Kisutu: Mahakama yatupilia mbali hoja za Meya wa Dar es Salaam kutaka asalie madarakani, yasema hoja za mwombaji hazina miguu ya kusimamia

Huyo akatafute kazi nyingine asilete ujuaji mwisho akalala mlupango na Mahakama imeshaitupilia mbali kesi yake!

Wee ni poyoyo tu unayeshabikia upumbavu huu wa ukiukwaji wa sheria na taratibu za Utawals bora!
Hivi huyu Mhe.Mwita angelikuwa ni wa CCM tungeshuhudia huu upumbaf unaoendelea hapa? Makosa yote ni maigizo tu ili kujustify huu uhuni!
Jiulize kwanini Tume ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Mstahiki Meya Mwita imeundwa na RC Paul Makonda…!
 
Huyu hakimu anafikiri kwa kutumia kile kitu cha kati. Huwezi kuwa na ubongo ukasema hakuna hasara atakayoipata! Tumuulize mbona kumpindua Rais ni kosa la jinai? Kwani akipinduliwa rais anapata hasara gani? Kile cha kati kinafikiri kweli!
 
Naombeni kujuzwa utofauti uliopo kati ya watu hawa; mwanasheria, wakili na hakimu.
 
Lakini pia mahakama ipo sahihi sana kusema,haiwezi kuzuia kikao cha kumuondoa kwa sababu hata akiondolewa hapati hasara yoyote!! Hapo ndo nimepapenda kweli..!! Kwani mwita anapata hasara gani akiondolewa kuwa MEYA!.?0
Uchu tu wa madaraka
Jana kapanda bajaji kawahi ofisi halafu kajipiga mapicha eti yupo ofisini
Kuna maana gani kukaa ofisini kazi haziji,na saini zote zimeshaondolewa benki
 
Nimesoma na kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa akidi haikutimia wakati wa kumuondoa Mstahiki Meya wa Dar es Salaam. Kuna sheria taratibu za kumwondoa Mstahiki Meya yeyote lakini kama sheria, taratibu na kununi hazikufuatwa mimi naona waanze mchakato upya. Mstahiki Meya atakapoenda Mahakamani na akasikilizwa na sheria zikafuatwa basi Mstahiki Meya atawabwaga chini. Ninashauri sheria, taratibu na kanuni zifuatwe kumuondoa Mstahiki Meya madarakani.
 
Kama ni kweli basi Mkurugenzi ataonekana kituko kuongoza kikao cha maamuzi ambacho akidi haijafikia
 
Hakika inashangaza sana kuona Upigaji kura wa kutokuwa na imani na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam ukigubikwa na vurugu na kugushi jina na saini ya Diwani aliyopo nje ya nchi lakini Waziri mwenye dhamana na Tamisemi akiwa kimya.Ni vema suala hilo likatolewa ufafanuzi wa kina na Waziri ili kuondoa Sintofahamu iliyowakumba Wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ilitoa kesi ya hawali ya meya kuwa na hofu kuondolewa.hapakuwepo na ushaidi ulionyesha kuwa meya walitaka kumuondoa.Yeye bado ni meya kwa kuwa hata hii waliyo kaa kikao cha kumuondoa kwa nguvu kimekiuka kanuni na sheria kwa kuwa hakukidhi idadi ya wajumbe ya 2/3
 
Mpango mkakati wa shetani bado unaendelea kutamalaki ktk nchi ya Mungu, tusali na kuomba sana kwani hakuna aliye salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…