PreGE2025 Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

PreGE2025 Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la uhaini Wakili Nassoro Katuga.
Nimefurahi John Mallya na yule mwingine hawamo.

Mungu ni mwema
 
Wewe fala kwa mfano mimi sipo nyumbani ni mtumishi wa serikali hapa maktaba kuu ta taifa pembeni ya kisutu.
Namsapoti lissu na hapa nakusanya details za kuzimwaga humu
Kumbe huitaki serikali ya ccm afu umeajiriwa na serikali ya ccm 😂

Em acha kazi ili kuonyesha nia ya dhati ya kutaka mabadiliko mana unaifanya kazi serikali ya ccm
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008606 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Geofrey Mhini, Hakimu Mkazi Mwandamizi.

Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho kuendela na shauri ya njia ya mtandao>>> JoT - Virtual Court

Shauri limepagwa kwa usikilizaji wa awali leo 24/04/2025 saa tatu asubuhi. Hii ya Uchochezi
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, Tundu Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka la uhaini.

Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la uhaini Wakili Nassoro Katuga.

Mbali na Shitaka hilo anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kuhusu kuharibiwa kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, kutumika kwa Polisi kuipa kura na Majaji kutotenda haki kwa kuwa ni wateule wa Rais.

Hata hivyo Mahakama hivyo ilisema haina uwezo wa kusikiliza makosa ya uhaini na kuhairisha kesi mpaka leo April 24, 2024.

Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limepiga marufuku wananchi kwenda Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Hapo sawa hakuna visingizio
 
Back
Top Bottom