Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Kumbe kabendera huwa analia?
Huyu kibaraka ni kweli kwamba ipo siku atayalipa matusi yake?
Kamtukana nani na wapi? Mbona kwenye mashtaka take hakuna sehemu ameambiwa ametukana? Ufafanuzi please
 
Ni mahabusu wangapi hufiwa na watoto,wake au wazazi wao wakiwa mahabusu? Je,hawa huruhusiwa kwenda kuwaaga/kuwazika ndugu zao ila Kabendera pekee akanyimwa haki hiyo kiuonevu? Kama sivyo basi,kwa nini mjadala usijikite kutafuta haki hii ya mahabusu kwa ujumla wao na sio Eric peke yake? Wasomi tuko sawa hapa?

Sent using Jamii Forums mobile app
nilimsikia jaji mkuu akisema zipo sheria kandamizi lakini sio jukumu la mahakama kuzirekebisha wao niwatekelezaji, wabunge ndio wenye wajibu wakuzirekebisha na mahakama watazitekeleza, sasa wabunge wetu akina zitto mnyika sugu nao wanalalamika kama sisi tunavyolalamika, pia ipo haja ya kupima uelewa wa watu tunaowapeleka bungeni tunapeleka watu wa ajabu mno wanakalia kulumbana tu badala ya kuisimamia serikali
 
Kuna mi mtu ni kama mishetani ikiongozwa na shetani wao mkuu. Nenda mama Verdina wanakagera tunakulilia. Nchi inaongozwa na washamba.
 
Hapa ni baada ya Mkoloni na Mkoloni mamboleo kuondoka na sisi kujitawala...
 
Binafsi mimi siyo Mwanasheria. Kisheria huwezi kumtoa mtu mahabusu ili kuhdhuria tukio fulani halafu tena umrudishe mahabusu. Suala la Kabendera kweli inasikitisha lakini Mahakama haina la kufanya zaidi ya kumpa pole sana.
 
Nakubali, na nimesema Kabendera kafanyiwa dhulma. Hawakupenda anachoandika wakambambika kesi. Serikali zetu dhalimu za dunia ya tatu ndivyo zinavyo operate.

Lakini napinga kusema apewe fursa kuzika kwa sababu tu wanahabari wenzie wamekuwa wakimpazia sauti.

Wangapi wamefungwa kwa dhulma hatuwasikii wakifiwa?

Ukitetea haki tetea ya kila mtu, sio ya mwenye sauti tu.

Simtetei kama yeye bali kama jamii yeyeto mimi wewe utakuwa kule jela ni mtakuja haina mwenyewe.Kama wanawezapewa haki ya matibabu nje ya gereza wakakaa zaidi ya masiku hospitalini nn masaa machache tu ya kuaga wapendwa wao maana si jambo la kujirudia akiondoka mpendwa kaondoka arudi thus nasema tuwe kama civilized taratibu sheria sio misahafu.
 
Waendelee kucheza na maisha ya watu ila mwisho wao upo!
masoudkipanya_B62FJ1KDOIG.jpeg
 
Umeshasema mshtakiwa kwa maana bado hajakutwa na hatia.
Vipi ikitokea akaachiwa huru kwa kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
Usiwe unajitoa ufaham tu mwenzio amefiwa na bi mkubwa wake!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio tu mshitakiwa, huyo ni mtuhumiwa, tena tuhuma za kupika, ndio maana mpaka leo bado wanaunganisha dots ili kupata ushahidi, wanyama hao tunaishi nao.
 
Kweli mahakama ilifungwa mikono? Kweli kisheria mtuhumiwa haruhusiwi kuhudhuria mazishi ya mwanafamilia? Angalia mfano mmoja kati ya mingi:

Aug 16, 2019
TWIN FALLS — A woman charged with murder in the death of her child will be allowed to attend the baby’s funeral.
Amanda Dunlap, 24, faces eight counts of felony injury to a child, one count of misdemeanor injury to a child, and one count of murder in the first degree. She was charged shortly after the October 2017 death of her 20-month-old daughter, Lyryk Altom, from serious injuries
.
 
Nimewaza hivi, niko upande wa Erick na sipendi jinsi watu wanavyobambikiwa kesi ili kuwakomoa lakini anajua hasa nini alikuwa anakifanya, labda nia yake ilikuwa nzuri lakini alivyofanya haikuwa yenye kupendeza. Yeye mwenyewe anajua hatari iliyokuwa inaweza kumkabili na hata mtakumbuka siku aliyochukuliwa kwake, ukweli alikuwa anapotea ila alikuwa 'amejiandaa' ndio mpaka leo yupo.

Mnakumbuka vifo vya maafisa kama wa tatu Wizara ya mambo ya nje kitengo Misaada kutoka EU? Walikufa ndani muda mfupi sana?

Na mmeona jinsi wanachama wa EU na US kupitia balozi zao wanavyolifatilia kwa umakini hii suala la mashtaka dhidi ya Erick na hata kuonyesha Sympathy kwa msiba wa mama yake?

Nimewaza tu

huko baadae nadhani tutashtakiana sana
Hivi kwa siku zijazo upande wa serikali ukiamua kujitoa kwenye kesi hii vp hatutasema kuwa kesi hii ni ya kutengeneza kwa lengo la kumkomoa Bw Erick???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom