PreGE2025 Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

PreGE2025 Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wameisha sema chadema wamemuomba Raisi aifute na pia Nchimbi kasema Wana siasa wapende kuomba Radhi - ndio njia ya kutokea
Kwahy wanamlaumu rais kwa kumkamata Lissu afu hapo hapo wanamuomba wamuachie 😂
 
Napoteza muda na i.d.i.o.t take ur time
Yan ww huna tofauti na polisi, mnawalaunu polisi kutumika na serikali ya ccm wakati hapo hapo nawe pia unaifanyia kazi serikali ya ccm 😂
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam Inayoketi Kisutu Shauri la Jinai namba 202504102000008606 Jamhuri dhidi ya Tundu Antipace Lissu mbele ya Mhe. Geofrey Mhini, Hakimu Mkazi Mwandamizi.

Tafadhali tumia kiungo (link) kifuatacho kuendela na shauri ya njia ya mtandao>>> JoT - Virtual Court

Shauri limepagwa kwa usikilizaji wa awali leo 24/04/2025 saa tatu asubuhi. Hii ya Uchochezi
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, Tundu Lissu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka la uhaini.

Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la uhaini Wakili Nassoro Katuga.

Mbali na Shitaka hilo anatuhumiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kuhusu kuharibiwa kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, kutumika kwa Polisi kuipa kura na Majaji kutotenda haki kwa kuwa ni wateule wa Rais.

Hata hivyo Mahakama hivyo ilisema haina uwezo wa kusikiliza makosa ya uhaini na kuhairisha kesi mpaka leo April 24, 2024.

Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limepiga marufuku wananchi kwenda Kisutu kusikiliza kesi hiyo.
Watawala wanaogopa nini sasa kama wana uhakika hayo mashitaka siyo ya mchongo?
 
Hata mimi nina mashaka haya ni maroboti. Haiwezekani wawe wengi mitandaoni lakini kwenye field yupo Heche na Mnyika tu!
Sina shaka hata.

Miaka 15 nawasoma hawa, nina ubao(blackboard) wangu kabisa, nawachora, najua wanavyoingia na kutoka.

Kwanza huyo ana glitch. Lazima aandike posti mbili kwanza....umeona ehhh

Akiona neno CHADEMA tu huyo. Hata kiswahili kajifunzia JF😅🔥🔥🔥
 
Hii ni tactic ya kupunguza watu kuangalia .

Kwani hao vilaza wa mahakama pia hawana YouTube channel ili waweke live stream?

Hiyo link traffic imekuwa kubwa hivyo imejam sio wote wataangalia tayari watawanyima access watu wengi tu.

Kesi ya Gachagua ilikuwa live na yoyote aliyotaka aliangalia kwenye TV au YouTube.

Yanafanya mambo kizamani sijui kumfurahisha nani, yaani ofisi kubwa na teknolojia imekuwa yenyewe bado yapo gizani.


View: https://youtu.be/Hb5TB7Uyamk?si=Pv91jKBuehox60oJ
 
Back
Top Bottom