si afadhali hata hiyo mifano uliyoonyesha,wewe angalia matumizi mabovu ya lugha waliyonayo asilimia 80 ya Watanzania,hivi Sasa hawaongei kiswahili sanifu,hasa kwenye matumizi ya viambishi
utakuta awe kiongozi wa nchi, Mwalimu,anayejiita mwanaharakati wa lugha, waandishi na watangazaji wa habari ni kuboronga na kubagaza kwa kwenda mbele
kiambishi Cha wakati uliopita kutumika kwa wakati uliopo
mambo kama
aliyepo badala ya aliye
aliyekuwepo badala ya aliyepo
iliyokuwepo badala ya iliyopo
yaani matumizi ya viambishi vya wakati uliopita kwa wakati uliopo yameshamiri kwa asilimia 80 ya Watanzania na inaonekana ni jambo la kawaida
kwa kweli kiswahili kipo Gizani