Kiswahili cha Kisiasa Kwa Watanzania: Ikulu sio Eneo Specific, ni Makazi ya Rais, Tuna Ikulu ya Magogoni, Chamwino, Sasa Hadi Ikulu ya Chato!

"kwa sisi ambao ka Kolona ni kaugonjwa kadogo ambacho hakatishi na tusitishane, hatuwezi kukuambia ka Kolona!"

Mkuu Paskali, kwa mtu ambaye hukurupuka tu kusoma maandishi yako bila ya kutuliza akili yake, hataweza kamwe kukuelewa na kuishia kukulaumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu P,
Sikubaliani na wewe kwamba ikulu ni pahali popote Raisi atakapoamua kufanyia kazi. Ikulu si Raisi au jengo peke yake. Bali Ikulu ni jengo na wafanyakazi wa jengo. Raisi hafanyi kazi peke yake, Raisi ni taasisi na ana vyombo vyake na vinafanyia kazi sehemu au maeneo maalum. Vyombo hivi vimeratibiwa na kupangiwa maeneo au sehemu za kufanyia kazi, kati ya maeneo hayo Chato haijawahi kuwemo au kuthibitishwa kwamba ni eneo moja wapo. Raisi kama individual ni muajiriwa wa ikulu, au niseme wa hayo maeneo ya kazi zake.

Ila ikiwa utasema kama Raisi wetu ameamua kufanya kazi akiwa nyumbani kwa kuwa yumo katika wale wanaotajwa kama 'covid-19 vulnerable groups' na katika mazingira haya ya sasa ya hali ilivyo hasa Dar es Salaam, niseme tu katika hali hio hakuna ubaya. Ila hili nalo lingeekwa wazi tu kwetu ili tujuwe kwamba Raisi wetu anafanyia kazi nyumbani kwa sasa!
 
Si uhakika kama umeisoma hii post mpaka mwisho kabisa..Umeishia kichwa cha habari basi...Kumbe wilaya ya Chato ina Ikulu ndogo...Pascal nilikua sijui ili
 
. Mkuu Pasco. Asante. Naomba niweke sawa. Kuna ikulu (state house) ambayo ni mali ya serikaii kama Chamwino. Kuna nyumba ya mapumziko au rest house au ikulu ndogo ambayo ni mali ya serikali lkn pia kuna nyumba ya kuishi anayokaa mtu awe rais au vingine. Hii ya Chato ina hadhi gani?
Z
 
Rais na amiri jeshi mkuu, dunia IPO katika vita dhidi ya Corona, TZ pia ikiwemo. Vita hivi ni dhidi ya adui asiyeonekana bali madhara yake. Moja ya sifa za Rais ni kuilinda katiba ya nchi na kulinda uhai wa RAIA awaye yeyote dhidi ya majanga na vita kwa gharama yoyote ile kwani amekabidhiwa hiyo dhamana.

Anapaswa kuingia katika uwanja wa mapambano kwa kuhamasisha na kutoa amri na makatazo yatakayolinda RAIA wake dhidi ya huyu adui. Ikulu ya Chato itatumika tu pale Rais akiwa mapumzikoni na kwa nn aende ajifungie huko wakati huu ambao nchi inamuitaji kuliko wakati mwingine wowote.

Hapa ndipo alipofeli na usitetee kisa huu ni mwaka wa uchaguzi unajitahidi kupalilia njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal, nadhani kuna mahali umekosea. Kwa tafsiri mpya kwa kadiri ya kamusi ya kiswahili, 2020 version, Ikulu ya Rais ni mahali popote atakapokuwepo Rais. Kwa hiyo Ikulu inatembea na Rais.

Kama ikitokea Rais wetu akawa Lilongwe au mjini Gitega au Uvira, basi automatically, wakati Rais yupo huko, na Ikulu itakuwa huko. Tanzania statehouse is not static, it is dynamic, can change its location depending movements of the President.

Tatizo kubwa ni kubwa watanzania wengi hawajibidishi kusoma ili kuweza kuelewa hizi tafsiri za kisasa za lugha ya Kiswahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujamwelewa kabisa. Rudia kusoma tena, utaelewa anachotaka kusema Pascal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal, watanzania wengi elimu ya uraia inatupiga sana chenga, kwenye ziara nyingi za Rais neno ikulu ndogo ni la kawaida, kwani hawa vijana hawasikilizi hata taarifa za habari wala kusoma mitandao yenye habari za uhakika?.Utakuta mtu anabisha na kushupaa kwa mambo aliyopaswa kujua kwenye uraia wa kidato cha pili, kama sio darasa la sabab na sita.
 
Hujamwelewa kabisa. Rudia kusoma tena, utaelewa anachotaka kusema Pascal.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umetumia kipimo gani kutambua kwamba sijamuelewa Pascal?

Wewe ndiye Pascal? au unataka kusema ubongo wako na wa Pascal unafanana namna ya kufikiri?

Ulitaka nimjibu kama unavyofikiri wewe?

Ningekuwa sijamuelewa nisingejibu hoja yake na ndiyo maana hata yeye mwenyewe ameonesha appreciation kwenye hoja yangu.

Hakika wewe ndiyo hujaelewa maandishi yangu mkuu. Soma tena usipoelewa nitakufafanunulia vyema mkuu.
 
Common sense and reason... nadhani wewe siyo msomi!
Wewe ulieqt from wikipedia ukadhani ndio concrete supportive qt ya uongo wako ndio Msomi??
Barudia Wikipedia MTU yeyote aweza edit akawea updates bila kujali anapotosha ama lah #Rudishulendugu
 
Wewe ulieqt from wikipedia ukadhani ndio concrete supportive qt ya uongo wako ndio Msomi??
Barudia Wikipedia MTU yeyote aweza edit akawea updates bila kujali anapotosha ama lah #Rudishulendugu
common sense and reason!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…