya ccm 2020, la hasha.
Akili imewarudije, fafanua tafaadhali, so called great thinker.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni MBWA pekee anaweza kutoa maoni haya!
 
Ukatili ni sifa za kishamba sana ni sawa na ugangwe!!
 
Mungu ndiye aliyesema tiini sheria za wanadamu na tiini wenye mamlaka! Huyu kavunja sheria ina maana kavunja amri ya Mungu na wanadamu. Sasa unaposema Mungu atakulipia mi sikuelewi.
Uhuni huo kafanyie kijijini kwenu!
 

Who is kabendera? Watuhumiwa wangapi wamefiwa na hawajaenda kuzika? Hata kasusura alifiwa na hakuruhusiwa, isiwe huyu mwenye makosa makubwa hivyo? Amejitakia, na hawa wapinzani wanajifanya kuuchukua msiba kama wao, ingekuwa mimi ndio mahakam nisingemtoa kamwe ili walio nyuma yake wajifunze. Hii sio serikali ile iliyoitwa dhaifu na legelege, mtaisoma namba, walisema akina mnyika tena bungeni kwamba anatakiwa dikteta, sasa wewe unalalamika
 

Wahame chama wana ujanja gani, watangaze kushindana naye wakati saa hii wanaishi kama digidigi porini? Hapo walipo wanakufa na tai shingoni.
 
Huo ni woga wa kuogopa kivuli, kwani wanasiasa sio watanzania eti wasiongelee udhalimu wa dola, unataka nani sasa aongee, mbona rais wenu anafanya kampeni za siasa mpaka usiku wa manane yeye hatafuti turufu ?, halafu anatuambia kazi ya urais ngumu eti huwa inafika usiku wa manane hajalala, wewe saa nane usiku unapiga simu wavuta bangi kwenye ukumbi wa disco utaacha kuwa na uchovu
 

Hebu weka hayo makosa makubwa ya Kabendera tuyaone, isiwe ww ni wale bendera fuata upepo.
 
Kwani dhamana iliwekwa kwa ajili ya wafungwa au watuhumiwa? Tumia akili kidogo boss!
Kwahiyo kabendera ni mfungwa? Huyo ni suspect,hivyo dhamana mahakamani ni haki ya mtuhumiwa.
 
Kwahiyo kabendera ni mfungwa? Huyo ni suspect,hivyo dhamana mahakamani ni haki ya mtuhumiwa.
Siyo kila mtuhumiwa ana haki ya dhamana mkuu. Inategemea na shitaka aliloshitakiwa nalo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…