Kiswahili fasaha kinatoweka

Hili jambo nilijalibu kulifatilia sio kwetu tu tunaobadirisha maneno ata nchi za wenzetu pia iko hivyo hivyo basi mgeni akija anafunzwa kiswahili fasaha wazawa tunabaki na mityevengo kuosea tu 😂😂😂
 
si afadhali hata hiyo mifano uliyoonyesha,wewe angalia matumizi mabovu ya lugha waliyonayo asilimia 80 ya Watanzania,hivi Sasa hawaongei kiswahili sanifu,hasa kwenye matumizi ya viambishi
utakuta awe kiongozi wa nchi, Mwalimu,anayejiita mwanaharakati wa lugha, waandishi na watangazaji wa habari ni kuboronga na kubagaza kwa kwenda mbele
kiambishi Cha wakati uliopita kutumika kwa wakati uliopo
mambo kama

aliyepo badala ya aliye
aliyekuwepo badala ya aliyepo
iliyokuwepo badala ya iliyopo

yaani matumizi ya viambishi vya wakati uliopita kwa wakati uliopo yameshamiri kwa asilimia 80 ya Watanzania na inaonekana ni jambo la kawaida
kwa kweli kiswahili kipo Gizani
 
Mpaka tuseme😂
 
Vyombo vya habari vinavyoongoza kutumia kiswahili fasaha ni ITV na Radio One.

Radio One walianzisha hadi kipindi cha Kiswahili asubuhi jumamosi, nadhani muasisi alikuwa Julius Nyaisangah (marehemu hivi sasa), akaja kukiendeleza kipindi Regina Mziwanda ambaye yupo BBC hivi sasa. Pia Regina aliendeleza hii hadi Clouds, ndio akarithi Mwihava ndio huwa unamsikia Mwihava akimuuliza muuliza maswali Oni Sigala.

Kuonyesha = kuonesha.

Kuonesha = kuona

Kuonyesha = kuonya.

Masaa = saa
 
Bado hujasikiliza vipindi vya burudani kwenye media

a go bai ze nem, the mvp, twissaa 😁
 
Usanifu wa Kiswahili katika mazungumzo ni nadra sana,kupata matamshi sahihi ya sarufi ya Kiswahili kunahitajika umakini ulio toshevu kwa wenye kuifahamu lugha.
 
Hata wewe unakosea.

Ndiyo = ndio
 
kuna neno linapendwa hilo

KUDADAVUA

wakimaanisha kufafanua. hata viongozi utasikia wanatumia. sijui ni kiswahili cha wapi
 
Katika mchakato wa kusanifisha Lugha ya Kiswahili,Wakenya walipinga sana lahaja ya kiunguja kuwa ndo lahaja ya usanifu wa Kiswahili,nadhani kasumba hii ndo sababu wao kutumia lahaja zao hasa kilamu.
 
Mwanamke anayeandika
axante = asante
tantee = asante
xawa = sawa

Na mengine ya aina hiyo aise huo upuuzi siwezi kuuvumilia, imenibidi na mini niwe mpuuzi kuandika hivyo ili niwaambie.
kuna kajomba kangu hako kanapenda kuandika hivyo yaani hadi inakera.
 
Wale jamaa wa kanda ile nao wamechangia kwa haya:
Sipendi-Sipendagi mf.Mimi sipendagi hayo mambo!
Kwenda-Kwendaga mf.kule tunakokwendaga!
 
Hapa umeandika au umeongea au umesema?
Kiswahili kibovu kabisa. Mleta uzi kauandika ule ukweli wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…