Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Lakini kumbuka yule ni mama yake, angekuwa mjukuu maneno yako yangekuwa ya maana sana
kuomboleza kwa huzuni Bibi kizee aliyetimiza umri wa kuishi ni janga la kusikitisha.
Makabila yetu hufanya sherehe na siyo kuhuzunika.
Teia hii ni sehemu ya ujinga usiyo wa kihaya labda kwa watu wa Dar..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Non above the law ,hakuna cha umaarufu, kujulikana ,kuwa kiongozi wala mwanamziki jela ni jela na ukishajiingiza huko lazima utoke kama sheria inavyosema
Magufuli ametoa msamaha kwa Wahujumu Uchumi ..Kwamba wakiri kwa barua kisha walipe
Hivi sasa waliowengi wako huru..

Magu alitumia sheria gani kuwasamehe?

Hii ni zaidi ya ruhusa ya siku moja kuzika Mama mzazi.
 
Ni mahabusu wangapi hufiwa na watoto,wake au wazazi wao wakiwa mahabusu? Je,hawa huruhusiwa kwenda kuwaaga/kuwazika ndugu zao ila Kabendera pekee akanyimwa haki hiyo kiuonevu? Kama sivyo basi,kwa nini mjadala usijikite kutafuta haki hii ya mahabusu kwa ujumla wao na sio Eric peke yake? Wasomi tuko sawa hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hamna hiyo precedence anakuwa ngumu sana, swali ulilouliza only smart people wanaweza jiuliza, Mimi pia nilikuwa nasoma comments nashangaa, of course ni kitu kinaumiza kutokwenda kumzika mama, ila precedence ikoje? Je kuna watu walisharuhusiwa kuzika ndugu zao wakiwa ndani? Kama wapo kwa vigezo vipi? Kama hawapo kwann kabendera a set precedence? Je mahakama ingewapa na wengine ruhusa hiyo kama kabendera angeruhusiwa? Tuiache mahakama ifanye kazi, si kila jambo ni Siasa mitandaoni.
 
Sometimes nadhani Sisi Watanzania hatuko makini au tunapenda kukosoa bila sababu?...hivi unaweza kuifatisha post hii na hili swali kweli!?..au ulikua unawahi kuwa wa Kwanza Ku comment?!.. Tafadhali soma Kwa umakini kabla hujasema chochote...post iko very clear na alichokiandika mwandishi akihitaji graduation ya std VII kukielewa...Naomba Watanzania tuwe makini..we can do better if we become a little bit careful in these small things but critical.
 
USSR,
Mh Duni Haji akiwa mahabusu kwa kesi ya Uhaini Mahakama ilimruhusu aende nyumbani kwao akamzike mama yake mzazi.
 
Inawezekana kabisa hakuna utaratibu huo hapa nchini kwetu. (Kenya nimeona kupitia vyombo vya habari walifanya kwa Sarah Cohen. Aliruhusiwa kuhudhuria mazishi ya mume wake aliyetuhumiwa kumuua)

Watanzania walio wengi waliguswa na ishu ya Erick Kabendera kwenda kumzika mama yake, kwa sababu wanafahamu yeye 'mtuhumiwa' ndiye aliyekua tegemeo la uhai wa huyo mama yake.

Isitoshe watanzania tulio wengi tunaamini baadhi ya kesi zilizofungiliwa za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ni za kukomoana tu! Na baadhi ya wenye mamlaka walishatamka hivyo hadharani! Sasakuna sababu gani ya kumshikilia mtu badala ya kumruhusu kwenda kumzika mama yake?

Kama Taifa tunatakiwa tubadilike! Kurudisha sheria za kikoloni kwenye karne hii ya 21, ni kujirudisha tu nyuma kimaendeleo, na hasa katika nyanja za kidemokrasia, uwazi na uhuru wa habari na kutoa maoni.
 
..kwani Kabendera alikuwa akiwabambikia watu keso za uhujumu uchumi, kiasi kwamba leo iwe halali kulipiziwa na aliopata kuwatesa?

..Kabendera ni muandishi, anatumia kalamu. Kwa msingi huo yeyote anayetatizwa au kuchukizwa na anayoandika Kabendera anapaswa kumjibu au kumpinga kwa kalamu.
Kwamba nawe uwe mwandishi wa habari za kichunguzi ili umjibu kichunguzi? Alaaa kuuumbe ndo maana hata Mond akisutwa na Kiba huwa anamjibu kupitia muziki!
 
Kuna mengi ya kujifunza.

Ufalme uliotoka kwa Mungu, kwa kadiri ya kitabu ya cha Mithali, kilichoandikwa na mfalme Sulemani una sifa zifuatazo:

1) mfalme huwa kama kijito chenye kutiririsha maji katika ardhi kame

2) mfalme huwa kama jabali liletalo kivuli ambacho watu hujikimga na juankatika jangwa

Kinyume chake, ufalme utakao kwa shetani:
1) huwa ni majuto kwa wana wote wa nchi.

YATAZAMENI YOTE KATIKA ROHO, HAMTAKOSA HEKIMA YA KUYACHUNGUA YOTE YALIYOJIFICHA.
 
Magufuli ametoa msamaha kwa Wahujumu Uchumi ..Kwamba wakiri kwa barua kisha walipe
Hivi sasa waliowengi wako huru..

Magu alitumia sheria gani kuwasamehe?

Hii ni zaidi ya ruhusa ya siku moja kuzika Mama mzazi.
Ongelea mlichokiweka humu,hao wahujumu uchumi walisamehewa ili wakazike mama zao?mbona mnakuwa hamna akili jamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani alizaliwa peke yake? Lini mshitakiwa aliwahi ruhusiwa kwenda kwenye mazishi? Au hii iwe special kwa huyu, mwandishi habari? Wakulima je? Wafugaji je?
Tusiishie kusikitika, tuepuke kujiingiza kwenye mambo ya kujitakia. Kulikuwa na kila njia ya kuachana na hayo lakini naona alijivunia ushujaa.
Kosa lake ni lipi haswa? Kuhujumu uchumi au kuiambia dunia ujinga na uchafu unaoendelea hapa Tanzania?
 
Waendelee kucheza na maisha ya watu ila mwisho wao upo!
masoudkipanya_B62FJ1KDOIG.jpeg
 
Back
Top Bottom