Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo Mahakamani, ambapo Wadau wa Maendeleo wa Tanzania kutoka kwenye Taasisi za Kimataifa wameshiriki kesi hiyo ya Ugaidi kwa lengo la kujua kinachoendelea, Maofisa hao wengi wao wamefika ili kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo .

Ugaidi katika nchi ni jambo baya linaloweza kuwatisha wawekezaji , hivyo ilikuwa ni lazima wadau wa maendeleo kuhudhuria kesi hiyo ili kupima kiwango cha ugaidi kwa lengo la kulinda wawekezaji kutoka kwenye nchi zao , maana ni hatari kuwekeza kwenye nchi yenye Ugaidi

Just thinking aloud. Mbona kesi ya wale walioambiwa masheikh ya ugaidi hawakutaka kujiridhisha ni kitu gani kinaendelea?
 
Hawa jamaa nilifikiri baada ya kuwalegezea msimamo wetu juu ya corona ndio watukuwa wameridhika. Mbona chokochoko zao tena wakati tumeamua kuenda na dunia inavyoenda.?!

Labda mtawawini kwa kutangaza hadharani kuruhusu ushoga maana hiyo nayo ni sehemu ya kwenda na dunia inavyoenda.
 
Mwaka huu utaangaika sana na kujaribu kila neno unalofikiri linavuta attention ya watu, lakini ni kujilisha upepo. Watanzania tunapuuza sana mambo ya Chadema na pia tunakupuuza sana posts unazoleta humu.
Sasa kama unapuuza/mnapuuza,wewe mbona umejibu?!
 
Hiyo kesi inakwenda kufutwa. Kitendo cha hao wadau wa maendeleo kwenda mahakamani leo ilikuwa sawa na kutuma ujumbe Serikalini kwamba hawapo na Serikali bali wapo na Mbowe.

Mwenye akili yeyote atajitafakari. Na ikitokea hii kesi ikafutwa, itakuwa aibu kubwa kwa Mkuu wa Nchi. Ingebaki kuwa aibu kwa IGP na Polisi wake, lkn yale mahojiano ya BBC yamehamishia fedheha hii upande wa juu zaidi.

Lkn ni heri nusu shari kuliko shari kamili. Kesi itafutwa, IGP ataondoka. Maisha yanaweza kuanza upya.

Uwezekano wa Warioba kuitwa kazini upo wazi.. ikishindikana, itakuja kuwezekana tukiwa tumechelewa.

Nashauri Chama changu kitumie HEKIMA YA MWALIMU NYERERE MIAKA ILE YA 90!
hakuna kitu kama hicho hao walienda kuchungulia tu kama wachunguliaji wengine hawawezisema lolote
 
KESI IMEFIKA PATAMU, SASA DUNIA YOTE ILIYOKUWA HAIFAHAMU MATENDO YA CCM YA AWAMU YA 5 NA YA SASA YA AWAMU YA 6 YATAANIKWA NA KUFAHAMIKA KINAGA UBAGA

Kesi hii ya Mbowe itakuwa ktk vitabu kama kesi ya serikali ya makaburu dhidi ya Nelson Mandela. Kesi hii itasomwa ktk historia baada ya CCM kungolewa kutoka madarakani kwa kupitia uchaguzi huru kama kesi ya : Mpinzani Freeman Mbowe ndani ya 'mahakama' za CCM. ifahamike katika mabano neno 'mahakama' ni kuwa CCM inataka kuburuza Mahakama zitumike vibaya pamoja na mfumo wa kusimamia / kuchunguza za jinai (criminal justice system) nzima, lakini imani yetu bado ipo kuwa Mahakama hapa bila "mabano" ni mhimili huru na itatenda haki na kukataa mbinyo wa aina yoyote ile toka upande wowote.

Historia inasema makaburu waliokuwa ktk serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini iliona waAfrika raia wengine waliokuwa wanadai kuwa watu-uhuru, kutaka demokrasia shirikishi na Marndeleo ya watu wote walikuwa ni hatari na wangeweza kuchelewesha maendeleo ya vitu kama madaraja, reli, flyovers pamoja ni miradi mingine mikubwa iliyokuwa ya mfano barani Afrika. Madai hayo ya serikali ya kibaguzi ya wachache ya miaka hii yanarudiwa na CCM miaka hii ya 2015 - 2025. Na CCM pamoja na serikali yake kudai wapinzani ni watu hatari wasio na uzalendo na wasioitakia Tanzania maendeleo.

Soma utetezi wa Nelson Mandela alipofikishwa mbele ya korti na utetezi huo wa Nelson Mandela kuenziwa na watu wote duniani na taasisi kubwa za kimataifa na vyuo vikuu vijana kufunguliwa macho juu ya tawala kandamizi za kibaguzi, katili na vinazokandamiza utu wa watu na haki zao kwa kisingizio cha kujenga uchumi, madaraja, flyovers, mabwawa ya umeme n.k
1628856318510.png


2878995_images_9.jpeg
 
Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo Mahakamani, ambapo Wadau wa Maendeleo wa Tanzania kutoka kwenye Taasisi za Kimataifa wameshiriki kesi hiyo ya Ugaidi kwa lengo la kujua kinachoendelea, Maofisa hao wengi wao wamefika ili kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo .

Ugaidi katika nchi ni jambo baya linaloweza kuwatisha wawekezaji , hivyo ilikuwa ni lazima wadau wa maendeleo kuhudhuria kesi hiyo ili kupima kiwango cha ugaidi kwa lengo la kulinda wawekezaji kutoka kwenye nchi zao , maana ni hatari kuwekeza kwenye nchi yenye Ugaidi

Wewe Dada una Mambo,maofisa wepi hao,nilidhani mabeberu Kumbe ngozi nyeusi,beberu halina muda wa kufanya bageining na gaidi,Mbowe is gone!!!!
 
Je walisemaje walipoambiwa haletwi Leo mahakamani kwa sababu magari ni mabovu?
Tabia ya jeshi la police kuniaribia nauli yangu kwa visingizio vya ajabu ,eti magari mabovu kumleta mwamba , sio kwamba mnakandamiza haki za mh Mbowe bali pia mnavunja haki yangu,

IGP unamagari MANGAPI ? Mpaka gari la kumleta mh Mbowe mahakamani likose? Endeleeni na janja janja ila yana mwisho
 
Kipindi cha jk kesi kubwa ubakaji !
Kipindi cha magufuli kesi kubwa hujumu uchumi !
Kipindi cha SSH kesi kubwa sasa ugaidi !

Hii nchi bwana
Halafu samia kawatoa wazanzibara wenzake, kaanza kuwatesa watanganyika...
 
Watu weupe wamekuwa ndio kimbilio la weusi na waarabu wanaoteswa na ndugu zao.
Hii dunia Ingekuwa ni mwafrika na mwarabu pekee hakika isingekalika.
Mwafrika roho mbaya mwarabu katili.
Unashindwa kuelewa hao watu weupe wazungu ndio wanaounda matatizo ili msiwe stable.
Unashindwa kuelewa kipindi mwarabu unaemwita katili Gaddafi alipotaka kuifanya Afrika ijitegemee wazungu unaowatukuza wakamuua.
Unashindwa kuelewa hao wazungu wanakutawala kikoloni mambo leo.
HII DUNIA MZUNGU NDIO KAIHARIBU KILA KONA.
MWARABU UNAEMWITA KATILI KAKUPA MISAADA MINGI HAPA TZ KWA TAASISI ZAKE KM OIC,TIF N.K N.K HAO WAARABU UNAOWAITWA MAKATILI WAMEKUSAMEHE MADENI NA WAMEKUKOPESHA BILA RIBA.
TAFITI MAMBO USIMEZE PROPAGANDA.
 
Kipindi cha jk kesi kubwa ubakaji !
Kipindi cha magufuli kesi kubwa hujumu uchumi !
Kipindi cha SSH kesi kubwa sasa ugaidi !

Hii nchi bwana
Akija Rais Mpya Askofu Gwajima naye kesi kubwa zitakuwa ni za kujirekodi tukinyanduka! 😁 Thithi idhi Tanzania bhana!!
 
Hayo si maandamano aliokataza IGP Sirro??? Mbona vijana wa IGP Sirro wamejikausha hawaja wakamata sasa wala kuwatawanyisha na mabomu ya machozi???

Halafu utakuta hata huyo huyo IGP Sirro ametoa mpaka escort ya police na ulinzi kwa wahusika wa haya maandamano. Aibu ilioje hii.

Ama kweli wahenga walisema "Debe lililo tupu, ndio lenye kelele zaidi". Kelele zote, Vitisho Vyote, Vitimbi Vyote, Uonevu Wote na Kutunishiwa misuli wanafanyiwa wanyonge wasio jiweza na wasio na nguvu ya kujitetea tu nchi hii.
Hao wana diplomatic privileges na diplomatic immunity
 
Back
Top Bottom